Kuna kunguni kwenye mabweni ya UDSM. Chuo kitafute suluhisho

boblyy sams

Member
Jul 1, 2015
26
32
Habari wanajamvi,,,
Hali ya usingizi katika chuo pendwa cha udsm sasa ni mbaya,,,,, kunguni wameondoa ladha yote ya usingizi imeisha,,, sio hostel za campus wala mabibo hali ni mbaya. Watu wanakesha vimbwetani waweza fikiri wanasoma kumbe watu wanakimbia kunguni vitandani kwao ,,, sasa hivi makundi sogozi ya whatsapp (whatsapp chat groups) yapo active sana usiku maana watu hawalali kwasababu ya kunguni..
Hatua stahiki zichukuliwe
 
Poleni japo post yako imekaa kishabiki Badala ya kiuhalisia
Sio kawaida hostel zote ziwe na kungunguni kwa wakati mmoja
Kwa nini usiseme tu hostel unayokaa au kitandani kwakwako kuna kunguni?
Nimeongea na rafiki yangu yupo moja ya hostel wala hajui hii habari
Pole lakini
 
Kwani mkiwa likizo uongozi wa chuo haufanyi fumigation?
 
Tatizo mnatokea maeneo mbalimbali wasaf na wachafu mnakutana pamoja.imizaneni kufanya usafi na mpulize madawa kama na magodoro yaan hao wadudu dawa ni kuchoma moto tu,hamna namna.polen
 
Nimeishi hostel za mabibo, nilikuwa nikisikia hizo habari za kunguni lakini sijawahi kuwaona/kuwakuta kwenye baadhi ya vyumba nilivyoishi!
Hao kunguni watakuwa baadhi ya vyumba tu na wengine hujificha kwenye yale magodoro wanayogawa!
 
Hahaha...umenikumbusha musoma tech 2010_2012 tulikuwa tuna share na kunguni gada(ugali)...thlvyonwambia headmaster kuleta dawa eti akasema kuwaua kunguni wote ilihitajika million mia7...
 
aibu

mkija field mnaonekana watanashat haswa nyie mnaosoma education kumbe mkrud chuon nimwendo wakutafunwa duh! hahahaaaaaaaaaaaaaa!

Team Bugene sec
 
Dah kwa kweli nililala pale mabibo siku moja nilihaha. Hata ukilala sakafuni wanakushukia aisee
 
Habari wanajamvi,,,
Hali ya usingizi katika chuo pendwa cha udsm sasa ni mbaya,,,,, kunguni wameondoa ladha yote ya usingizi imeisha,,, sio hostel za campus wala mabibo hali ni mbaya. Watu wanakesha vimbwetani waweza fikiri wanasoma kumbe watu wanakimbia kunguni vitandani kwao ,,, sasa hivi makundi sogozi ya whatsapp (whatsapp chat groups) yapo active sana usiku maana watu hawalali kwasababu ya kunguni..
Hatua stahiki zichukuliwe
Umekwenda Chuo kulala au kusoma....... Piga pindi utalala kwako
 
hata mimi yameshawai nikuta.. hao wadudu ukimbeba mmoja akadandia nguo yako... ukaingia nae chumban kwako... siku hiyo hiyo wanazaliana hata kama ni dume nae anazaa tu au jike ambaye mimba hana.. anazaa tu kwa fujo ili wakutese usiku

I once experienced these bugs kwa kweli hao kuwamaliza Labda maombi
 
Poleni japo post yako imekaa kishabiki Badala ya kiuhalisia
Sio kawaida hostel zote ziwe na kungunguni kwa wakati mmoja
Kwa nini usiseme tu hostel unayokaa au kitandani kwakwako kuna kunguni?
Nimeongea na rafiki yangu yupo moja ya hostel wala hajui hii habari
Pole lakini
Muulize vizuri rafiki yako, huenda anakuonea aibu kusema, nmewahi kuwa shuhuda katika hili
 
Back
Top Bottom