kuoa mwanamke wa kizungu inabidi ujiandae.

Acheni ubaguzi...

Mnabagua wageni...mnabagua wakwenu...mwisho wa siku mtajikuta mmezingirwa na hao mliokua mkiwasrma vibaya tu sasa sijui mtafumba macho mpendane nao au mtabaki mkishangaa tu!!

Wazungu kama waafrika tu wapo ambao ni wanapenda kumchukulia mwanaume kama kiongozi wa familia na ambao wanapenda wao ndio wawe viongozi.Hamna kitu/tabia yoyote ambayo ni sahihi wewe kuhusisha na kundi zima la watu wa aina fulani kwasababu hata siku moja huwezi kukuta watu wa aina fulani wote wakiwa na tabia zinazofanana ziwe nzuri au mbaya!!!

Kwahiyo anaetaka kuoa mzungu akimpata ambae anaona ni size yake acha aoe.,.acha kuharibia watu wengine bahati zao!!
 
Acheni ubaguzi...

Mnabagua wageni...mnavagua wakwenu...mwisho wa siku mtajikuta mmezingirwa na hao mliokua mkiwasrma vibaya tu sasa sijui mtafumba macho mpendane nao au mtabaki mkishangaa tu!!

Wazungu kama waafrika tu wapo ambao ni wanapenda kumchukulia mwanaume kama kiongozi wa familia na ambao wanapenda wao ndio wawe viongozi.Hamna kitu/tabia yoyote ambayo ni sahihi wewe kuhusisha na kundi zima la watu wa aina fulani kwasababu hata siku moja huwezi kukuta watu wa aina fulani wote wakiwa na tabia zinazofanana ziwe nzuri au mbaya!!!

Kwahiyo anaetaka kuoa mzungu akimpata ambae anaona ni size yake acha aoe.,.acha kuhatibia watu wengine bahati zao!!

The number of ignoramuses in this forum is beyond astonishing!
 
Kijiji gani tena huko? Mie nimezaliwa Sikonge na naishi Sikonge.

Nilikuwa sifahamu kuwa nina mke mwingine. Huyu basi naona Wazazi wangu (Mungu awalaze pema, Amen) waliniozesha Mke na mie wala sikujua wakati nikiwa masomoni. Unajua matatizo ya kuondoka kwenda Form one hata hujabarehe, ndiyo unakuwa umekimbia kwenu kiaina. Unakuja kubarehe uko shuleni. Unaenda hadi JKT, baadaye Chuo kikuu na mwisho unaanza kazi. Sasa wazee wakiona kabinti fulani kanalima sana, kanatwanga sana, kanabeba kuni kibao, kanapenda watoto nk wanaona haka katamfaa Mwanetu Sikonge. Wanakuozesha wakati haupo na wewe ukifika, unakuja na mawazo mengine kabisa na mke wa hivyo anakuwa hakufai tena maana mnaongelea mawimbo tofauti na inaweza kuchukua muda sana kumpa na yeye shule. Ila kama una muda, ni SAFI SANA.

FL, nilikuwa sifahamu kuwa na wewe ni wa SIKONGE. Nashukuru kufahamu. Wavezya sana ilumbu lyane :)
Wavezya kutogwa woo!

Wapanga sikonge?
 
Hatari kubwa jirani kuna mwaume wa kizungu kaowa mwanamke wa kihaya.mwanamama analalamika bwana ni baridi sana hana joto kama wabongo.
 
Kwani wabantu kwa wabantu ndo hakuna mipango ya kando? Na wabantu wanaotoka nje ya mahusiano yao what is missing? Kwa sababu kila siku humu watu wanalia kutendwa. Au sababu za mtu aliyeoa au kuolewa na mzungu zinazomfanya acheat ni tofauti na sababu zinazomfanya mbantu aliyemuoa au kuolewa na mbantu mwenzake? Kama ndo hivyo basi mimi sikulijua hilo.

Sema mkubwa.Swala si mzungu,swala ni individual na anatabia gani na mta-make mahusiano gani.
 
Mie nilikuwa nawaona watoto wa Kizungu miaka ileee. Unakuta Binti akiwa na Mcongo basi anaondoka Kwasakwasa hadi unakaa chini.

Akiwa na Mtanzania, Mduara hadi anajua kuimba "Kachirii Kachirii, Saga."

Akiwa na West Africa, basi anaondoka Mapouka ni kasheshe. Akiwa na Mnigeria/Ghana basi Fufu ndiyo home.

Yupo mmoja kwa sasa Dar kaolewa na Mshikaji, yeye unamkuta hadi mtoto kambeba Mgongoni na khanga :)

Wanawake wote ni sawa ila UTALALA ULIPOTANDIKA. Samaki usipomkunja yungali mbichi, basi UTAKUNJWA WEWE.

La muhimu ni kufahamu wewe na yeye (muelimishe) sasa ni mwili mmoja. Haya ya kufanyiana mashindano nani anatawala ili akajisifie nje, mnarudishana sana nyuma wote. Inatakiwa msaidiane kwa kila hali ili muendeleze maisha yenu kwani mkikwama, ni aibu yenu wote. Mkifanikiwa basi ni Heshima yenu nyote. Mkishaanza kushindana ndani ya nyumba kuwa nani ni mkali, ili tu mkajisifu kwa marafiki zenu, basi huo mji ujuwe umekwisha. Fanya mahesabu yako vizuri na ukiamua kuowa, hata awe ni Mzee, kaa naye chini na mueleze nini unakitegemea kwake kama Mke na kipi akitegemee kwako kama mume.

Haya ya kupika, kuosha nguo kwani ni shida gani? Kama mkeo yuko kazini bado na wewe umerudi mapema, kwa nini usipike? Kwa nini usisaidie kusafisha nyumba? Unakuta mama na Mimba yake mtumbo huo, bado alikuwa kazini na akifika lazima apike, na jamaa limekaa tu kwenye TV linabadilisha Chanel za TV na kama Ngereja kakata umeme, basi katoka kwenda kupata Moja baridi na kitimoto. Kwa nini usiwe na huruma kwa mkeo na kumsaidia baadhi ya kazi? Unaogopwa kuchekwa kuwa "Mwanaume anapika" khaaaa!!!!! Kwanini unajali wanayosema watu wa mbali kuliko kujali anavyojisikia MKEO/MUMEO?

Mkiwa na wanawake/wanaume na hasa siku za mwanzo, waonyesheni hasa tabia zenu ili mwisho wa siku kusiwe na kulia/kusaga meno. Mtavuna mlichopanda. Ukiwa mkweli kwa mkeo, basi hatakuacha hata kuweje. Atakuwa na wewe na kukusaidia bila kujali anapata kipato kikubwa kiasi gani.

Nilishaona Film Documental ya Wageruman wanaoishi nje. Mmoja alikuwa kaolewa na M-Jamaica na wakawa wamehamia Jamaica. Mama ni meneja wa Mzinga wa hotel ya Kitalii na jamaa ni Mkulima. Mchana mama yupo kazini, gari zuri, ofisi safi na jioni anarudi nyumbani kwa mumewe na binti yake na nyumba hata umeme haina. Jamaa anaenda shambani kulima na kutunza mifugo, time to time anavuta JANI, anarudi mapema kupika na usiku wanapata wote chakula nyumbani (kumbuka mama kazini ana misosi mizuri tu). Ila kama Mwanamke kakupenda, basi ataacha kazi German, atakuja Jamaica na kwenda kuishi kwenye nyumba ya hali ya chini huku akiacha mazingira ya hali ya juu ambayo akitaka, muda wowote anaweza kurudi kuishi kwenye nyumba ya hali ya juu. Ila hilo siyo lengo la MAPENZI.

Mwingine aliyenifurahisha ni Mama President wa kampuni ya BOSCH akiitwa IZA BOSCH. Huyu mama na UTAJIRI wake woote, anaishi na Boyfriend aliyetokea Eastern German. Jamaa ni masikini sana. Anatembelea gari la kizamani mno la Easter German (Trabant). Sasa siku moja wanaonyesha jamaa ana Birthday na mama anahangaika kumtafutia zawadi. Angeliweza kumpa hata ndege akitaka ila mama anadai hiyo itamnyanyasa sana jamaa maana siku yeye akiwa na birthday, jamaa atakuwa anahaha amnunue nini yeye Iza ili afurahi? Mama alienda kiwandani na kuwaambia Wahandisi watengeneze chuma fulani cha ndani ya gari (pambo) ambalo jamaa alikuwa akikitafuta kwa siku nyingi. Siku hiyo jamaa alipopata kichuma cha TRABANT yake, alifurahi sana sana. Chuma hicho ni bei nafuu tu kama ukikipata kinauzwa. Jamaa alikuwa happy na kujua hata yeye hahitaji kununua kitu cha bei kubwa kwa sababu mama hana Complex nyingi na kufanya SHOW OFF.

Doo, unaweza kuandika GAZETI ila ukweli ni kuwa haya mambo hayana Formula. Unaweza kuowa mke wa RANGI yoyote ile na yakakupata. Kuna kaka yangu aliowa Mke huyoo, na tena ana asili ya Kisukuma, ni heri hata angelikuwa kaowa ngozi Nyeupe/Nyekundu/Njano.
Nina rafiki yangu, mwanaume, mzungu wake amecorp vizuri kweli, yuko kama mswahili kabisa hana shida, hadi ugali anajua kupika
 
Wengi waliooa wadhungu wanajuta kisirisiri. Kuna baba alioa mmarekani wakati akiwa masomoni huko miaka ya early 70s mwanamke alivyofika dar kaona maisha ndivyo sivyo karudi kwao na mtoto walozaa wote. Huyu baba ana life nzuri sana sasa hivi na ana familia (watoto wake ni rafiki zangu) lakini mpaka leo hajawahi kumwona mwanae na hajuhi hata atampataje. Watoto wake wa kibongo wenyewe wanasema tuna dada US ila hatumjuhi. Huyu baba anajutia muda wake alopoteza na huyu wife.

Kuna mifano mingi hasa ya wale waliooa wanawake wa ki russia wengi hawajuhi watoto wao kwani wake zao walisepa nao. Mara elfu kuolewa na mdhungu kuliko kuoa. Itakula kwako unless uwe na pesa kweli kweli ndiyo kidogo wanatia adabu.

Mifano iko mingi sana ya wanaume wabongo waliooa wazungu na kisha baada ya kuzaa wakakimbia na watoto

Halafu mwanaume anaoa tena bongo kujifariji na kutorokwa ,nasema wapo wengi,ingawa hii tu haiharamishi ndoa za hivyo,cha muhimu ni kuchukua tahadhari
 
He he heh!!! kazi kweli kweli!!! Bro ameishi Uingereza more than 10 years, juzi karudi nyumbani (bongo) kutafuta mke....coz kule kashindwa!!! Why? Wanawake wa kizungu wasumbufu sana.... ukitaka kuwa nao kwanza lazima akukondisheni uishi maisha anayotaka yeye.
 
Yah ni kweli chamoto wanakiona waliooa wazungu.lakini bora kuendeshwa kidogo kuliko kuwa na mbantu mwenzio huku ulaya anaenda Liwa tigo na wajanja mitaani kwa dola mia huko we unamenyeka job,na hata ukigundua huwezi mfanya kitu na anakwambia. Kabisa mguse akupeleke jela alipwe godis
 
Ktk kipindi chote nilichokaa US nimewahi kudate wazungu 11. Ni kama wanawake wengine ile one thing they have in common......personal hygiene yao ni mbovu sana! Balaa linakuja pale ukimkuta anafuga mbwa ama kajibwa hapo ndio kama una kinyaa basi utashindwa. Wanalala nao hawa dogs, wanawabusu, wanawa-hug, wanatembea nao kwenye magari basi ni shombo ya mbwa all the time. Ukienda bafuni ni manyoya ya mbwa ktkt bathtub. Nimlishindwa.
Ni wanawake ambao wako very caring. Akikupenda yuko radhi kuiga utamaduni wenu na hata vitumbua atapika na hata kangara atakunywa. Shida yao ni usafi wa mwili na nyumba na hayo majibwa yao
 
me naona kama ni mateso tu,wale watu dah
hata apite naked wala sistuki,....ila ipite ngozi nyeusi imeacha kimgongo tu doh,.....

Kuoa mdhungu ni shida,usizani anaeoa kampenda kweli.
mia.......
 
Acheni ubaguzi...

Mnabagua wageni...mnabagua wakwenu...mwisho wa siku mtajikuta mmezingirwa na hao mliokua mkiwasrma vibaya tu sasa sijui mtafumba macho mpendane nao au mtabaki mkishangaa tu!!

Wazungu kama waafrika tu wapo ambao ni wanapenda kumchukulia mwanaume kama kiongozi wa familia na ambao wanapenda wao ndio wawe viongozi.Hamna kitu/tabia yoyote ambayo ni sahihi wewe kuhusisha na kundi zima la watu wa aina fulani kwasababu hata siku moja huwezi kukuta watu wa aina fulani wote wakiwa na tabia zinazofanana ziwe nzuri au mbaya!!!

Kwahiyo anaetaka kuoa mzungu akimpata ambae anaona ni size yake acha aoe.,.acha kuharibia watu wengine bahati zao!!
huna exposure na umenikasirisha...
 
Mi naona nitabia ya mtu tu..as hata hao wanao kuja owa nyumbani bongo after papers wakija na walembo wao hapa baada ya mda utasikia wameashana kisa mnageria kaingia....tuache kuwa na uoga wamaisha nakutegemea kwa kuwa umeowa mzungu basi wewe umasikini basi....tuache kuwa wabaguzi ata hao dada zetu kama una mshiko wanakupotezea tu vile vile...tukubali kuwa na maamuzi magumu ya bilia kutegemea marafiki au ndugu kukuamulia maisha yako.......tuache ushabiki sio na maendeleo kwetu....ebu turudi na kuangalia mambo ya kujadili...nchi haina umeme,mafuta,elimu duni,cost of living is going up,uchumi umekufa na mambo mengi yamsingi kuliko wa mwanamke waki bantu au mzungu...
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom