Kuona wachawi kuna maana gani?

Kuona wachawi kuna maana gani?

Mbona mmeuwenga sana
Mtoto anaona sababu bado anakuwa hana dhambi.

Ukikua mwili unakuwa najisi kwa uzinzi na mengine mengi haswa kula nyama
Mbona mmeuwenga sana uzinzi?
 
Nakumbuka nikiwa mdogo, angalau miaka 6-7, katika kijiji kimoja ndani ndani huko Tanzania, niliwahi kushuhudia wachawi wakiingia ndani ya chumba nilicholala nyakati za usiku mzito.

Niliweza kuwaona wachawi kila mara walipoingia ndani ya chumba kwa siku tofauti tofauti.

Walikuwa wanawake angalau watatu au wanne waliokuwa uchi na walijifunga vitu kiunoni mfano wa kamba. Niliwatizama katika mwanga hafifu wa giza lakini niliwaona na kuwashuhudia kwa macho yangu.

Ni kumbukumbu halisi ambazo hazikuwahi kufutika mpaka nimekuwa mtu mzima.

Sifahamu kama mtu wa kawaida anapoweza kuwaona wachawi ni jambo linalokubalika katika ulimwengu usiionekana?

Ama huenda katika umri ule, nilikuwa nina uwezo wa kutizama wachawi katika ulimwengu usioonekana?

Baada ya kuanza kukua, sikuweza kuwaona tena.

Niliwashuhudia wakitembea na kuwanga ndani ya chumba. Kila nilipojaribu kupiga kelele, mama yangu alikuja mbio na kisha wachawi walikimbia na nilivisikia vishindo vyao vizito kama vya tembo.

Je, hili linaweza kumaanisha lolote?
tuendelee kujifukiza
 
Kuna miaka na mm nilikua kama wewe...Dk akamwambia mama huyu mwanao ana malaria kali...nikatibiwa since there sikuwah kuona ndo zile homa zinapanda kichwani hiyo ya kupiga piga kelele usk kwa watoto sio nzuri wanasema...
Kwaiyo unataka kusemaje[emoji23]
 
Ndio ila ukila kitimoto hata wachawi hawaji kabisa nyama nyekundu sio nzuri sana ..

Huku kwetu tunawaona wanga wamenasa kwenye mabati deile
Ivi wachawi na mapepo ni tofauti eeeh maana nakumbuka kwenye bibilia yule jamaa mwenye mapepo alipokutana na Yesu mapepo yakamwambia Yesu turuhusu tuwaingie wale nguruwe
 
Aisee hizo ngoma mimi hua nazisikia lakini huwa nazipuuza najua labda uko kuna vigodoro vya uswahilini vinaendelea tena mi nazisikia mida yaa saa tisa kwenda saa kumi....duu aisee uku Mtwara kiboko[emoji119]

ila ni kheri tu uzipuuze maana kama kitu hakikuathiri sioni haja kubwa ya kuimiza kichwa nacho
 
ilikua ni ndoto tu baada ya kula kiporo Cha wali
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom