Ushauri Muhimu kabisa waanze na Nyumba kwa sababu:
1/Nyumba ni mali isiyohamishika hivyo ni dhamana muhimu mahali popote pale duniani iwe Mahakamani, Benki, Biashara, Maishani, Kazini nk.
2/Thamani ya Nyumba inakwenda inaongezeka kila siku(Hata siku wakitaka kuiuza wataiuza kwa thamani kubwa zaidi).
3/Watakuwa wameondoa gharama za kupanga na usumbufu wake(Watakuwa huru sana)
4/Nyumba ni Akiba ya kudumu maishani(Wataishi wao na vizazi vyao)
5/Nyumba ni kipimo cha Heshima, Hekima, Busara na Upeo kijamii, kifamilia, kimila, kiserikali nk.
6/Nyumba ni Mtaji wa Maisha(Hawatatoa tena pesa zao kila siku au kila Mwezi kulipia gharama za kuishi kwenye hiyo nyumba zaidi wanaweza kupata kipato zaidi kama sehemu ya hiyo nyumba watapangisha)
7/Nyumba inaweza kuwaletea vitu vingine vingi kama Gari kama watafanya mahesabu vizuri(Kwa mfano wanaweza kuitumia kama dhamana katika taasisi za kipesa kukopa pesa za kununulia gari nk.)
NOTE;
Kwanini wasianze na Gari:
A/Gari inahitaji gharama kubwa sana kulihudumia(Kwa mfano Insurance, Kodi ya Mapato, Mafuta ya kila siku, Service ya kila mara, Parking ya kila siku, Trafiki, Vipuri nk)
B/Gari itakuzidishia gharama zaidi za maisha pasipo msingi.(Mfumo wako wa maisha unaweza ukabadilika ili kukidhi tu fahari ya kumiliki gari. eg.Kula, kuvaa, Makazi, matembezi, Marafiki, Ndugu, Jamaa nk.) Hili jambo nimeliona kwa watu wengi sana mijini. Kifupi Gari halipatani sana na mbana matumizi!!!
C/Thamani ya Gari mara nyingi inakwenda ikipungua tokea ile siku unalimiki.
D/Gari ni chombo kinachochakaa kwa upesi sana kadri siku zinavyokwenda au unavyolitumia(Mara nyingi magari mengi yanakuwa yameanza kuchakaa vibaya baada ya miaka mitatu tu!!)
E/Gari lina tabia ya kukugeuza kuwa Mtumwa wake(Kwa mfano Wakati wote litakuhitaji kutoa pesa zako mfukoni ili uweze kulitumia). Kifupi Gharama za Gari ziko juu zaidi wakati wa kulitumia kuliko hata wakati wa kulinunua!!