Kununua gari au kujenga nyumba

Kununua gari au kujenga nyumba

kupanga ni kuamua...km wana watoto tayari...waanze kujenga sasa sababu hakuna anayetaka kukaa nyumba ya kupanga na watoto wakubwa...ila km bado hawana watoto wanunue tu gari..then ndio waanze plan ya kujenga.
 
Habari wadau, Nina rafiki yangu wa siku nyingi alinifuata hivi karibuni kuniomba ushauri, yeye ameoa na wamebahatika kupata watoto wawili, kwa sasa anaishi nyumba ya kupanga. Ameniambia yeye na mkewe wapo katika malumbano ya kuhusu kipi waanze kukifanya kati ya kununua gari ama kununua kiwanja na kuanza ujenzi!! Kipato chao kwa mwez jumla huwa kati ya sh lak 8 hadi mil 1 na lak 2. sijui ndugu zangu mngewashauri waanze na ujenzi au gari?

Samahani mi naomba nimuulize maswali machache kabla sijamshauri. Kwanza inabidi aseme mpaka sasa ana kiasi gani cha kufanya hicho anachotaka? Maana kataja kipato chake kwa mwezi pengine anakula chote? Nikiwa na uzoefu kidogo kwenye mambo ya ujenzi hivo vitu havina comparison maana gari kuna ambayo 3rd hand unaweza pata hata kwa 3m but nyumba hadi uingie ndani na wewe unasema naishi kwangu si chini ya 30m kwa kijana wa kipato kama hicho. Sasa hapo cjui anaweza kuanza na lipi? M3 akianza jenga anaishia msingi nao hujaisha kwa nyumba ya kawaida ya kijana wa kipato kama chake so it will take him 5 years akiwa na savings ya 5 kwa mwezi kukamilisaha nyumba ya kiasi nilichosema hapo juu. Hapo toa gharama ya kiwanja maana hilo ni gari jingine. Na hata gari wengine wananunua kurahisisha shughuli fulani ili kujiongezea kipato. Ni hayo tu
 
Mimi ningewashauri watafute kwanza kiwanja, halafu wazichange tena watafute gari la kawaida. Wakishakua na kiwanja na gari waanze ule ujenzi wetu wa kimaskini. Nyumba itachukua muda mrefu, lakini itaisha. Wakiendelea kupoteza muda wakumbuke watoto watahitaji kwenda shule, hivyo kipato chao kitazidi kupungua
 
Samahani mi naomba nimuulize maswali machache kabla sijamshauri. Kwanza inabidi aseme mpaka sasa ana kiasi gani cha kufanya hicho anachotaka? Maana kataja kipato chake kwa mwezi pengine anakula chote? Nikiwa na uzoefu kidogo kwenye mambo ya ujenzi hivo vitu havina comparison maana gari kuna ambayo 3rd hand unaweza pata hata kwa 3m but nyumba hadi uingie ndani na wewe unasema naishi kwangu si chini ya 30m kwa kijana wa kipato kama hicho. Sasa hapo cjui anaweza kuanza na lipi? M3 akianza jenga anaishia msingi nao hujaisha kwa nyumba ya kawaida ya kijana wa kipato kama chake so it will take him 5 years akiwa na savings ya 5 kwa mwezi kukamilisaha nyumba ya kiasi nilichosema hapo juu. Hapo toa gharama ya kiwanja maana hilo ni gari jingine. Na hata gari wengine wananunua kurahisisha shughuli fulani ili kujiongezea kipato. Ni hayo tu

Acha kumdanganya mwenzio na magari 3rd hand. Gharama zake ni kubwa maana nyingi zimeshachoka. Na hio nyumba ya chini ya mil 30 ndio ikoje?? anyways, nyumba hata ikichukua miaka 5 mwisho wa siku utahamia kwako na kuepuka gharama za kodi na kero nyingine
 
[QoUOTE=Mfa maji;8567510]Acha kumdanganya mwenzio na magari 3rd hand. Gharama zake ni kubwa maana nyingi zimeshachoka. Na hio nyumba ya chini ya mil 30 ndio ikoje?? anyways, nyumba hata ikichukua miaka 5 mwisho wa siku utahamia kwako na kuepuka gharama za kodi na kero nyingine[/QUOTE]
mtoa mada fuata yako tu hapa utachanganyikiwa tu
 
hakuna baba mwenye gari kuna baba mwenye nyumba,na heshima ya mjini nyumba ukiwa na nyumba unauwakika wa kuishi mjini
 
Waoga wa maisha huanza na nyumba ila kwa watu jasiri gari kwanza mengine baadae. Ukiwa na gari kwanza waweza kodisha, networking, unakopesheka, kama ni mtu wa skirts basi gari ni sumaku.

Gari kwanza mengine baadae,acha woga kijana

Hahahahaha
 
hakuna baba mwenye gari kuna baba mwenye nyumba,na heshima ya mjini nyumba ukiwa na nyumba unauwakika wa kuishi mjini

Haya mawazo ya kiswahili sana, 'ukiwa baba mwenye nyumba what next' yani uwe na nyumba kisa kuitwa baba mwenye nyumba?
 
Chenye umehimu hapo ni nyumba tu...Gari maumivu kwa mshahara huo....kwasababu gari itahitaji kwenda service, mafuta kila wiki, bado ujapata emergency....mwisho kabisa gari siku yoyote limepata ajali ndio mwisho wake...bora ya nyumba unawekeza hta watoto watakuja kuiona...Magari kila siku yanatoka mapyaa! NYUMBA NDIO KILA KITU.
 
Kama wana kiwanja waanze ujenzi...lkn kwa kipato hicho kama hina kiwanja.huna gari na unataka kujenga...bora ununue gari ufe kijerumani na tai shingoni.

Unaweza kupata kiwanja chamazi au mabwepande...utafikaje mkuu wakat unaendesha huo ujenzi wa kimasikini?....sidhani kama kwa sasa unaweza kujenga nyumba ya vyumba 3 kwa gharama ya chini ya 25M...yeye ana watoto wawili huwezi kujenga polisi posti watoto watalala vp wanakua bado mkweo hajaja kusalimia.

Mungu awe nasi maisha haya bila kuwa fisadi hata kdg hujengi...mshahara hautoshi kbs.
 
hiyo nyumba ya kupanga ina parking au ndio kwenda kupaki ccm?
 
Ukiona mwanaume kanunua gari wakati hana nyumba na wala hana uwezo wa kuijenga, basi ujue kichwani kwake hamna kitu! Kumbuka, mahitaji makuu ya Mtanzania yanaainishwa kuwa ni Chakula, Mavazi na Malazi(Nyumba)! Lakini pia, wajua nyumba inaongeza thamani kila kunapo kucha, wakati gari linapungua bei kila kunapokucha! Zaidii, hakuna gharama za uendeshaji nyumba, bali kuna gharama za uendeshaji gari! Na mwishooo, duniani koooote, hakuna Baba mwenye Gari, bali kuna Baba mwenye Nyumba!NB; HESHIMA YA MWANAUME NI NYUMBA, GARI (BILA NYUMBA) NI HESHIMA YA WAVULANA!
 
Te te teeee aiseee mkuu hapo kwenye 'wavulana' umetumia vigezo gani, dah 😄😄
 
hakuna maisha rahisi kama kuwa na gari. Binafsi nilianza na gari. Kuna siku nilikuwa na mizunguko mjini ofisi kama tatu, nilichukua teksi nikaenda pa kwanza, nikarudi,nikaenda pa pili nikarudi, pa tatu, wakaniambia rudi saa8, nikakimbia ofisi kwetu, saa 8 nikaita teksi iyo na kwenda...mizunguko yote haikuzidi kilometre25, jamaa akaniltea bill ya shilingi elfu 39,000 na waiting charge 5,000/= , sikukaa mwezi nikaagiza gari.
Ushauri tu kwa vijana wenzangu wanaoona future kuwa itakuwa nzuri basi jaribu ivi,
Nunua gari dogo lenye consumption ya fuel kuanzia km 10 per litre,mpaka 12, u shall never regret, service km 3000 sh 50,000 wakati kwa teksi hapo unadaiwa kama laki8 ivi,
Ujenzi utakuja wala usiwe na haraka.
Taadhari: Kama kipato chako ni kidogo,chini ya lak350,000/= tafadhari tumia daladala wala sio teksi wala kunua gari, sio dharau au kejeli bali ndo ukweli, fikiria hesabu ya haraka 350,000*12= 4.2 mil per year, hapa service tuweke hata laki200,000/= spea tuseme tu sh laki300 per anum na fuel laki6 p.a parking kwa mjini 360,000 na ule , ulishe familia. Kwa gari tayari ishakula minimum 1.5 mil, kodi tuseme una familia rum 2 tu sh 100,000/= thus 1.2 mil hapo utalia na kutupa gari.

Ila kama kipato ni kuanzia lak5, wakuu achana na taksi na daladala, tumia usafiri rahisi, private drive,
faida zake:
-Utaenda kokote kwa muda wowote unaotaka
-utasevu ela badala ya kutuima taksi km2 sh elf7 utatumia sh 500 kwa mafuta ya gari/ robo litre.
-Badala ya kukimbilia daladala na kuchafuka na kusababisha kufua kila siku, waweza kufika unakoenda unanukia,kiatu baniani mbaya, pasi bado nguo imesimama, nk nk
-Utasimama unapotaka na kuondoka unapoamua, eg unatoka posta kwenda pugu, unapitia kinondoni unasolve ishu, unaenda magomeni unamuona anayekusubiri, unapitia ubungu unabeba mifuko yako ya simenti3,.... nakuambia kwa daladla posta kinondoni 400 na umechafuka vilivyo, kino mpaka magomeni 400 na matusi ya konda, magomeni ubungo 400 umelipa elfu5 na konda anabisha eti change kashakupa,ubungo kwenda pugu na mifuko ya sementi 3 utalia na kusaga meno na route hii inakugarimu masaa 5 wakati private ni lisaa limoja tu.

utani//Kama haujaoa kama Gsana, aah aah ah nakuambia utang'oa chuma cha ghorofa, kama mtarajiwa hautawaza kumfuata moro au masaki au mkuranga, miguu minne haichezewi.

All in all, gari ni lubricant na access device ya other all activities you plan.

OMBI: ACHANA NA TAKSI VIJANA WENZANGU,TUTUMIE HII NJIA MBADALA.
Binafsi sina pesa ya kupandia taksi ndo maana nikanunua mwananjenje!bata mweupeeee!
 
Mi nadhani jama wanunue gari tu sababu project ya ujenzi ni life time project utajenga kwa miaka mi5 hata,kwa sababu kwa kipato chao cha mil 1.2 kwa mwezi hawawezi

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Ukiona mwanaume kanunua gari wakati hana nyumba na wala hana uwezo wa kuijenga, basi ujue kichwani kwake hamna kitu! Kumbuka, mahitaji makuu ya Mtanzania yanaainishwa kuwa ni Chakula, Mavazi na Malazi(Nyumba)! Lakini pia, wajua nyumba inaongeza thamani kila kunapo kucha, wakati gari linapungua bei kila kunapokucha! Zaidii, hakuna gharama za uendeshaji nyumba, bali kuna gharama za uendeshaji gari! Na mwishooo, duniani koooote, hakuna Baba mwenye Gari, bali kuna Baba mwenye Nyumba!NB; HESHIMA YA MWANAUME NI NYUMBA, GARI (BILA NYUMBA) NI HESHIMA YA WAVULANA!

nahisi unashindwa kuelewa mada mkuu, apa ni kipi kianze na sio kipi kiachwe milele...Ukiitwa baba mwenye nyumba ianongeza nini?hesjima?utaila heshima? na eti hakuna gharama ya uendeshaji nyumba, uko serious kweli?una nyumba?au zile za vijijini?maana uku sisi wenye nyumba lazima tulipie pango la serikali kwa mwaka, annual fee. Alaf mkuu nyumba sio kuwa maanake ni malazi, malazi ni mahala pa kuishi, hata ukipanga unaishi.
Gari ianze nyumba ifuate...ni maoni yangu tu! by Mvulana, Gsana wa jf, Baba mwenye nyumba na mvulana mwenye gari,ah ahah!
 
KIDOLEGUMBA waambie waanze kutafuta kiwanja wajenge nyumba yao, muda huu tayari wana watoto wawili na bado wapo nyumba ya kupanga na bado watoto wengine wanakuja (cz wataendelea kuzaa), nyumba zenyewe hizi kila mwaka kodi inapanda kuna muda vyumba viwili / vitatu havitoshi.

Pia endapo atanunua gari lazima awe na mahali pa kupaki kama hiyo nyumba waliopanga haina parking ndio hilo gari litalala ccm au kituo cha kulaza magari, uwezo wa kufanya maintenance ya gari, mafuta kilasiku, insurance na trafiki barabarani. Ni bora akawa mvumilivu kwa kuendelea kupanda daladala muda huu.
 
Last edited by a moderator:
Haya mawazo ya kiswahili sana, 'ukiwa baba mwenye nyumba what next' yani uwe na nyumba kisa kuitwa baba mwenye nyumba?

aya ni zaidi ya kiswahili mkuu...watu wanalewa sifa...utasikia yule waziri yule si alikuwa anaishi kwangu wakati anasoma udsm, yaani mm nilikuwa nikirudi home hakooi, uyu dogo uyu ananijua!mimi ndo mwenye nyumba wake wa kwanza bhana,so what?watu wanalewa sifa!
 
hiyo nyumba ya kupanga ina parking au ndio kwenda kupaki ccm?

aah aah aah kupark ni ccm mkuu, buku kwa siku1, ila ujue 100% ya nyumba za mjini tuseme magomeni hata si zaidi ya kadirio la 20% ndo zenye parking. Sisi na wenye nyumba woote tunakimbilia na tunagombania parking ccm!
 
Nyumba kwanza gari baadaye. Huwezi kamwe kulinganisha Gari na Nyumba, Nyumba ni zaidi ya Mali. Hiyo ndio hekima na sio ufahari. Maisha ni kupanga na sio kuiga.

Una mke na watoto, anza kuwaza kuwa na Nyumba kwanza kwani ipo siku uchumi wako unaweza kuyumba au Ukafariki dunia, sijui Mkeo na watoto wako watakuwa wapi?
 
Back
Top Bottom