Kuolea nyumbani kunadumisha ndoa

Unaona sasa? Kwa hiyo unatangaza kushindana na mwanaume?

Sio mashindano ni kila mtu kutimiza wajibu wake not becoz I'm a woman ndo basi nakufanyia tuu,Kama ni kazini nami naenda nami nachoka Kama wewe,so we either help each other or housegirl atusaidie,
 
Tupate uzoefu wa walioolewa nchi za magharibi.
Natalia, Muke Ya Muzungu, Kongosho na snowhite (yule bf wako wa praimare muhindi)
hebu tupeni uzoefu wenu?
ahahhhahahhaah mi kweli bana nimeolewa nchi za kaskazini lakini failure yoyote niliyopata kwenye ndoa yangu sijwahai kuona connection na makabila yetu!
kimsingi mi ni wale watu walio mchanganyiko kwisha kazi!
mimi mama yangu mnyaki,baba yangu mngoni,mume wangu baba yake mchaga mama yake mhaya!sasa hapo kuna kama makabila tofauti ndo ingekuwa source ya matatizo mi si ningekuwa niko chuo cha sita saa hizi?
NDOA NA MAFANIKIO YAKE NI MTU BINAFSI wajameni!
 
Mada hii ina ukweli ndani yake.

Ndugu yangu mmoja kaolewa na kabila tofauti, siku wakikwaruzana shemeji anamwambia kuwa kwetu mwanamke hawezi kukujibu au kufanya hivi kwa mmewe.

Wangekuwa wote kabila moja hoja hiyo isingekuwepo zaidi ya kutafuta suluhisho katika ugomvi wao.
 
Wiyelele, mi nakubaliana na wewe kabisa. Kuna mambo mengi ambayo yanatofautiana iwapo mtu umechanganya haya mambo!

hata mie naunga mkono yako mengi na walio katika hali hii watakuwa mashahidi. sio lugha tu, hata shughuli nyinginezo katika maisha ya kawaida sana. tuwashauri vijana waoe nyumbani. wachagga wanasema" usioe chasaka"yaani mtu/mwanamke asie wa nyumbani kwake, nadhani waliliona hilo mapema,
 
hata mie naunga mkono yako mengi na walio katika hali hii watakuwa mashahidi. sio lugha tu, hata shughuli nyinginezo katika maisha ya kawaida sana. tuwashauri vijana waoe nyumbani. wachagga wanasema" usioe chasaka"yaani mtu/mwanamke asie wa nyumbani kwake, nadhani waliliona hilo mapema,

japo hatuna uweze wa kibinadamu wa kutazama ndani ya mioyo ya wazazi wetu pindi tunapooa makabila mengine, wazazi huwa wanaumia sana. Maumivu yao yanatokana na sisi kukaidi ushauri wao. Mfano, baba yangu alinikataza sana kuoa mke wangu. sasa nateseka nae vibaya sana! Akirudi home kwa vile amekulia uchochoroni Dar, ndo taraabu kila siku hadi unashindwa kusoma na kulala vizuri. Angekuwa mke wanyumbani, mbona ningefaidi sana jamani?
 
Ndugu wana JF,

Asalaam aleikum. Mmezoea kuniita mwenye matatizo lakini leo nimekuja na wazo hapa. Mi naona ndoa za wale ambao waliolea kwao au mke na mme wanatoka Mkoa mmoja naona wana raha zaidi kuliko sisi tuliooa makabila mengine haya. Kuna wakati ambapo ungapenda kuongea kilugha, lakini unashindwa. Mfano, mimi akija mdogo wangu nikiongea nae kilugha naona mke anakuja juu nakusema tuongee kiswahili. Utamu wa hadithi ni lugha, na lugha yenyewe ni ile ya mama na sio ya mke. Hili halihusiani na ukabila lahasha kwa maana upendo hauna ukabila wala dini. Lakini nahisi wenzetu wanaoongea lugha moja ndoa zao zinadumu zaidi na upendo unakuwa bomba kila wakati. Wewe unaonaje na mme wako au mke?
Love has no boundaries!
 
Of course, you will not know the boundaries if u have not experienced any problem.

Again, love has no boundaries. That's why even the queen of Sheba fell in love with king Solomon of Israel. That's why Ben Mkapa (chinga) married Anna Mkapa (chaga), Scott Pippen, Joseph Warioba, Nelson Mandela, Olusegum Obasanjo,........and the list goes on. Mapenzi ni maelewano na sio eti kwa kuwa mnatoka sehemu moja ama kabila moja ama dini or race. Moyo wako na wake ikigongana na kupendana basi toshaaaa
 
Sio kwamba ukioa/olewa wa kabila lako unakuwa na furaha zaidi ila ni kwamba adjustment especially during the first years of marriage inakuwaga rahisi kuliko yule alieoa/olewa na mtu kutoka kabila tofauti. Kama wewe ni mtu unamind sana tamaduni za kabila lako na ungependa kudumisha ningekushauri uoe/uolewe na mtu wa kabila lako. Kama wewe umezaliwa humuhumu mjini wala it doesn' matter sana kama unaoa/olewana mtu wa kabila lenu au la!! Mlughalugha aoe/olewe na mlughalugha mwenzake!!Born town aoe/olewe na born town mwenzake!!
 
Sio kwamba natapatapa, ila naona wenzangu wana furaha sana na ndoa zao. Nilipochunguza nikaona wengi wameoa kwao au mikoa ya jirani ambayo wanaelewana lugha.

hahahahahahaaa!uwiiii!mmenivunja mbavu sana kwa thread hizi wiyelele!Namkumbuka mwinyi mpeku wa sani ana vimisemo vyake na hapa nanukuu "Mboga usiyoila huijui chumvi yake"Asanteni hahahahahahaaa
 
kuna raha yake lakini kazi ipo kwetu sisi ambao baba mkinga na mama msambaa.sasa hapo hata ukioa mkinga au msamba bado haina maana ya kabila moja.labda utafute mchanganyiko kama wako.
 
kuna raha yake lakini kazi ipo kwetu sisi ambao baba mkinga na mama msambaa.sasa hapo hata ukioa mkinga au msamba bado haina maana ya kabila moja.labda utafute mchanganyiko kama wako.

Kwani baba akiwa Mkinga na mama msambaa, ukiulizwa kenu wapi unajibuje?
 
Back
Top Bottom