Kuoa/kuolewa sio sababu ya kunenepeana

Kuoa/kuolewa sio sababu ya kunenepeana

Mndengereko

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2011
Posts
7,319
Reaction score
3,432
Heshima kwenu wanajamavi,poleni na mihangaiiko ya kujenga nchi sisi wengine tuko busy na kuibomoa. Moja kwa moja niende kwenye topic kuna trend inayoendelea hivi sasa kwa wanandoa unamkuta mwanamke mzuri anavutia ana kila kitu ambacho mwanamke mzuri inabidi awe nacho. Akishaolewa sasa ndo shughuli inaanza utukunyema unamkuta mtu ananepeana mpaka kero na ule uzuri wote uliomfurahisha muoaji/mumewe umepotea.

Haeleweki tumbo liko wapi na nyama za ubavuni ziko wapi ukimuuliza oooh nimeridhika maisha mazuri, mume wangu ananipa kila ninachohitaji na nakula vizuri. Sasa kama wewe unakula vizuri na Rihanna asemaje? au unataka kutuaminisha kwamba wewe unakula vizuri kuliko Angelina Jolie ila mbona wao bado wana miili yao ile ile.

Kula vizuri sio tatizo tatizo ni kupangilia kula kwako ili kumaintaina uzuri wako/shape yako. Sio ishu wala nini umeolewa ulikuwa mzuri unavutia mtoto wa haja mume wako alikuwa hakuchoki ana hamu muda wote atembee na wewe basi maintain hiyo hali (uzuri wako) ili usimpe vishawshi visivyo vya lazima mumeo na aendelee kukutamani all the time. Haijalishi mme wako ni mpole,mstaarabu au anakujali kiasi gani human being is selfish by nature kila mtu anapenda vitu vizuri so ni wajibu wako (sole responsibility) kumaintain uzuri wako ukijiweka hovyo mumeo anawezaa kutafuta vizuri.


Back to us boys/men na sisi kuna baadhi yetu wanajibweteka sana wakishaoa. Kabla ya ndoa tunajijali kula vizuri kwa wastani na vimazoezi viwili vitatu vya kudanganyia ilimradi kuweka mwili katika mpangilio. Shughuli inaanza mtu akishaoa anajisahau na kunenepeana hovyo mpaka unakuta mwanaume ana kitambi kikubwa kama mimba ya miezi minne kha!! Sio ishu wala nini ukimuuliza ana kwambia mama fulani fundi bwana anajua kukarangiza sijapata kuona.

binafsi hiyo haiwi sababu ya kutosheleza kuhalalisha unenepeanaji wako wa ghafla kama kuku wa broiler. Cha msingi ni kujipenda na kumaintain maumbo yetu.

Kwa kumalizia nisiwachoshe ni kwamba najua wengi wetu tukioa au wanawake kuolewa basi time hubana sana kutokana na ubusy wa majukumu ya kifamilia. Lakini ukweli jukumu la kumaintaini mwili wako na kukufanya uwe unaonekana kama wa mtu(romantic) ni letu wenyewe haijalishi upo busy kiasi gani. Na hili swala linatuhusu wote wala haijalishi kama ni mseja au umeoa/kuolewa.

Naomba kuwasilisha.

cc : ICHANA mwekundu Mr Rocky Tized Mashaxizo mshana jr Eshy m.s
 
Huku mtaani ndo wamezidi mkuu, kuna mrembo mmoja kaolewa hapa yaani alikua bomba balaa, akikupita lazima umsalimie, mwaka haujaisha kawa bonge hadi kukaa seat ya mbele kwenye carina hawezi, anakaa seat ya nyuma pekeake....
 
hahahha lols ,umeona eeh...yani ndo mana thread za namna ya kuwinda mume haziishi,siku mdada akimpata anajirestisha baada ya kazi nzito akishazaa ndo kabisaa,dah inatia huruma
Wanja, ma weaving, top dress tupa kule ni madira tu na twende kilioni lol....
 
Ndoa imekuwa kitu adimu sana kwa karne hii hadi inafikia kulazimisha/kulazimishana, ndo maana baada ya kuolewa mtu anabwaga moyo
 
Haaaaaaahaaaaaaaaahaaaaaaaaaa Mndengereko umeniacha hoi yaani six pack kabla ya ndoa baada ya ndoa mimba ya miezi minne yalaaaaahhhh.
 
Last edited by a moderator:
kuna ubaya gani mtu kunenepa,,uyo waliyeoana ndio wanajuana....ndoa na iheshimiwe na watu wote
 
Bora uwaambie wamezidi hawa. Unakuta ulikao kalikuwa modal lakin gafla linakuwa fukunyuku linaungana kwanzia kifua hadi makalio yaan mpaka kero kila ukijaribu kushika huku unakuta minyama uzembe aaaghrrr...... Mpaka unaona kinyaa kulisogelea. Kutana na kitu modal ya ukweli kama shemej N kila unapomuona hisia lazma zije
 
Last edited by a moderator:
Baada ya kuusoma huu uzi umenifurahisha ...kuna wimbo sijui nani kaimba ila unamaneno kama haya “Kimbaumbau kanenepa kawa kama tukunyema....“
 
Naungana na wachangiaje wengine ndoa imekuwa adimu sana siku hizi vijana tuko busy kujipanga na maisha ndo maana mwanamke akiolewa anaridhika kwamba keshaweka shida chini
 
hahaha Mndengereko maisha ya bongo ni magumu sana kujiweka juu si kazi ndogo wallah sasa ndo umepata mume ukikohoa tu waulizwa nini shidaa kwanini nisinenepe kila kitu unapewa acheni tujiachie lol
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom