Kuosha Vyombo

mim nilijua tokea mwanzo ni vyombo vya mezani,niliwashangaeni saaaaana kudhani hili ni fumbo,
Kama ungekuwa ni wewe cheusi umeandika wala nisingekuwa
na tatizo lakini mwanakijiji huwa anatabia ya kuandika maudhi
yenye tungo tata.
 
Muoshee chombo chake na yeye aoshe chako...kesho tena itampa hamu ya kupika nawe...!
 
Hahaha unaona sasa, Mwanakijiji watu wameingia mkenge walikuwa wanatafsiri vingine
MM ni mjanja sana amehisi kitu kinamuvuzishwa mie nahisi ni vyombo vilevile vinavyong'ang'aniana na mwili hahaha....we unaonaje
 
Haoshi mtu vyombo bana unless muwe ndani ya ndoa changa.Hivi Bishanga kweli na umri huu kukura kakara mara nidondoshe misahani,mara ukoko unimwagikie,lol kwa lipi hasa,najipendekeza kwa nani,ili iweje?

unajipendekeza kwangu!!!
 
Aisee kweli bana. Nisingemtilia mashaka pale mwanzoni nadhani wengi wasingepeleka huko walikozipeleka fikra zao.

Na mimi wala si mchoyo wa ushirikiano. Napika, napakua, natenga, naosha, na kuvipanga vyombo kabatini.

Ooh whaao!!..Wanaume wachache wenye moyo huo wengi wanaogopa kudharaulika na kuonekana wamelishwa juju kwa tafsiri zao:-(

Inaonekana Mwanakijiji hajawahi kusuuza hata kijiko sembuse bilauri!!..ndiyo mana kauliza hili swali
 
Mie wa kwangu tukimaliza kula anaenda kuosha vyombo vyetu wote tuivovitumia sijui wewe
 
Vyombo hivi siyo vile
Vya huku siyo kule
Vya jikoni siyo pale
Vyomo vile vya kulia!

Vyombo siyo vya sirini
Vyombo vile vya mezani
Siyo vya kule chumbani
vyombo vile vya jikoni!

Siyo vyombo vya gizani
Vilivyong'ang'ana mwilini
Vya vyakula vya gizani
Vyenye kuliwa shukani

Vyombo hivi ni sahani,
Na vijiko vya mezani
Sufuria za jikoni
Bakuli za kabatini!

Mlivyonavyo mawazoni
Silo niwaulizeni
Sijui tatizo nini
Mmewaza ya chumbani!

Mkisha kula pamoja
Vitamu tena vya haja
Mtaosha kwa pamoja
Au aoshe mmoja?

Swali nawaulizeni.

M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji)

Yaani kumbe ulikuwa unamaanisha visahani na vibakuli vya chakura. mimi nilifika mbali sana mpaka nikaweka hii scenario lakini sikuweza kupata jawabu

Viombo=Chama
Walaji= Mafisadi kwa ujumla wao
Chakula= Ufisadi

Kwababu chakula huchafua viombo, vivo hivyo ufisadi huchafua chama(viombo), baada ya vyombo kuchafuka ni lazima visafishwe, nani wa kusafisha? ni mapacha watatu tu swali bado linarudi pale pale kwanini mapacha watatu tuu.
 
Vyombo hivi siyo vile
Vya huku siyo kule
Vya jikoni siyo pale
Vyombo vile vya kulia!




Mkisha kula pamoja
Vitamu tena vya haja

Mtaosha kwa pamoja
Au aoshe mmoja?

Swali nawaulizeni.

M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji)
 

...duuu, bado mpo na vyombo?

Chombo hivyo chombo gani kiasi cha kupewa thamani nani akoshe?
kwangu mie chombo thamani yake wakati wa kupakua na kula. Hayo ya
kukosha na kusahaulika kabatini wala hayaniumizi kichwa.

Halafu mnajua umbile la chombo linachangia ladha ya chakula?
Namaanisha, waweza kula usishibe, au mmoja wenu kuvimbiwa.

Chombo!

 
Nafanya kazi na mke wangu na wote tunarudi nyumbani tumechoka...hatuna house girl hivyo twafanya kazi zote kwa kushirikiana.
tunapika kwa pamoja,akiwa anapika mboga basi mie napiga ugali au wali...tukimaliza akiosha vyombo mi nina suuza.
jmosi na jpili sote tupo free.asubuhi ya jmosi ni usafi kwa kwenda mbele na jioni ni mtoko kwenda kusuuza nafsi.
jpili asubuhi ni ibadani na mchana no muvi zaidi na mambo mengine ya wakubwa.
hakuna ubwana wala utwana.
naomba hali hii isitoweke kamwe.
 
1. Wote mlikuwa na njaa.
2. Mkashirikiana wote kupika.
3. Mkainjoi chakula wote.

Kwa sababu process zote muhimu za maandalizi milikuwa wote, so inabidi muhitimishe kwa kuosha wote hivyo vyombo.


Kila mtu si aoshe chombo chake basi!
 
Mkuu wana kondoo walio wengi wameongoka karibuni na bado hawajaanza nena kwa lugha.
Tafadhali watazame nao pia kwani hawataelewa mafundisho haya.
alamsiki
 
Back
Top Bottom