Kuoana bila kutaka watoto - yawezekana? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuoana bila kutaka watoto - yawezekana?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mzee Mwanakijiji, Jan 27, 2011.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Jan 27, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Kwamba watu wawili mnaopendana mnaamua kuoana na kuishi maisha ya pamoja bila kutaka kuwa na watoto au kupanga kuwa na watoto. Je hili linawezekana katika jamii yetu au kila ndoa inapimwa kwa mafanikio ya kuwa na watoto na kwamba bila ya watoto ndoa inaonekana kama haikamiliki na hivyo mtu yuko radhi kufanya "lolote" ili awe na watoto?
   
 2. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #2
  Jan 27, 2011
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Upo huo uwezekano MMKJJ lakini kwa hali fulani tu.

  Nimeona kwa mfano mwanaume ambaye amefiwa au kuachana na mkewe akataka kuoa tena ili apate mwenza ( companion) na siyo mama wa watoto.Wapo wanawake wenye kutamani kuwa na companion kwa vile labda walishazaa na hawataki watoto tena.Mara nyingi mwanaume mwenye mwanamke kama huyo, hataacha "kutafuta mtoto kando".Kwa vijana wenye umri wa kuzaa sijui kama hili linawezekana.

  Kwa kifupi nadhani ulazima wa kuzaa uko kwa wanaume zaidi Nionavyo mimi.
   
 3. CPU

  CPU JF Gold Member

  #3
  Jan 27, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,871
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Mi nadhani kwa utamaduni wetu mwafrika mtoto/watoto ni ishara kubwa ya mafanikio ktk maisha ya ndoa, na ndoa inakamilika mkizaa watoto hata katika maandiko matakatifu wanasisitiza umuhimu wa kuwa na watoto. Maisha bila mtoto ni kama mlioana kuridhishana kimwili tu, kitu ambacho mnaweza kufanya bila hata kufunga ndoa
   
 4. CPU

  CPU JF Gold Member

  #4
  Jan 27, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,871
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Kama mwanamke alishazaa kabla ya kukutana na mwanaume ambaye hajazaa, hapo ulazima unakuwa kwa mwanaume kweli lakin pia kama mwanaume alishazaa kabla hajakutana na mwanamke ambaye hajazaa basi ulazima utakuwa kwa mwanamke

  Nje na maelezo hayo, umuhimu wa kuzaa upo kwa pande zote mbili, mwanamke na mwanaume
   
 5. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #5
  Jan 27, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Uwezekano upo...tatizo ni watu wa nje watachukuliaje uamuzi huo!
   
 6. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #6
  Jan 27, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  CPU.. sasa kama mmoja wao baada ya ndoa ikagundulika au ikatokea sababu ya kutokuweza kuzaa ina maana yule mwingine ana haki ya kuzaa nje ya ndoa au ndoa ivunjike hata kama bado wanapendana?
   
 7. Pearl

  Pearl JF-Expert Member

  #7
  Jan 27, 2011
  Joined: Nov 25, 2009
  Messages: 3,042
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Mimi nadhani,si kama tunapanga kutokuwa na watoto hapana ,mipango ya watoto,nyumba na vitu vingine wengi walio kwenye ndoa hata wasio kwenye ndoa,wanaongea na kupanga lkn swala linakuja je sasa tumeshindwa kufanikisha ile mipango yetu,je tutaweza kupendana kama mwanzo?tutaweza kuwa na furaha tuliyokuwa nayo?swala la watoto kama binadam tunapanga,tunaomba,tunatamani,lakini Mungu ndie atoae vyoteas u kwn failer to plan is to plan to fail.
   
 8. CPU

  CPU JF Gold Member

  #8
  Jan 27, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,871
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Mzee Mwanakijiji kwa kanuni za ndoa, wawili huapa kupendana, kuvumiliana, kuheshimiana bila kusahau kulinda ndoa yao. Hata kama mmoja wao anatatizo la uzazi wanapaswa waendelee kuishi maisha waliyoapa kuishi ktk kiapo cha ndoa (yaani ktk shida na raha).
  Lakin ndoa sio kifungo, maelewano ndio nguzo kuu ya ndoa ambayo inajengwa kwa upendo.
  Kwahivyo kama wanandoa wanahitaji mtoto, na mmoja wao (ambae ana tatizo la uzazi) ataridhia mwenzake azae mtoto na mtu mwingine ili wapate mtoto basi ni jambo jema, lakin sio kuzaa na mwingine pasipo mwenza wako wa ndoa kujua.
  Au la, basi muendelee kuishi pasipo kuwa na mtoto au ikiwezekana mnaweza ku-adopt mtoto/watoto
   
 9. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #9
  Jan 27, 2011
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Swala la kuzaa baada ya kuoana ni tarajio la kijamii kufuatana na tamaduni nyingi hasa za kiafrika na hata kiasia.
  Wengi kabla ya kuoana hawafanyi mjadala kuona kama wakishindwa kuzaa itakuwa vipi.Matokeo yake siku hizi watu wanapeana mimba kabla ya ndoa ili kuepuka lawama huko mbeleni.

  Swali la kutaka kuona kama inawezekana watu wakaoana bila kuweka matarajio ya kuzaa katika mila, desturi na tamaduni zetu, ni muhimu hasa kwa kipindi au zama hizi. Watu wanaoana kwa gharama kubwa sana, wanataka kuzaa kwa udi na uvumba lakini kibaya zaid ndoa hazidumu, watu wanaachana, watoto wanajikuta kwenye familia zilizovunjika.

  Je isingekuwa bora watu wakaangalia upya umuhimu wa kuzaa kulinganisha na ugumu wa kuvumilia machungu ya ndoa kwa ajili ya kulinda haki na maslahi ya watoto wanaowataka?
   
 10. CPU

  CPU JF Gold Member

  #10
  Jan 27, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,871
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Kuzaa na kulea ni MAJUKUMU ambayo kila binadamu aliyekamili anapaswa kuyatekeleza kwa mujibu wa maandiko. "Mungu alipowafukuza Adam na Eva kutoka kule bustani ya Aden, aliwaambia kuwa nendeni mkazaane muijaze dunia"

  Kimaisha ni suala zuri sana tena sana kupanga kutozaa kama uwezo wa kulea utakukwamisha, au hamtaweza kuvumilia machungu ya kulea watoto, lakini utajikuta unabanwa na maandiko matakatifu. Hebu imagine waliotuzaa nao wangepanga wasizae tungekuwepo hapa JF kuchangia hii mada?? Je hatuoni kama kutozaa kwa makusudi ni dhambi kwa maana ya kuzuia kusiwepo vizazi vijavyo???
  Tujadili . . . .
   
 11. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #11
  Jan 27, 2011
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 475
  Trophy Points: 180
  Kwakweli kwa jamii yetu mwaka mmoja ukikata tu wanandoa hawana watoto tayari ni presha na maneno kedekede. Inapendeza kwa wanandoa kuwa na makubaliano yao ila wasichanganyikiwe na maneno au maswali kuhusu watoto kama wameamua kuishi bila kutaka watoto.
  Binafsi kama nina uwezo wa kupata watoto sitopenda tuishi na mume wangu bila watoto. Nisipofanikiwa hamna jinsi mana watoto ni majaliwa!
   
 12. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #12
  Jan 27, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Ni kweli kabisa kwenye jamii yetu Choice ya kupata watoto sio ya wanandoa pekee...., kuna shinikizo la wazazi, ndugu mpaka marafiki..., hata kama nyie wawili mkipanga otherwise..., watu wataanza kuwasema na kuwabana kwamba labda huyu tasa, na maneno mengi.... I wish watu wangewaachia issue kama hizi wanandoa wenyewe
   
 13. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #13
  Jan 27, 2011
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Swala la dhambi au la, nitasita kulijadili kwa sababu kil aleo tunatenda dhambi mbaya zaidi ya kutotaka kuzaa. Ingekuwa watu tunaogopa dhambi hivyo mbona dunia ingekuwa paradiso? Watu wangeogopa pia kujiingiza kwenye tabia za kuleta misukosuko kwenye ndoa ambayo hupelekea watu kutengana na kuumiza watoto waliowazaa kwa "kufuata maandiko".
   
 14. Lyangalo

  Lyangalo JF-Expert Member

  #14
  Jan 27, 2011
  Joined: Sep 10, 2009
  Messages: 681
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  Ndoa ni makubaliano ya watu wawili mke na mme na watoto ni matokeo ya ndoa. Kama wamekubaliana na wanaamini walichokubaliana na wakakisimamia hakika inawezekana kabisa. Tatizo letu kubwa tunaangalia sana jamii itatusemaje au kutuonaje! Je wagumba ambao huwa wahazai huwa jamii inawaonaje? mnaweza kuwa na msimamo wenu halafu wa nje waambieni nyinyi ni wagumba. Zamani watu walikuwa wanashindana kuzaa watoto wengi. Lakini kwa sasa utasikia mtu anasema huyu mtoto mmoja anatosha ingawa atakutana na dhuruba kali toka kwa wazani ndugu na jamaa lakini akiamini hivyo inawezekana.

  kwa upande mwingine inategemea hayo mapendekezo ya kutozaa yalipotolewa je waliafikiana sawasawa? au mmoja wao alikubali tu ili wakiingia kwenye ndoa am-pressulise mwenzake kuzaa. Hapa ndo pa kutafakari!
   
 15. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #15
  Jan 27, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Kimsingi lengo la kwanza la ndoa (lazima wawe mke na mume) ni Love (upendo/ intimacy) la pili ni Unity (unitive factor) na mwisho ni Procreation (Kuzaa watoto). Tatizo la jamii zetu zimefanya tatu kuwa moja na hii ndo inayofanya hiyo statement hapo juu isikubalike kijamii but inawezekana tu. Ndo maana katika imani yangu (kidini) hakuna ndoa inayovunjwa eti kwa kuwa hawapati watoto. Ndoa ni kamili immediately baada ya consummation.
   
 16. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #16
  Jan 27, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,548
  Likes Received: 18,218
  Trophy Points: 280
  Mzee Mwanakijiji, kuoa ni wajibu ila watoto ni majaliwa.
  1. Kuna ndoa nyingi ambazo hazikujaaliwa kupata watoto na bado zinadumu daima kwa upendo wa dhati. Nyingine wame adopt watoto, na nyingine wanaishi na watoto wa ndugu zao.
  2. Kama chanzo cha ukosefu wa mtoto ni mke, ana hatari ya kunyanyasika na masimango toka mama mkwe wa mume na mawifi, hali inayopelekea waume wasio na misimamo imara, kuchepuka ili angalau asifutike kwenye uso wa dunia.
  3. Kama chanzo cha ukosefu wa mtoto ni mume, then mke lazima awe mvumilivu sana, kwanza kwa kumfichia siri mumewe, pili kwa kukubali masimango ya kunyooshewa vidole kwa vile kiafrika bado wanaamini chanzo cha ukosefu wa mtoto ni mwanamke tuu.
  4. Baadhi ya wanawake wanagundua tatizo ni mume, hushauriana na mume, wajiibe kwa siri, kutengeneza mtoto ali kumfichia siri mume. Wake hawa hujiegesha kiaina kwa target na ikitokea, huahikikisha imetokea kama one night sto, wala wewe hutaaambiwa, labda tuu mpaka watoto wanapokuwa, unaona mbona yule mtoto wao coppy right na watoto wako!.
  5. Lakini pia ziko familia hapa hapa Tanzania, hawana matatizo yoyote ya uzazi, lakini wameoana na wameamua hawataki watoto.
  6. Na kuna familia nyingine mimi nikiwa ni mmoja wao,tulipooana tulipanga tupate watoto wawili tuu, lakini sasa ninao 6!, na bado sio mwisho!.
   
 17. Nazjaz

  Nazjaz JF-Expert Member

  #17
  Jan 27, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 5,345
  Likes Received: 1,131
  Trophy Points: 280
  Ndugu zangu hawatakawia kuniwekea vikao kuwa kwanini sishiki mimba.
  Mi nataka watoto, nikitaka mwanaume wa kustarehe naye wapo wengi tu, kuanzia makuli hadi maofisa
   
 18. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #18
  Jan 27, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Hii ndio point ya Mwanakijiji kwamba iwapo mnataka watoto ni sawa..., lakini Je kama hamtaki watoto inawezekana mkaishi bila watoto..., Kutokana na jamii yetu ni vigumu sababu ya shinikizo, kutoka kwa jamii tofauti na culture nyingine huu ni uamuzi wa wanandoa wenyewe na sio mtu mwingine
   
 19. Gaga

  Gaga JF-Expert Member

  #19
  Jan 27, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,565
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Mi naona kama kuna uwezekano wa kupata watoto iwe hivyo, na kama ikitokea mmoja atakuwa hana uwezo wa kuzaa wote wawili wavumiliane tu, sababu waliapa kuvumiliana katika shida na raha wakati wanafunga pingu za maisha.
  Pili wale ambao walikuwa na uwezo wa kuzaa halafu wakapatana wasizae mi naona huu ni uselfishness tu wa watu. wenyewe wazazi wao wangeamua hivyo wangekuwepo? watto ni faraja kubwa kwenye ndoa
   
 20. L

  Leornado JF-Expert Member

  #20
  Jan 27, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,534
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Lbda uhamie ughaibuni kwa mila za kiafrica hilo swala ni gumu kama wote mnazaa.

  Kuna nchi nyingi Ulaya magharibi unakuta watu ni careeer tu hivyo hawana muda wa watoto so hawazai, lakini uzeeni wanajuta na kufa kama anonymous huku serikali ikitaifisha mali zao, ya nini yote hayo?? zaa bwana.
   
Loading...