Kuolea nyumbani kunadumisha ndoa

Kuolea nyumbani kunadumisha ndoa

Nakubaliana na wewe, japo sio kuhusu lugha. Manake kuna wasiojua mother tongue zao kwa kukulia mjini. Kwenye ndoa, tamaduni ni chanzo kikubwa cha migogoro. Kama walau mnaamini kwenye same stuff (najipatia picha nnavyochukia matambiko na babangu Mtambuzi anavyoyafyagilia)

Ila inapendeza sana kama wote mnaelewana kuhusu tamaduni, lugha nk.
 
Ndugu wana JF,

Asalaam aleikum. Mmezoea kuniita mwenye matatizo lakini leo nimekuja na wazo hapa. Mi naona ndoa za wale ambao waliolea kwao au mke na mme wanatoka Mkoa mmoja naona wana raha zaidi kuliko sisi tuliooa makabila mengine haya. Kuna wakati ambapo ungapenda kuongea kilugha, lakini unashindwa. Mfano, mimi akija mdogo wangu nikiongea nae kilugha naona mke anakuja juu nakusema tuongee kiswahili. Utamu wa hadithi ni lugha, na lugha yenyewe ni ile ya mama na sio ya mke. Hili halihusiani na ukabila lahasha kwa maana upendo hauna ukabila wala dini. Lakini nahisi wenzetu wanaoongea lugha moja ndoa zao zinadumu zaidi na upendo unakuwa bomba kila wakati. Wewe unaonaje na mme wako au mke?

kama ingekuwa ni kweli basi kenya kungekuwa hakuna divorce! maana wao kwa ukabila wanapenda oana wao kwa wao lakini kila siku kesi na mauaji ya kutisha! cha muhimu ni upendo! wazazi wangu ni makabila tofauti na mpk leo wanapendana mpk tunawadmire!
 
Ngoja nikwambie Wiliyeye, wewe kuanzia leo hii ukirudi home kama unachuki na mkeo ziondoe , na pia mkiss mkeo kama mwanzo mlipokutana.
Pili penda kucheza na kuongea na wanao , wasaidie Homework zao, yaani wewe kuwa busy na watoto wako utaona na yeye anakuja na mtaongea vizuri bila kutegemea.

Sisi wamama tukiona mwanamme anapenda sana watoto tunafarijika , Automatically tunawapenda waume zetu.
lile penzi ulilokuwa hulipati, kwa muda utaanza kulipata, kama alikuwa hakushirikishi kwenye mambo yake ataanza kukushirikisha na NDOA yako itachipua upya kama mwanzo.

Fanya hayo, Ukiwa Juu na Mkeo Yuko Juu hakutakuwa na suluhu mmoja lazima ashuke ndipo mtaelewana.

Wapo wanawake ambao wakiona hilo watabadilika na kuwa wema. Think about this; una mke, unaongea kilugha na ndugu yeye anakuja juu! Ananuna mbele ya wageni, na kutamka kwamba hataki vilugha. Hafui nguo, hatandiki kitandani, haonji chakula cha mmewe kikipikwa na HG, Wala hakagui nguo za mmewe kama zimechanika au kama buttons zimekatika!

Mtu umejaribu kumwelewesha lakini imeshindikana, hata wazazi wake pia wanaona mtoto wao ni mvivu! Ndo maana nasema pengine wanaume wanakurupuka sana hapa. Ni bora uoe kabila lako kwa maana unalielewa sana.
 
Ni sawa kabisa! Hata watoto kuwafundisha lugha mbili (ya mama na ya baba) ni shughuli; lakini kama lugha ni moja tu watoto wana-enjoy! (Ndi wa Mureba nshamba na mukazi wange wa Mureba nshamba)

Shumaramu Waitu...!
 
Inategemea unaishi wapi..........ukiowa mtu wa kwenu mkae huko kwenu mkiwa huku mujini wala hakuna maana sana zaidi ya kuendekeza ukabila tu.....hicho kilugha chenu mtaishia kuongelea chumbani
 
Ndiyo maana mimi sijaolewa nategeshea wa.kwere wenzangu waje waniopoe lakini nao hawaji! Nikichoka kusubiri, itabidi niende kujisalimisha kwa m.kwere mwenzangu wa magogoni huenda akanisaidia.
 
Ndugu wana JF,

Asalaam aleikum. Mmezoea kuniita mwenye matatizo lakini leo nimekuja na wazo hapa. Mi naona ndoa za wale ambao waliolea kwao au mke na mme wanatoka Mkoa mmoja naona wana raha zaidi kuliko sisi tuliooa makabila mengine haya. Kuna wakati ambapo ungapenda kuongea kilugha, lakini unashindwa. Mfano, mimi akija mdogo wangu nikiongea nae kilugha naona mke anakuja juu nakusema tuongee kiswahili. Utamu wa hadithi ni lugha, na lugha yenyewe ni ile ya mama na sio ya mke. Hili halihusiani na ukabila lahasha kwa maana upendo hauna ukabila wala dini. Lakini nahisi wenzetu wanaoongea lugha moja ndoa zao zinadumu zaidi na upendo unakuwa bomba kila wakati. Wewe unaonaje na mme wako au mke?
hakika huu ni ukweli unaoumiza japo wengui waweza kuja na hoja za 'uongo unaoponya'
 
Inategemea unaishi wapi..........ukiowa mtu wa kwenu mkae huko kwenu mkiwa huku mujini wala hakuna maana sana zaidi ya kuendekeza ukabila tu.....hicho kilugha chenu mtaishia kuongelea chumbani
ukiwa bara lingine, mtu wa bara lako ni wazo zuri, ukiwa nchi nyingine mtu wa nchi yako aweza kuwa wazo sahihi, ukiwa mkoa mwingine mtu wa mkoa/kanda yako ni chaguo, wilaya nk.
Kiujumla inategemea how big is the box you are in na kiwango cha uelewa na uchumi mliomo. Kazi wala sio utani!

Wapo wanawake ambao wakiona hilo watabadilika na kuwa wema. Think about this; una mke, unaongea kilugha na ndugu yeye anakuja juu! Ananuna mbele ya wageni, na kutamka kwamba hataki vilugha. Hafui nguo, hatandiki kitandani, haonji chakula cha mmewe kikipikwa na HG, Wala hakagui nguo za mmewe kama zimechanika au kama buttons zimekatika!

Mtu umejaribu kumwelewesha lakini imeshindikana, hata wazazi wake pia wanaona mtoto wao ni mvivu! Ndo maana nasema pengine wanaume wanakurupuka sana hapa. Ni bora uoe kabila lako kwa maana unalielewa sana.

Hapana Wiliyeye si kweli kwamba ukioa home ndiyo suluhisho la matatizo, la hasha wewe mueleze kuwa pindi nduguzo wakiwepo unapenda kuongea nao kiligha na si kwamba mnamsema yeye, Pia usikubali kula chakula alichopika HG, tatu kama hatandiki kitanda wewe tandika, ukiona mashuka machafu toa tandika mengine, penda kufua nguo zako, angalia mwenyewe shati zako, usimuulize kitu wala usimkasirikie, Pia penda kuchukua muda wako mwingi kucheza na wanao, kuwasaidia Home work.
Ukiona hapo home panakubore Chukua wanao nenda nao katembee urudi home late, watoto wameshakula pamoja na wewe mfikie kulala.
Nakwambia ataumia sana na atataka kuongea nawe, sasa hapo ndipo pakumwambia duku duku lako lote, kuwa hupendi nn.
 
sa mie niiliyehama nchi kabisa si ndio nna hasara sana, lolest!"

Hahahah.. u r not alone!!!

Alafu da cacico, yule ndo mista!??
Na lile ndo pozi gani sasa...kha, au mlimalizia morning glory kwenye foleni!??
 
Last edited by a moderator:
ukiwa bara lingine, mtu wa bara lako ni wazo zuri, ukiwa nchi nyingine mtu wa nchi yako aweza kuwa wazo sahihi, ukiwa mkoa mwingine mtu wa mkoa/kanda yako ni chaguo, wilaya nk.
Kiujumla inategemea how big is the box you are in na kiwango cha uelewa na uchumi mliomo. Kazi wala sio utani!

Kwa akina omujubi kwa kweli ni vigumu kutoowa "nyumbani" for the obvious reason.........you are spared

ukiwa bara lingine, mtu wa bara lako ni wazo zuri, ukiwa nchi nyingine mtu wa nchi yako aweza kuwa wazo sahihi, ukiwa mkoa mwingine mtu wa mkoa/kanda yako ni chaguo, wilaya nk.
Kiujumla inategemea how big is the box you are in na kiwango cha uelewa na uchumi mliomo. Kazi wala sio utani!

Kaka, you have a huge world view! Big up
 
Wapo wanawake ambao wakiona hilo watabadilika na kuwa wema. Think about this; una mke, unaongea kilugha na ndugu yeye anakuja juu! Ananuna mbele ya wageni, na kutamka kwamba hataki vilugha. Hafui nguo, hatandiki kitandani, haonji chakula cha mmewe kikipikwa na HG, Wala hakagui nguo za mmewe kama zimechanika au kama buttons zimekatika!

Mtu umejaribu kumwelewesha lakini imeshindikana, hata wazazi wake pia wanaona mtoto wao ni mvivu! Ndo maana nasema pengine wanaume wanakurupuka sana hapa. Ni bora uoe kabila lako kwa maana unalielewa sana.

inadepend what I get back from doing all that,Kama hunifurahishi don't expect anything of that kind from me,wanaume wengi wanapenda kufanyiwa wakati wao hata majukumu yao hawayatimizi,
 
Unaona sasa? Kwa hiyo unatangaza kushindana na mwanaume?
 
Ngoja nikwambie Wiliyeye, wewe kuanzia leo hii ukirudi home kama unachuki na mkeo ziondoe , na pia mkiss mkeo kama mwanzo mlipokutana.
Pili penda kucheza na kuongea na wanao , wasaidie Homework zao, yaani wewe kuwa busy na watoto wako utaona na yeye anakuja na mtaongea vizuri bila kutegemea.

Sisi wamama tukiona mwanamme anapenda sana watoto tunafarijika , Automatically tunawapenda waume zetu.
lile penzi ulilokuwa hulipati, kwa muda utaanza kulipata, kama alikuwa hakushirikishi kwenye mambo yake ataanza kukushirikisha na NDOA yako itachipua upya kama mwanzo.

Fanya hayo, Ukiwa Juu na Mkeo Yuko Juu hakutakuwa na suluhu mmoja lazima ashuke ndipo mtaelewana.

Change needs that the mind should be emptied before one could accommodate any new idea.
 
Kutokana na uzoefu wangu, na jinsi nilivyoitathimini ndoa yangu kama mfano, huenda ningakamata mke wa home ningekuwa na wakati mzuri sana kuliko sasa. Nadhani kilichobaki ni kutoa ushauri kwa wale ambao hawajaoa au kuolewa.
 
Ahsante kwa kutukumbusha kaka sisi ambao bado hatujaingia huko
 
Back
Top Bottom