Bachela kujipikia ni kupoteza muda na Pesa

Pantomath

JF-Expert Member
Jan 4, 2019
789
3,230
Tafakari utagundua, kama ni mtu unayetumia mda wako vizuri basi utagundua unapokua unaishi mwenyewe, ukaamua kujipikia iwe kwa mtazamo huuu

1. Ni kitu unapenda kutoka moyoni,
2. Unapoishi hakuna mgahawa karibu
3. Uchafu wa migahawa inayokuzunguka
4. Huwezi kutunza pesa hivyo bora ununue chakula hata ukiishiwa unachakula n.k lakini sio sababu ya Saving.
5. Mgahawani hawapiki chakula kizuri.

Lakini kinyume na hapo kama unaamini una save chochote basi unajidanganya, unapoamua kujipikia basi kwa kujua au kutojua umekubali haya :

1. Kupoteza mda,
Hiki ndio kipengele kikubwa, kuanzia manunuzi/maandalizi, kupika kwenyewe, kuosha vyombo, kusafisha jikoni, kupanga na shughuli nyingne zote zinazofanyika jikoni...

2. Kero za takataka,
Hasa ndugu zangu wa mjini, umepika ushamaliza mambo yako tumbo limejaa, kipengele ukiangalia makololo ya mabaki ya vyakula, hapo ndio unafikiria pakuyapeleka, Nyumba nyingne hazina Waste disposal nzuri, ni timing ifike usiku ukatupe barabarani.

3. Kero ya kucheza na bajeti,
Mda wote wewe kuwaza, unga nusu shilling kadhaa,mafuta nusu bei ile, Sukari kilo sijui sh ngapi, kesho ukienda bei imebadirika unakua mkali..

4. Gharama,
Kujipikia ni gharama, usijidanganye kabisa eti kuna kitu una save, Leo hii unaweza ukaenda mgahawani ukala chakula cha Buku, niambie ni katika mazingira gani utajipikia chakula baadae ukijumlisha mboga, chakula, gas, viungo, Chumvi n.k utakua umetumia chini ya buku? Nipe hio bajeti hapa na kweli iwe applicable.

5. Hasara,
Katika upikaji sio mda wote unachopika unakila chote, kuna kubakia, kuharibika, kuharibu, kuunguza n.k zote hizo ni lost ambazo ukiziweka kwenye mahesabu unazidi kuongeza budget..

6. Ratiba,
Upo sehemu unafanya hili na lile, kichwani unawaza kwenda kugombana na masufuriaa, unalazimika kufunga hata ofisi sababu umekua mfungwa wa kujipikia

Faida za kula mgahawani..

1. Unaokoa mda, hili ndio kubwa, utatumia huu mda kufanya mambo mengine ya msingi
2. Unaokoa pesa, hapa sitii neno
3. Unakua flexible na nini ule, Nyumbani mda mwingine unalazimika kula kitu ambacho kuhutaka sababu tuu ndio kimebaki hutaki kukiharibu
4. Unakua huru na ratiba zako mda ukifika unaenda kula unaendelea na ratiba.
5. Usafi, mda mwingi ndani panakua pasafi, unapofanya usafi ni wakawaida, Kinyume na hapo unatembea njiani vidole vinanuka vitunguu..
6. Unaepuka kero za takataka na maji taka n.k

Katika hayo yote simaanishi ndio usijue kupika, simaanishi usiwe na chombo hata kimoja,

Jifunze kupika, mana hujui na mazingira gani utalazimima kupika..

Nunua vyombo vyote, siku kwa kujiachia ukaona leo na mimi nijipikie, hio pia iko poa

ILA SIO KUA MTUMWA WA MAPISHI..
Pia kwa kiasi kikubwa hapa nazungumzia wale tuliopanga, wale wenye ratiba ngumu, wale tunaoishi mijini,

Familia au mpo zaidi ya mmoja kupika yaweza kua options nzuri, Pia katika hili Sijalenga wanawake.

Niko tayari kukosolewa na kurekebishwa kwa hoja itapendeza.

Najua ni maisha yako, Sijakupangia namna ya kusihi, ni mtazamo tuu.

Bachelor Pika For leisure.
 
Kila nipatapo nafasi ya kuwa nyumbani Huwa napenda kujipikia michemsho sana sana siku ya ijumaa au jumamosi, huwa na enjoy sana, ila nikiamka na hangover inabidi nikimbilie chimbo la mama jane nikatwange mtori au supu nzito sana.

NB: Sijawahi kuridhika na ugali wa bar haswaa pale ninapoagiza kitimoto, kama nina hamu ya kitimoto ni bora niifunge tu ili nikapike ugali wangu nyumbani hata iwe saa 8 usiku. Mbinde ni kwenye kuosha vyombo, sufuria inaweza kaa hata siku 3 bila kuoshwa
 
Umeniibia ratiba yangu mkuu...nami napita humo humo
 
Kuna vitu unafanya halafu siku ukakaa ukatafakari utaona ulichagua njia isiyo sahihi kabisa....

Unapokua unaishi mwenyewe, ukaamua kujipikia basi labda iwe kwa mtazamo huuu

1. Ni kitu unapenda kutoka moyoni,
2. Unapoishi hakuna mgahawa karibu
3

Najua ni maisha yako, Sijakupangia namna ya kusihi, ni mtazamo tuu.
Kitakachonifanye nipike ni kumsaidia mpishi tu ila sio kujipikia. Biashara za kutumia nusu saa kupika chakula cha kukila ndani ya dk 5 sijawahi fagilia kabisa.
 
Nikijipikia mboga itabaki nitaila wakati Mwingine.

Nikijipikia nitakula kile kitu roho inapenda.

Nikijipikia Nina uhakika na chakula ninachokula

Nikijipikia napunguza gharama za matumizi
Matumizi sio kweli.
 
  • Thanks
Reactions: _ID
Kupika kwangu mimi kupika nakula more health kuliko kununua..afya yako ni bora zaidi .hoteli nyingi za bei nafuu chakula unakula chakula kichafu, Hakina ubora ( upikaji wa bora liende) etc.
Honest kupika nakula more health kwanza spices zote kwa afya ya kula nazo ( tangawizi,karafuu, etc)

Pia natengeneza mboga za majani na vyakula vyote napika kwa kiwango nachohitaji ziwe.
Na upikaji wa upande wa mwanaume ni few minutes kitu kipo mezani...

Nyumbani kwako kama una Friji , microwave, jiko la gesi na blender. Basi unakuwa ktk nafasi nzuri ya kula utakavyo..vyakula vingi unapika na kuweka kwenye Friji kama (nyama, maharage etc ) ndio nchi zilizoendelea utaratibu wao huo...

Vijana endeleeni kula chips na vyakula vya take away tatizo la nguvu za kiume halitawaacha..
 
uko sahihi, kujipikia bachela ni bajeti kubwa na uharibifu wa chakula maana kikibaki utalazimika kukitupa kwa kuwa kitakuwa kimechacha. Mgahawani unapewa madikodiko mengi kwa gharama ndogo na huokoa muda wa kupika upate muda wa kupumzika unaporudi nyumbani baada ya kazi
 
Kuna vitu unafanya halafu siku ukakaa ukatafakari utaona ulichagua njia isiyo sahihi kabisa....

Unapokua unaishi mwenyewe, ukaamua kujipikia basi labda iwe kwa mtazamo huuu

1. Ni kitu unapenda kutoka moyoni,
2. Unapoishi hakuna mgahawa karibu
3. Uchafu wa migahawa inayokuzunguka
4. Huwezi kutunza pesa hivyo bora ununue chakula hata ukiishiwa unachakua n.k lakini sio sababu ya Saving.

Lakini kinyume na hapo kama unaamini una save chochote basi unajidanganya,

1. Kupoteza mda, hiki ndio kipengele kikubwa, kuanzia manunuzi/maandalizi, kupika kwenyewe, kuosha vyombo, kusafisha jikoni, kupanga na shughuli nyingne zote zinazofanyika jikoni...

2. Kero za takataka, hasa ndugu zangu wa mjini, umepika ushamaliza mambo yako tumbo limejaa, kipengele ukiangalia makololo ya mabaki ya vyakula, hapo ndio unafikiria pakuyapeleka, Nyumba nyingne hazina Waste disposal nzuri, ni timing ifike usiku ukatupe barabarani.

3. Kero ya kucheza na bajeti, mda wote wewe kuwaza, unga nusu shilling kadhaa,mafuta nusu bei ile, Sukari kilo sijui sh ngapi, kesho ukienda bei imebadirika unakua mkali..

4. Gharama, kujipikia ni gharama, usijidanganye kabisa eti kuna kitu una save, Leo hii unaweza ukaenda mgahawani ukala chakula cha Buku, niambie ni katika mazingira gani utajipikia chakula baadae ukijumlisha mboga, chakula, gas, viungo, Chumvi n.k utakua umetumia chini ya buku? Nipe hio bajeti hapa na kweli iwe applicable.

5. Hasara, katika upikaji sio mda wote unachopika unakila chote, kuna kubakia, kuharibika, kuharibu, kuunguza n.k zote hizo ni lost ambazo ukiziweka kwenye mahesabu unazidi kuongeza budget..

6. Ratiba, upo sehemu unafanya hili na lile, kichwani unawaza kwenda kugombana na masufuriaa, unalazimika kufunga hata ofisi sababu umekua mfungwa wa kujipikia

Faida za kula mgahawani..

1. Unaokoa mda, hili ndio kubwa, utatumia huu mda kufanya mambo mengine ya msingi
2. Unaokoa pesa
3. Unakua flexible na nini ule, Nyumbani mda mwingine unalazimika kula kitu ambacho kuhutaka sababu tuu ndio kimebaki hutaki kukiharibu au
4. Unakua huru na ratiba zako mda ukifika unaenda kula unaendelea na ratiba.
5. Usafi, mda mwingi ndani panakua pasafi, unapofanya usafi ni wakawaida, Kinyume na hapo unatembea njiani vidole vinanuka vitunguu..
6. Unaepuka kero za takataka na maji taka.

Katika hayo yote simaanishi ndio usijue kupika, simaanishi usiwe na chombo hata kimoja,

Jifunze kupika, mana hujui na mazingira gani utalazimima kupika..

Nunua vyombo vyote, siku kwa kujiachia ukaona leo na mimi nijipikie, hio pia iko poa

ILA SIO KUA MTUMWA WA MAPISHI..
Pia kwa kiasi kikubwa hapa nazungumzia wale tuliopanga,

Kwa watu wenye Familia au zaidi ya mmoja Hilo la kupika yaweza kua options nzuri, Pia katika hili Sijalenga wanawake.

Niko tayari kukosolewa na kurekebishwa kwa hoja itapendeza.

Najua ni maisha yako, Sijakupangia namna ya kusihi, ni mtazamo tuu.
Oa kijana hata kwa mkopo.
 
Hii kitu yaupishi inaanzia mbali sn. .utotoni,km home ulifunfishwa kupika ukienda migahawani kuna test/ladha ya chakula unaikosa migahawani ndio chanzo cha wengi kupika...sio kuahawana hela no...kingine wamama wengi wanachemsha nakujaza mafuta instead ya kuunga mchuzi vzr I hate that
 
Kupika kwangu mimi kupika nakula more health kuliko kununua..afya yako ni bora zaidi .hoteli nyingi za bei nafuu chakula unakula chakula kichafu, Hakina ubora ( upikaji wa bora liende) etc.
Honest kupika nakula more health kwanza spices zote kwa afya ya kula nazo ( tangawizi,karafuu, etc)

Pia natengeneza mboga za majani na vyakula vyote napika kwa kiwango nachohitaji ziwe.
Na upikaji wa upande wa mwanaume ni few minutes kitu kipo mezani...

Nyumbani kwako kama una Friji , microwave, jiko la gesi na blender. Basi unakuwa ktk nafasi nzuri ya kula utakavyo..vyakula vingi unapika na kuweka kwenye Friji kama (nyama, maharage etc ) ndio nchi zilizoendelea utaratibu wao huo...

Vijana endeleeni kula chips na vyakula vya take away tatizo la nguvu za kiume halitawaacha..
Hili umeliongea vyema kabisa mfano huku mikoani migahawa mingi vyakula hawaungi na nazi hii ndio sababu ya kuamua tu kupika mwenyewe pale unapopata nafasi mimi huwa napenda jioni nipate wali na samaki nazi iliyokolea
 
Nikijipikia mboga itabaki nitaila wakati Mwingine.

Nikijipikia nitakula kile kitu roho inapenda.

Nikijipikia Nina uhakika na chakula ninachokula

Nikijipikia napunguza gharama za matumizi
Huyu atakuwa anasumbuliwa na uvivu!
 
Back
Top Bottom