Kununua gari au kujenga nyumba

Kununua gari au kujenga nyumba

Nunueni kiwanja kwanza muwe na uhakika kwamba mkipata nguvu mtajenga,kwasababu ardhi inapanda bei kila kukicha na maeneo mazuri yanazidi kuchukuliwa unless mnataka kujenga chalinze.Japo pia wazo la kujenga kwa kipato hicho itawagharimu hata miaka 15 labda kama mnataka kujenga mahala pa kujihifadhi sio nyumba ya kisasa.

Kama mnakopesheka,nendeni taasisi za kifedha mchukue mikopo itawasaidia kukimbizana na value for money na kusogeza malengo yenu.
 
Jamani mie naona aanze kwanza na kiwanja. Mimi nilianza na kiwanja baadae msingi na sasa natafuta hela ya finishing. siku baba mwenye nyumba akisema toka naenda kwangu. nikiwa kwangu natafuta hela ya gari sasa. maisha yana changamoto ambazo haziepukiki jamani ada hiyo na january hii ngoja nifanye kazi kama mtumwa mie.
 
Kwa hali ya dar usafiri muhimu saanaa....inakurahisishia mambo yako mengi mno..wanunue gari ya wastani tu ila pia kiwanja wanacho.?????..sio wanunue gari ht shamba la laki8 hawana...I dont regret having a car...ingawa nilianza nunua shamba/kiwanja kabla ya gari....
kwani amekwambia ana mishe za kuzunguka na hiyo gari.
kama utajenga nyumba ya 30-20m uwezi kushindwa kununua gari ya 4-7m zingatia ukinunua gari utakuwa na running cost za gari ambazo zipo juu na za nyumba ya kupanga na itakulazimu kupanga nyumba nzima ili u mechi.
go for the building
 
Jamani mie naona aanze kwanza na kiwanja. Mimi nilianza na kiwanja baadae msingi na sasa natafuta hela ya finishing. siku baba mwenye nyumba akisema toka naenda kwangu. nikiwa kwangu natafuta hela ya gari sasa. maisha yana changamoto ambazo haziepukiki jamani ada hiyo na january hii ngoja nifanye kazi kama mtumwa mie.
alafu unaweza kununua gari hata hamu hija kuishwa inagongwa na wewe ndio mwenye makosa.
na maanisha risk ya gari ni kubwa kuliko risk ya nyumba
 
Mimi nawashauri waanze na gari flan simple isiyokula mafuta sana. Itawasaidia sana na amini usiamini itawaongezea hata confidence na self asteem watajikuta wanabuni hata mbinu za kuongeza kipato. Mimi nilianza na gari 3 yrs ago, baadae kiwanja na nikajikuta nimejenga niko kwangu. Ukiwa na gari bana kuna furaha flani unakuwa nayo! Chukulia mmetoka kidogo wewe na wife mkakaa na washikaji pale Calabash. Mnakaa labda kimara au tabata, hapo tu mlipokaa mnawaza jinsi ya kuondoka, taxi expensive, daladala ndo hivyo tena mnafika hoi. Katoto kakipata homa ghafla usiku unakawahisha fasta hospital, mkwe kakutembelea kumchukuwa au kumpeleka kituoni siku anafika au kuondoka.......ziko faida nyingi kwa kweli ukiwa na kausafiri!
s
Mods naona button ya LIKE nashauri iwe na ya DISLIKE
 
Gari ni rahisi sana kununua tatizo linakuja katika kulitunza kwa wastani gharama za kuendesha gari hazipungui millioni tisa kwa mwaka ikiwemo wastani wa mafuta ya shillingi 15,000 kila siku inayofanya kuwa 450,000 kwa mwezi na kwa mwaka 5,400,000/- achilia services zenye wastani wa 100,000/- kwa mwezi barabara zetu si unazijua! hivyo kuna 3,600,000/- bado gharama za pack mjini kila siku kama 600/- kupaki jioni 1000/- au mlinzi kuosha gari 2000/- kwa siku.
lakini lililo tamu zaidi ni mitoko ya hapa na pale mama atataka kila harusi mchange ili muende kutembelea familia na mengine zaidi.
ki ukweli nilipokuwa na gari sikuweza kuanza ujenzi ila mara baada ya kupata ajali na gari kuwa haifai kabisa ujenzi ukaanza tena. hivyo achana na gari kwanza wacha watu wakucheke lakini lazima ujue nini unataka

ujenzi ni rahisi sana unaweza kuamua kununua matofari au kufyatua inategemea
tenga kila wiki 60,000 kwa tofari moja shillingi 1000/- utapata matofari 60 kwa mwezi matofari 240 kwa miezi sita 1,440 ambayo haya yanaweza kukusaidia kufikisha nyumba kiunoni.
au nunua nifuko minne kila wiki kwa shilling 60000 itaongezeka kidogo kila mfuko tofari 35 kwa mifuko minne tofari 140 kwa mwezi tofari 560 kwa miezi sita 3660 zinatosha kwa kiasi kikubwa kujenga nyumba ya kawaida.
jipange kwa mpango uleule weka hela ya ujenzi baada ya kukusanya matofari kwa miezi sita na anza ujenzi

Mmhh kaka me nnamiliki gari lakinI sI kwa mahesabu yako..service kila mwezi 100000???.kwahiyo mil9 kwa mwaka maana yake gari inakost kwa mwezi 750000 realy.?? Labda unamiliki gari ipi mwenzetu....me yangu walaaaa
 
Nunua pikipiki kwa ajili ya kusimamia ujenzi(kufuatilia kazi site etc). Ukimaiza ujenzi unauza hiyo pikipiki au inakuwa bodaboda ukiwa unatafuta gari.
 
Ukiwa na nyumba inaongezeka thamani kadri miaka inavyosonga wakat gari linashuka thamani.
 
me naona kama hela wanazo n bora waanze ujenzi kidogo kidogo na kama kuna ya ziada basi wachukue economise car wanao jua wamsaidie itawarahisishia mizunguko yao ya hapa mjini.....

ila aisee nyumba muhimu

gari linakula kila siku kama wewe....

linaumwa linahitaji matibabu na likipigwa linaumia halitaki kutembea likiwa limeumia ..

lisipofanya kazi au kutumika linakufa duh!!!!!
 
Habari wadau, Nina rafiki yangu wa siku nyingi alinifuata hivi karibuni kuniomba ushauri, yeye ameoa na wamebahatika kupata watoto wawili, kwa sasa anaishi nyumba ya kupanga. Ameniambia yeye na mkewe wapo katika malumbano ya kuhusu kipi waanze kukifanya kati ya kununua gari ama kununua kiwanja na kuanza ujenzi!! Kipato chao kwa mwez jumla huwa kati ya sh lak 8 hadi mil 1 na lak 2. sijui ndugu zangu mngewashauri waanze na ujenzi au gari?
kheeee?! ujenge nyumba?? kwa mshahara huo au?,hakika kama huna kipato kingine cha pembeni usije ukathubutu kuanza kujenga na huo mshahara,labda ujenge kwa miaka 6 na zaidi na apo kuna kufika katikati ela inakata mwisho wa siku hata matofali uliyopandisha yanaanza kuchakaa,nyumba inachoka hata kabla haijamalizika.

USHAURI WANGU:
mi naamini kabisa toka uzaliwe hujawahi kulala nje kwa maana umekosa nyumba..ila tangu uzaliwe mpaka leo unatembea kwa miguu tu...NUNUA gari litakusaidia katika mishemishe zako za kutafuta mshiko,kulala utalala tu haimaanishi kwamba usipojenga ndo utalala nje!!
 
Yeye kama mume anataka Gari au nyumba.Je Mke anataka gari au Nyumba??
 
Heshima Kwako Afande..
Ushauri Muhimu kabisa waanze na Nyumba kwa sababu:
1/Nyumba ni mali isiyohamishika hivyo ni dhamana muhimu mahali popote pale duniani iwe Mahakamani, Benki, Biashara, Maishani, Kazini nk.

2/Thamani ya Nyumba inakwenda inaongezeka kila siku(Hata siku wakitaka kuiuza wataiuza kwa thamani kubwa zaidi).

3/Watakuwa wameondoa gharama za kupanga na usumbufu wake(Watakuwa huru sana)

4/Nyumba ni Akiba ya kudumu maishani(Wataishi wao na vizazi vyao)

5/Nyumba ni kipimo cha Heshima, Hekima, Busara na Upeo kijamii, kifamilia, kimila, kiserikali nk.

6/Nyumba ni Mtaji wa Maisha(Hawatatoa tena pesa zao kila siku au kila Mwezi kulipia gharama za kuishi kwenye hiyo nyumba zaidi wanaweza kupata kipato zaidi kama sehemu ya hiyo nyumba watapangisha)

7/Nyumba inaweza kuwaletea vitu vingine vingi kama Gari kama watafanya mahesabu vizuri(Kwa mfano wanaweza kuitumia kama dhamana katika taasisi za kipesa kukopa pesa za kununulia gari nk.)

NOTE;
Kwanini wasianze na Gari:
A/Gari inahitaji gharama kubwa sana kulihudumia(Kwa mfano Insurance, Kodi ya Mapato, Mafuta ya kila siku, Service ya kila mara, Parking ya kila siku, Trafiki, Vipuri nk)

B/Gari itakuzidishia gharama zaidi za maisha pasipo msingi.(Mfumo wako wa maisha unaweza ukabadilika ili kukidhi tu fahari ya kumiliki gari. eg.Kula, kuvaa, Makazi, matembezi, Marafiki, Ndugu, Jamaa nk.) Hili jambo nimeliona kwa watu wengi sana mijini. Kifupi Gari halipatani sana na mbana matumizi!!!

C/Thamani ya Gari mara nyingi inakwenda ikipungua tokea ile siku unalimiki.

D/Gari ni chombo kinachochakaa kwa upesi sana kadri siku zinavyokwenda au unavyolitumia(Mara nyingi magari mengi yanakuwa yameanza kuchakaa vibaya baada ya miaka mitatu tu!!)

E/Gari lina tabia ya kukugeuza kuwa Mtumwa wake(Kwa mfano Wakati wote litakuhitaji kutoa pesa zako mfukoni ili uweze kulitumia). Kifupi Gharama za Gari ziko juu zaidi wakati wa kulitumia kuliko hata wakati wa kulinunua!!
 
Kwa kipato hicho ni bora watafute kiwanja waanze ujenzi...

Kuwa na gari ni kweli sio anasa lakini matunzo ya gari ni makubwa na mwisho wa siku wanaweza wakajikuta wanaishia kwenye nyumba za kupanga...

Ushauri wangu utabadilika kama kuna vyanzo vingine vya mapato zaidi ya hivyo ulivyotaja...
Well said. Kwa kipato hicho, mshahara wote utaishia kwenye gari, na nyumba wataisikia kwenye bomba.
 
Mleta mada kununua gari wakati kipato chako kidogo ni kitendo cha kuukaribisha umasikini uje kwa nguvu
ushauri hawa wanatakiwa waanze kujenga mapema kabisa ili waondokane na adha ya mambo ya upangaji na kabla hawajabanwa na majukumu makubwa sana ukiwa na nyumba huo ndio uanaume na ndio unaonekana unaakili kuliko kununua gari ya kujionyesha na halileti kitu chochote tofauti ya kuongeza matumizi tu
Habari wadau, Nina rafiki yangu wa siku nyingi alinifuata hivi karibuni kuniomba ushauri, yeye ameoa na wamebahatika kupata watoto wawili, kwa sasa anaishi nyumba ya kupanga. Ameniambia yeye na mkewe wapo katika malumbano ya kuhusu kipi waanze kukifanya kati ya kununua gari ama kununua kiwanja na kuanza ujenzi!! Kipato chao kwa mwez jumla huwa kati ya sh lak 8 hadi mil 1 na lak 2. sijui ndugu zangu mngewashauri waanze na ujenzi au gari?
 
Mleta mada kununua gari wakati kipato chako kidogo ni kitendo cha kuukaribisha umasikini uje kwa nguvu
ushauri hawa wanatakiwa waanze kujenga mapema kabisa ili waondokane na adha ya mambo ya upangaji na kabla hawajabanwa na majukumu makubwa sana ukiwa na nyumba huo ndio uanaume na ndio unaonekana unaakili kuliko kununua gari ya kujionyesha na halileti kitu chochote tofauti ya kuongeza matumizi tu

sawa mkuu!
 
kheeee?! ujenge nyumba?? kwa mshahara huo au?,hakika kama huna kipato kingine cha pembeni usije ukathubutu kuanza kujenga na huo mshahara,labda ujenge kwa miaka 6 na zaidi na apo kuna kufika katikati ela inakata mwisho wa siku hata matofali uliyopandisha yanaanza kuchakaa,nyumba inachoka hata kabla haijamalizika.

USHAURI WANGU:
mi naamini kabisa toka uzaliwe hujawahi kulala nje kwa maana umekosa nyumba..ila tangu uzaliwe mpaka leo unatembea kwa miguu tu...NUNUA gari litakusaidia katika mishemishe zako za kutafuta mshiko,kulala utalala tu haimaanishi kwamba usipojenga ndo utalala nje!!

usumbufu wa baba mwenyenyumba ni zaidi ya kulala nje!
 
Ufafanuzi zaidi unahitajika. Hatujaelezwa kama hizo pesa za kununulia gari au kujengea zitapatikana kwa mkopo au akiba (savings).

anamalengo ya ku save kiasi cha mapato yake ya mwezi ambapo kwa hesabu za haraka mwaka mmoja hakosi milion 7 hadi 9 ukiondoa matumizi!
 
Back
Top Bottom