Kuona wachawi kuna maana gani?

Kuona wachawi kuna maana gani?

GODZILLA

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2014
Posts
5,909
Reaction score
10,567
Nakumbuka nikiwa mdogo, angalau miaka 6-7, katika kijiji kimoja ndani ndani huko Tanzania, niliwahi kushuhudia wachawi wakiingia ndani ya chumba nilicholala nyakati za usiku mzito.

Niliweza kuwaona wachawi kila mara walipoingia ndani ya chumba kwa siku tofauti tofauti.

Walikuwa wanawake angalau watatu au wanne waliokuwa uchi na walijifunga vitu kiunoni mfano wa kamba. Niliwatizama katika mwanga hafifu wa giza lakini niliwaona na kuwashuhudia kwa macho yangu.

Ni kumbukumbu halisi ambazo hazikuwahi kufutika mpaka nimekuwa mtu mzima.

Sifahamu kama mtu wa kawaida anapoweza kuwaona wachawi ni jambo linalokubalika katika ulimwengu usiionekana?

Ama huenda katika umri ule, nilikuwa nina uwezo wa kutizama wachawi katika ulimwengu usioonekana?

Baada ya kuanza kukua, sikuweza kuwaona tena.

Niliwashuhudia wakitembea na kuwanga ndani ya chumba. Kila nilipojaribu kupiga kelele, mama yangu alikuja mbio na kisha wachawi walikimbia na nilivisikia vishindo vyao vizito kama vya tembo.

Je, hili linaweza kumaanisha lolote?
 
Ni kweli Mkuu hata nimewahi kuona nikiwa na umri 7 na nikaona kwa mara ya pili nikiwa na umri wa miaka 15 na hua nashangaa watu wanaoamini uchawi hamna
 
Kuna miaka na mm nilikua kama wewe...Dk akamwambia mama huyu mwanao ana malaria kali...nikatibiwa since there sikuwah kuona ndo zile homa zinapanda kichwani hiyo ya kupiga piga kelele usk kwa watoto sio nzuri wanasema...
 
Kuna miaka na mm nilikua kama wewe...Dk akamwambia mama huyu mwanao ana malaria kali...nikatibiwa since there sikuwah kuona ndo zile homa zinapanda kichwani hiyo ya kupiga piga kelele usk kwa watoto sio nzuri wanasema...
Popcorn plz Niko hapa kusubiri jibu
 
Wajuvi wa haya mambo watuambie. Hata mimi inanitokea hii kitu tangu mwaka 2012
 
Sikuona sura zao. Walikuwa wanatembea ndani ya chumba kama vivuli.

Lakini niliona maumbo yao ni ya wanawake.
Bibi Yangu Alikuwa miongoni mwao..aliwahi nishirikisha hiyo habari...tulikuwa majirani kabisa ....
 
Navyojua uchawi upo,lakini pia ukiwa una wasiwasi au unaogopa kitu usiku ata nguo iliotundikwa wewe unaweza ukaona kama mtu,au mkanda ukaona nyoka au mti barabarani ukaona jini ..wanaita illusion
 
Navyojua uchawi upo,lakini pia ukiwa una wasiwasi au unaogopa kitu usiku ata nguo iliotundikwa wewe unaweza ukaona kama mtu,au mkanda ukaona nyoka au mti barabarani ukaona jini ..wanaita illusion

Hiyo kweli, kuna sehemu nilipata kuishi yaani ilikuwa ikifika muda kati ya saa 7 hadi 9 usiku, nasikia kelele za ngoma za kiasili plus mayowe na vigelegele kama kuna sherehe zile za vijijini flani. Sikuwahi hata kuzijali ila siku moja nikamuuliza mtu na akanambia hizo ni ngoma za wachawi na inavyosemekana kuna eneo tunalopakana nalo ndio huwa makutano yao

hii ilinipa hofu sana yaani ikifika usiku hata nikisikia watu wanaongea au kutembea nje bhasi mapigo ya moyo yanaenda kasi na kutetemeka. Nikisikia kishindo chochote najua tayari washafika ila baada ya muda flani nilikaa sawa baada ya kuona mara nyingi najichezea akili mwenyewe
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom