Kuongeza kodi sawa, lakini haya yazingatiwe

johnmashilatu

JF-Expert Member
Sep 16, 2010
729
713
wiki hii Rais Samia Suluhu Hassan amezindua kiwanda cha kuunganisha malori kilichopo kigamboni, Dar es salaam ambapo serikali inaonekana kuunga mkono hoja ya wawekezaji kutaka kuongeza kodi kwa malori yanayoingizwa kutoka nje ya nchi.

Kimsingi sina pingamizi na kuongezwa kwa kodi hiyo lakini ningependa mambo kadhaa yazingatiwe kabla ya kufikia uamuzi huo.

Kwanza kinachofanyika kwa sasa ni sawa na wanaoagiza hayo magari nje ya nchi, kwani idadi kubwa kama sio zote za vjfaa 2400 vinavyotumika kuunga lori moja bila shaka ni kutoka nje ya nchi. Huyu anaingiza Lori na mwingine anaingiza vipande na kuja kuviunga ili kupata Lori.

Hoja hapa ni serikali kuwezesha watanzania kuanzisha viwanda vya matairi, nk na viwanda hivi vya kuunga magari vilazimishwe kununua malighafi zinazozalishwa ndani ya nchi.

Isije kutokea ya kwenye sukari ambapo wenye viwanda wanatumia mwanya huo na kusababisha upungufu wa kutengenezà ili sukari ikose na wao wapate vibali vya kuuza nje na kujinufaisha maradufu.

kabla kufikia uamuzi huo ambao pia umelenga wawekezaji wengine hasa wa glass, tuangalie SAAB SCANIA pale kibaha iliendeshwaje?
 
Hivi huu Uzi wako upo?
IMG_20240511_123025.jpg
 
Back
Top Bottom