Nakumbuka nikiwa mdogo, angalau miaka 6-7, katika kijiji kimoja ndani ndani huko Tanzania, niliwahi kushuhudia wachawi wakiingia ndani ya chumba nilicholala nyakati za usiku mzito.
Niliweza kuwaona wachawi kila mara walipoingia ndani ya chumba kwa siku tofauti tofauti.
Walikuwa wanawake angalau watatu au wanne waliokuwa uchi na walijifunga vitu kiunoni mfano wa kamba. Niliwatizama katika mwanga hafifu wa giza lakini niliwaona na kuwashuhudia kwa macho yangu.
Ni kumbukumbu halisi ambazo hazikuwahi kufutika mpaka nimekuwa mtu mzima.
Sifahamu kama mtu wa kawaida anapoweza kuwaona wachawi ni jambo linalokubalika katika ulimwengu usiionekana?
Ama huenda katika umri ule, nilikuwa nina uwezo wa kutizama wachawi katika ulimwengu usioonekana?
Baada ya kuanza kukua, sikuweza kuwaona tena.
Niliwashuhudia wakitembea na kuwanga ndani ya chumba. Kila nilipojaribu kupiga kelele, mama yangu alikuja mbio na kisha wachawi walikimbia na nilivisikia vishindo vyao vizito kama vya tembo.
Je, hili linaweza kumaanisha lolote?