Kiwango cha dini kinatokana pia na kadri watu wanavyoweza kuwawajibisha watawala wao au kadri watawala wao wanavyoweza kuwajibika kwa raia. Ukiwa katika taifa ambalo una uhakika wa kula chakula kizuri, kusafiri kwenye miondombinu bora kwa haraka bila ajali, kupata haki zako bila connections na kupigia watu magoti utafikiria mambo ya mungu kwa uchache zaidi na ni rahisi zaidi kuwa Atheist au Agnostic kuliko taifa ambalo kupata chakula kizuri, miondombinu bora, huduma za afya, fursa za kiuchumi na haki ni vigumu sana.
Mfano hapa Tanzania watu wanaona kupata kazi nzuri ni muujiza wa kushukuru na kutoa sadaka kabisa kwa sababu ya fursa chache za ajira, ila ukienda Ulaya, Marekani, Australia, Canada, Uarabuni au China sio muujiza kupata kazi kwa sababu fursa za kazi ni nyingi sana hadi nyingine zinakosa watu wanahitaji wahamiaji kuzijaza.