Kupanda kwa bei za Mafuta, Serikali inadanganya

Kupanda kwa bei za Mafuta, Serikali inadanganya

Your concern has been noted,thanks.Niseme hivi sasa, nchi yetu imekuwa ya ajabu sana.Si viongozi wakuu si wakaida,wote wamekuwa wachumia tumbo.Nani sasa atamuwajibisha mwingine?Bad times indeed for the 99%.
Mpaka wananchi watakapo pata akili ndiyo tutapata maendeleo lakini siyo kizazi chetu labda baada ya miaka 200
 
Mpaka wananchi watakapo pata akili ndiyo tutapata maendeleo lakini siyo kizazi chetu labda baada ya miaka 200
Hatutafika huko mkuu,we know what is going on.Infact hata 2030 itakuwa bahati.Na hata kama tungeweza kufika 2050 kwa mfano,the situation will be worse,because again,we know what the plans are for humanity.
 
Mlikuwa mnafurahia Wakenya kuja kununua mafuta kwetu kisa kwao mafuta yako juu sana
Mkauza mpaka wajanja wakaona ni fursa na mafuta kuadimika na mengine kufichwa na kuuza bei wanayotaka wao

Sasa marope anasema $ ndio sababu yaani the whole government hawana akiba ya $
Tumelalamika sana tuwe na akiba ya fedha za kigeni na tuwe na akiba kubwa ya dhahabu lakini wajanja wanapiga bila aibu

Wachawi wanajulikana
 
Swali rahisi Tu ..je nchi zote kuna ewura inayo tangaza bei?
Wenzetu kama Kenya na wengine wanafanyaje ?


The best solutions ni kuwa na kampuni moja kubwa ambayo ni public listed...

Bado unaendeleza ujinga wako, huelewi athari ya kukosekana kwa dollar ilivoathiri uchumi kama ulivojibu kijinga kule kwenye thread yangu, umeona wenye akili wamesema nini? Unakalia ushabiki lakini elewa kiufupi mna kiongozi mbovu asieweza kudhibiti uchumi wa nchi yake, na haujui hata black market za mafuta deepsea zinafanya nini! Ajabu kwelikweli kua na watu vilaza mfano wako
 
Kazi ya ccm ni kushabikia ujinga kujifafanua kidunia na kutatua changamoto kwao ni ndoto
 
CCM imeshindwa kuleta maendeleo ya kweli hawafai kuongoza nchi hii kwani hawana mipango madhubuti
 
Nchi wahuni wengi, wakisikia tetesi bei ya mafuta inapanda basi wiki nzima mafuta yanapatikana kwa tabu.Ewura wa kitangaza bei mpya saa sita siku ya siku inayo fuata mafuta ya naanza kupatika kwa wingi sana.Yaani wafanyabiashara mafuta wanafanya watakavyo.

Bi mkubwa anacheka na ndezi,waziri nae mmmmhhhhhh.......... anabebwa na jina la mzee wake, yaaani tabu tubu. Tujiandae na mfumuko mwengine wa bei za vyakula,kwani wafanyabiashara wa vyakula lazima hili biti la uhaba wa dola na ongezeko la mafuta lazima wapite nalo,japo kipindi hiki chakula kipo kingi.
 
Nchi wahuni wengi, wakisikia bei ya mafuta inapanda basi siku hiyo wiki nzima mafuta yanapatikana kwa tabu.Ewura wa kitangaza bei mpya saa sita siku ya siku inayo fuata mafuta ya naanza kupatika kwa wingi sana.

Bi mkubwa anacheka na ndezi,waziri nae mmmmhhhhhh.......... anabebwa na jina la mzee wake, yaaani tabu tubu. Tujiandae na mfumuko mwengine wa chakula,kwani wafanyabiashara wa chakula lazima hili biti la uhaba wa dola na ongezeko la mafuta lazima wapite nalo,japo kipindi hiki chakula kipo kingi.
Kazi sana dahh!!
 
Swali rahisi Tu ..je nchi zote kuna ewura inayo tangaza bei?
Wenzetu kama Kenya na wengine wanafanyaje ?


The best solutions ni kuwa na kampuni moja kubwa ambayo ni public listed...
Unamawazo mazuri sana je Samia anasoma hapa kweli?
 
Hata tuseme vipi? Hakuna litakalo fanyika. Maana hata hawa wabunge wa mchongo wakitaka kulizungumzia bi betina atazuiaisizungumziwe kwa sababu mume ndie boss wa ewura.
Bado narudi kwa Mama, amekuwa akidanganywa na kubeba familia hata pale panapo onekana kutakuwa na conflict of interest ..
Shid kiongozi nahis tatzo ndio linanzia hapo na
 
Kiukweli siwezi soma li post lirefu hivi ila nadhani mfumuko wa Bei ya mafuta haupo Tanzania tu
Shida mkuuu imeazia tu pale ww uliposhindwa kusoma anadiko huo ni uvivu ndio maaana umeandika kias rahis sana mkuu au ww ni unafaidika na mfumuko huu ?
 
Utangulizi
Tarehe 2 Agosti 2023 Serikali kupitia Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza bei mpya za mafuta ya petroli, diseli na mafuta ya taa. Taarifa hiyo imeonyesha kupaa sana kwa bei za mafuta kiasi cha kuzua taharuki na manungúniko miongoni mwa wananchi.

Taarifa inaonyesha bei za rejareja za petroli zimeongezeka kwa shilingi 463 (sawa na asilimia 16.9) kutoka shilingi 2,736 mwezi Julai hadi kufikia shilingi 3,199 mwezi huu (Agosti). Bei ya Diseli imeongezeka kwa shilingi 391(sawa na asilimia 15.3) kutoka 2,544 mwezi Julai hadi kufikia 2,935 mwezi huu kwa Dar es Salaam.

Bei hizi mpya zimeibua wasiwasi mkubwa hasa hasa katika kupandisha gharama za maisha na kuongeza kasi ya mfumuko wa bei ya bidhaa muhimu. Serikali kupitia Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) katika taarifa yake imeeleza kuwa mabadiliko ya bei yanatokana changamoto za upatikanaji wa dola za Marekani; mabadiliko ya sera za kikodi; ongezeko la gharama za mafuta katika soko la dunia (FOB) na gharama za uagizaji (premium).

Uchambuzi wa hoja na hali halisi ya gharama ya mafuta. Chama cha ACT Wazalendo tumepitia hoja zote zinazoelezwa kupelekea kupaisha kwa bei hizo ili kuona kwa kiasi gani zimechangia kwenye bei ya mafuta kwa kila lita moja ya Petroli na Diseli hadi kufika bandari ya Dar es Salaam. Uchambuzi wetu umegusia gharama halisi ya mafuta ya petroli, dizeli na mafuta ya taa katika soko la dunia (FOB); gharama za usafirishaji (premium); kodi na tozo za Serikali na gharama & faida za wafanyabiashara.
Kutakana na utafiti na uchambuzi tulioufanya tumebaini masuala yafuatayo;

Serikali kupitia EWURA imedanganya kuhusu ongezeko la gharama za Mafuta katika Soko la dunia. Mafuta yanayotumika mwezi huu (Agosti) ni yale yaliyoagizwa kwa bei ya soko la dunia ya mwezi Juni. Katika uchambuzi wetu tumeona kuwa gharama za mafuta katika Soko la Dunia kwa kipindi cha Mwezi Mei, Juni na Julai kwa kila lita moja ya petroli mwezi Aprili ilikuwa dola ya Marekani 0.53 (Tsh 1,311.7) kwa mwezi Mei ilikuwa dola ya Marekani 0.47 (Tsh 1,163.2) na Juni dola ya Marekani 0.47 (1,163.2) kwa mantiki hii bei ya mafuta katika soko la Dunia imeshuka na sio kupanda kama taarifa ya Serikali kupitia EWURA ilivyoonesha

Gharama za uagizaji wa Mafuta, katika Uchambuzi wetu tumebaini kuwa Gharama za uagizaji Mafuta kwa kipindi cha miezi mitatu hazikupanda bali zimeshuka. Taarifa za zabuni zinaonyesha gharama zilizotumika kuagiza mafuta kwa mwezi Juni zilikuwa dola ya Marekani 0.11 (Tsh 274.45) kwa lita Moja ikilinganishwa na bei ya mwezi Mei na April ambazo zilikuwa Shilingi 474 (dola ya marekani (0.19) na shilingi 499 mtawalia. Hivyo, basi mchango wa wa gharama za uagizaji (premium) sio hoja kubwa.

Changamoto ya Uhaba wa Dola za Marekani, ni kweli nchi yetu inakabiliwa na uhaba wa dola za Marekani ambayo ndiyo Fedha inayotumika katika kufanya manunuzi na uagizaji wa bidhaa za nje (importation) ikiwapo mafuta, changamoto hii ni kubwa sana kwani uhaba wa Dola za Marekani Una athari kubwa sana kwa taifa utakwenda kuathiri kwa kiasi kikubwa Uchumi wa Taifa na uchumi wa mtu mmoja mmoja, Uhaba huu unatokana na Kukosekana kwa uwiano wa urari wa kibiashara (balance of trade) kati ya mauzo ya nje na uagizaji wa bidhaa na huduma kutoka nje (import and export), katika mwaka wa Fedha 2022/23 Mauzo ya nje yalikua Dola bilioni 12 na Mnaunuzi yalikua Dola Bilioni 16, nakisi ni Dola za kimarekani bilioni 4 ambayo haijawahi kutokea nakisi kubwa namna hii kwa miaka ishirini (20) kadiri nchi inavyouza nje ndivyo inaongeza hifadhi ya Fedha za kigeni (Foreign reserve) na kadiri unavyonunua Zaidi unapunguza hifadhi na kusababisha kupungua kwa uwezo wa Taifa kuagiza bidhaa.

Kuongezeka kwa kodi ya mafuta, katika bajeti ya mwaka huu Serikali imeongeza shilingi 100 katika kila lita moja ya petroli na Diseli. Athari za uamuzi wa Serikali kuongeza kodi kwenye kila lita moja ya mafuta ndio imeanza kuumiza wananchi.

Serikali kusitisha kutoa Ruzuku ya mafuta kwa petroli na Diseli. Licha ya changamoto hii Serikali imeondoa ruzuku ya mafuta ya Petroli na Dizeli iliyokua ikitolewa kuanzia Agosti 2022 ili kupunguza makali ya bei na kuleta nafuu kwa walaji, hivyo Serikali imeondoa ruzuku na kuongeza ushuru katika Petroli na Dizeli.

Kushuka kwa thamani ya Shilingi dhidi ya Dola, thamani ya shilingi ya Tanzania inaendelea kuporomoka kwa kasi Agosti 3 mwaka 2022 Dola ya moja ya kimarekani ilikua sawasawa na shilingi za kitanzania 2,315.00 lakini mpaka kufikia agosti 3 mwaka 2023 Dola moja ya kimarekani ni sawa na Shilingi za kitanzania 2,545.00 ongezeko la shilingi 172.24 sawa na asilimia 10 kwa kipindi cha mwaka.

Hii ni hatari sana kwani itatubidi kutumia fedha nyingi sana kunua bidhaa nje, hali itakayosababisha bidhaa hizo kupanda bei (mfumuko wa bei) kama Mafuta (nishati), Mbolea na bidhaa za chuma ambazo tunatumia gharama kubwa kuagiza bidhaa na huduma hizo.

Kuhusu Uhaba wa Mafuta katika baadhi ya maeneo nchini, Kumekua na malalamiko ya uhaba wa mafuta ya petroli Dizeli na Mafuta ya Taa katika maeneo mbalimbali nchini kama vile Kagera, Katavi, Manyara na baadhi ya maeneo Mkoani Lindi, EWURA ilitoka hadharani na kusema kwamba ni njama za baadhi ya wafanyabiashara kuficha bidhaa hiyo ili kusubiri bei ipande waingize sokoni, Tunaona ni muhimu sasa EWURA ijitafakari upya kuhusu utekelezaji wa mamlaka yake ili Wananchi wa maeneo husika wasiendelee kupata taabu ya uholela wa kupanda bei na kukosa huduma.

Hivyo basi, kupanda kwa gharama za bei ya mafuta nchini kumetokana na Serikali kuondoa Ruzuku kwenye mafuta ya Petroli na Dizeli, Serikali kuongeza ushuru wa Shilingi 100 kwenye kila lita ya Dizeli na Petroli na kuporomoka kwa thamani ya Shilingi dhidi ya Dola ya Marekani kutokana uhaba wa dola.

Tunataka hatua zichukuliwe;
Katika uchambuzi wa bajeti ya Serikali kuu kwa mwaka 2023/24 tuliitaka Serikali kuchukua hatua za haraka katika kupunguza matumizi ya fedha kuagiza bidhaa na huduma nje ya nchi. Hatua hizo ni mwafaka zichukuliwe sasa ili kunusuru nchi kuingia kwenye hali ngumu zaidi.

1. Hatua za kupunguza uagizaji wa bidhaa na huduma nje ya nchi
(i) Serikali ianze kutekeleza matumizi ya nishati mbadala (gesi asilia). Kwa kuanzia Magari yote ya Serikali yaanze kutumia Gesi asilia (CNG) ili kupunguza kutumia fedha nyingi za kigeni kuagiza bidhaa za mafuta. Pendekezo hili pia litapelekea kupunguza matumizi ya Serikali kwa takribani shilingi bilioni 500 kwa mwaka. Hivyo basi, Bohari zote za Serikali (GPSA) zifungwe mitambo ya kujazia gesi asilia (CNG) mara moja.

(ii) Serikali iweke msisitizo kwenye utekelezaji wa mradi wa Mchuchuma na Liganga ili kuzalisha bidhaa za chuma kwa matumizi ya ndani na nje. Hii itasaidia kuokoa fedha za kigeni zaidi ya Dola za kimarekani Bilioni1.1 ambazo tunatumia kuagiza chuma kutoka nje kwa mujibu wa taarifa za Serikali.

(iii) Serikali iharakishe Mradi wa kusindika Gesi asilia wa Lindi (LNG) na kuufungamanisha na Mradi wa kuanzisha kiwanda Kikubwa cha kuzalisha Mbolea. Hii itasaidia kuokoa Fedha za Kigeni tunazotumia kuagiza Mbolea kutoka nje, ambapo mwaka 2022 tulitumia Dola za Kimarekani Milioni 503.

2. Hatua za mahususi za kikodi

(i) Serikali kupitia Shirika la Maendeleo ya Petoli Tanzania (TPDC) ijenge Hifadhi ya kutosha kutunza mafuta angalau ya kutosha miezi sita ili kama kutatokea mabadiliko ya bei katika soko la Dunia yasiathiri uchumi wetu kwa haraka.

(ii) Serikali irejeshe utaratibu wa kutoa ruzuku ya mafuta kwa petroli na Dizeli hadi hatua zingine za kukabiliana na bei zikamilike na tunarudia wito wetu iweke Ruzuku ya shilingi 500.
(iii) Serikali iondoe tozo ya shingi 100 iliyoanzishwa katika mwaka wa fedha 2023/2024.

3. Hatua za kuongeza uzalishaji na mauzo nje

1. Kuongeza mauzo ya bidhaa za kilimo nje ikiwemo kuongeza thamani ya mazao. Kwa mfano Korosho iliyobanguliwa inaweza kutuletea mpaka Dola za Kimarekani milioni 500 kwa mwaka na Soya (kwa kuuza China) inaweza kuingiza mpaka Dola za Kimarekani Bilioni 1. Hivyo hivyo kwa mazao kama ya Ufuta, Mbaazi, Kahawa na Pamba yanaweza kutuletea Fedha nyingi zaidi za Kigeni kwa kuongeza tija na uzalishaji.

2. Kuweka vivutio katika sekta ya utalii kwa kuongeza matangazo na kuboresha miundombinu ya Utalii ili kuongeza idadi ya watalii maradufu ya idadi ya sasa. Tukifika watalii Milioni 5 kwa mwaka, nchi yetu itapata fedha za kigeni mara tatu ya tunazopata sasa na kuongeza ajira nyingi kwa Watanzania.

3. kuongeza ufanisi katika Bandari zetu ili kufaidika na Uchumi wa jiografia kwa kuongeza idadi ya mizigo inayopita na kutoka nchi jirani maradufu ya tunayohudumia sasa. Sasa hivi mapato ya Fedha za kigeni tunayoyapata kwa huduma za usafirishaji (transit trade) ni Takribani Dola za Kimarekani Bilioni 1.9 tu kwa mwaka 2022 ilihali uwezo wetu ni wa kufikia mpaka Dola za Kimarekani Bilioni 12 kwa mwaka.
Mwisho, changamoto ya uhaba wa fedha una mchango mkubwa sana kwenye kuongeza bei za bidhaa na huduma tunazozinunua kutoka nje.

Ndg. Is-haka Rashid Mchinjita
Twitter: @Isihakamchinji1
Msemaji wa Sekta ya Nishati.
ACT Wazalendo.

Ndg. Ester Akhoth Thomas
Twitter: @esterthomas_1
Msemaji wa sekta ya Fedha na Uchumi
ACT Wazalendo.
05 Agosti, 20223
Najiuliza kitu kimoja. Mimi ni mfanyabiashara, huwa nanunua litre x kwa kwa gharama zote ambazo ni dola y. Kabla sijaanza kuuza, bei ya litre x imebadirika gharama zake kuwa dola z, je, utanipasa bei ya kuuzia ifanane na gharama za dola x au y? Maana nikiuza mzigo kwa gharama za dola x, nitakapokwenda kununua mzigo ukubwa uleule, naamini pesa itakuwa pungufu. Najiuliza tu kama lay person.
 
Kosa kubwa la mama lilianzia hapo kwa makamba,waziri yuko wa wafanyabiashara sio poa
Lakini katiba mpya ndio suluhisho la haya mambo yote. Maana wana takiwa kushtakiwa kwa kutumia madaraka yao vibaya. Huu ni ushenzi kabisa. Yaani hawana huruma na wananchi hawa jamaa.
 
Back
Top Bottom