Kuondoa machinga halafu kuruhusu ujenzi holela wa vibanda vya biashara sio sawa

mahindi hayaoti mjini

JF-Expert Member
Nov 29, 2022
1,221
1,267
Ni kweli Kariakoo ni sehemu ya biashara hilo halina ubishi, lakini ukweli mwingine pia ni makazi na matumizi ya wengi wapitao njia.

Embu pita tu pale Kariakoo uone jinsi nyumba zinavyobadilishwa, vichochoro vyote sasa ni viduka, gorofa zinabadilishwa kutoka makazi kuwa maduka kimya kimya, ujenzi unafanyika nyakati za usiku tu, wasimamizi wa sheria hawapo au wamebariki?

Haiwezekani twende tu kama wanyama, matokeo yake si mazuri. Hapakuwa na haja ya kuondoa machinga kisha kuruhusu hizo sehemu za wamachinga kujengwa ngazi za kupandia juu au kujenga vibanda vya mabati na kugusanisha na ukuta wa nyumba halafu mseme ni halali?

Huu ni uozo unaosubiri kunuka wakati wowote. Kuta za magorofa zimegusana kiasi hata paka hawezi kupita, ujenzi huu unapatikana Dar es Salaam peke yake.

Ni hatari wakati wa dharura, msije sema sikuwaambia.
 
Macho yako yanakudanganya ila maisha tunayoyapitia tunajua wenyewe. .
 
Dar ni jiji holela, "big village 'muda si mrefu halitafaa kuishi binadamu
 
Back
Top Bottom