Kununua gari au kujenga nyumba

Kununua gari au kujenga nyumba

Watu wengi wenye hela hawakimbilii kujenga. Kujenga kuna cost na kufilisi asikwambie mtu! Kwa mishahara mliotaja hapo ni wazi kama wanataka kujenga na kiwanja hawana itawachukuwa muda kumaliza nyumba na inaweza isiishe. Nawashauri wanunue gari ya biashara iwe inaleta hesabu na kupitia gari hiyo wanaweza kujenga!
 
mi nlinunua gari 2008 sikupata hizo shida hata kidogo for 2yrs, hivi wenzangu mwanunua make gani mbona mnacomplain complain? au ni 3rd hand cars!!
Jerrymsigwa inawezekana kwa kweli...mm mwenyewe gari yangu hainicost kiasi hicho..liko very friendly....cha kushangaza GARI HANA lkn anatuletea hesabu zisizo na mshiko...mimi gari yangu bajeti yake nI 160 tuu kwa mwezi..na service ni baada ya 3month maximum cost 80...ss hizo hesabu zake za wapi
 
Last edited by a moderator:
linachosha acha tu........mie sina pesa tu ila ningekuwa nazo kitu cha kwanza ingekuwa gari hayo ya nyumba

yangefatia baadae saaaaaaaaana
Heaven on Earth mshahara wote unaolipwa huo shoger hujaamua.jibane bane bana sio kula mapizza kila siku....punguza shopping...brazilian....si kila fashion lazma uwe nayo...kwa mwaka tu utaweka hela ya maana...sikushaurI ukope🙂🙂🙂
 
Last edited by a moderator:
bora gari hata ukifa utaenda kuchukuliwa nalo motchwarii!!!

bora gari ukiumwa utakimbizwa nalo hospital nyumba utafia ndani

gari inakukutanisha na watu wengi na unajifunza mengi chanel zinaongezeka duuu mafanikio kibao

gari inakula mafuta nyumba inakula umeme mapato ya ardhi nk
 
hii imekuwa tamu zaidi tumpe na jibu lingine
afikirie ni kwa jinsi gani anaweza kuongeza kipato ambacho kitamwezesha kuendesha gari bila usumbufu wowote mfano awe na mradi ambao unaweza kuingiza net 20,000 ambayo inaweza kutumika kununulia mafuta kisha aendelee na nyumba!
gari kwa kweli lina raha yake mimi mwenyewe huwa naona gharama ninazoingia inaponilazimu kukodi au kujikanyagakanyaga kuazima gari kwa rafiki yangu kama imetokea dharura kwani wakati mwingine hunilazimu kurudisha gari half tenk ili kesho ufikiliwe tena.
lakini ule ajali iliniuma sana na bima zetu za kushikisha ndo inafanya nimshauri mtu nyumba kwanza.
mwisho nyumba inalipa hataiweje na ni kujitoa kwa maana mno
 
Ushauri ni kua atafute kiwanja anunue, kisha anunue hilo gari kwa sababu viwanja vinapanda sana bei kila kukicha pia ni rahisi kuanza ujenzi kama unakiwanja. Hii inamaana utajenga kwa awamu tena kwa kudunduliza mfano msingi ukafata kozi nne, ukamalizia hadi kumi, ukafuata renta na kozi mbili, ukapaauwa kisha finishing taratitaratibu kulingana ela unayopata. nyumba huwa inajengwa hata miaka 10 ila inaisha maana kila hatua huwa inapita. Pia gari ni liability tena ni vampire ktk pesa kama haliingozi pato.

Well said
 
Waoga wa maisha huanza na nyumba ila kwa watu jasiri gari kwanza mengine baadae. Ukiwa na gari kwanza waweza kodisha, networking, unakopesheka, kama ni mtu wa skirts basi gari ni sumaku.

Gari kwanza mengine baadae,acha woga kijana
 
Kupanda kwa viwanja sio ishu si salary zinapanda jmn? Acheni woga jmn, hakuna raha ka kuwa na gari, hata viatu haviishi sana na dada zetu vile viatu high heels unaeza vaa(kwa dada zetu)
Ok amka basi ukojoe uende kanisani.
 
Ok amka basi ukojo uende kanisani.

ImageUploadedByJamiiForums1391229508.318239.jpg

Wewe sasaivi ni sa tisa mchana niamke kivipi?
 
Watu wengi wenye hela hawakimbilii kujenga. Kujenga kuna cost na kufilisi asikwambie mtu! Kwa mishahara mliotaja hapo ni wazi kama wanataka kujenga na kiwanja hawana itawachukuwa muda kumaliza nyumba na inaweza isiishe. Nawashauri wanunue gari ya biashara iwe inaleta hesabu na kupitia gari hiyo wanaweza kujenga!

Edson nafikiri mtazamo wako hauko sahihi sana kimahesabu na kimantiki.

Watu wengi wamejenga nyumba mijini kwa kipato cha chini zaidi ya hicho cha hao jamaa.
Binafsi naona kabisa kwa kipato hicho wanaweza kujichanga na ndani ya miaka miwili wakawa na Nyumba ya Kawaida ya Vyumba vitatu(Yenye wastani wa thamani ya Milion 12). Hii inawezekana sana!!

Kimantiki hawa jamaa wanataka Nyumba ya kuishi au Gari la kutembelea na sio kwa biashara.

Otherwise Maisha ni Nyumba na sio Gari.
 
Last edited by a moderator:
Wanunue gari halafu waiuze wanunue nyumba

Duh!! Imebidi nicheke tu. Yaani wanunue Gari kisha waiuze wanunue Nyumba!
Vipi kama watajenga nyumba halafu waiuze ili wanunue gari?

Unajua ndugu yangu kuna maswali mengine humu huwa yanaulizwa, ukikaa ukafikiria vizuri unaona kwamba aliyeuliza swali anakuwa aidha amepitiwa au ni "tabular rassa". Kwa mfano mtu akija na swali akauliza "Naomba ushauri kama ili niishi nahitaji kufanya kazi ama la", mtu kama huyu utamjibuje? Jibu zuri ni kumwambia possibly anatakiwa aishi kwanza bila kufanya kazi, kazi atakuja kufanya baada ya kuishi. Those are the best answers such a person you help him/her with!
 
Hahahahaaaaa wanadhani milion Saba unajenga nyumba!!!!! Narudia tena ukinunua Gari kuukuu ujie gharama za uendeshaji zitakua kubwa....ukiwa na Gari that means unauwezo WA kujenga pia. Ni suala la priority na Sababu za kukufanya ununue gari

Acha kupotosha mkuu, kipato chao kimewekwa wazi halafu unasema wakiweza kununua gari wataweza kujenga????
Kimsingi kwa kipato walichonacho wajue wakinunua gari itawachukua muda sana kujenga au wasiweze kabisa. yamkini hata gari yenyewe inaweza kuwa inapatikana barabarani siku chache sana za mwezi...
 
Acha kupotosha mkuu, kipato chao kimewekwa wazi halafu unasema wakiweza kununua gari wataweza kujenga????
Kimsingi kwa kipato walichonacho wajue wakinunua gari itawachukua muda sana kujenga au wasiweze kabisa. yamkini hata gari yenyewe inaweza kuwa inapatikana barabarani siku chache sana za mwezi...

Sa wafanyeje? Life is living today not tomorrow, nunueni gari mlete heshima mtaani banaa
 
Inawezekana kununua gari na kiwanja,tatizo ni kama unataka kiwanja katikati ya jiji.nyumba utajenga mwakani au mpango wa fedha ukikaa sawa
 
Back
Top Bottom