Ufisadi wa EPA ulianzia BoT wakishirikiana na wafanyabiashara.Hakuna sehemu iliyomuhusisha afisa wa MoF.La Saada Mkuya na ESCROW akaunti ebu fanya jitihada kama GT ulete ushahidi kuliko kuishi kwa kudhani dhani.
Fika Zanzibar. Uliza alichofanya Karume Jr kipindi alipokuwa Rais.Huwa najiuliza, iweje upande wa bara tu, mara EPA,Richmond, escrow, ufisadi mwingi. Mbona Zanzibar haya mambo machafu hayasikiki?
Kwani Kikwete ndio muasisi wa ufisadi? mkuu MOSSAD II wewe jitoe tu ufahamu lakini mafisadi wanajulikana kwa nasaba zao mpaka imani zao.Fanya tafiti uje na majibu
Mingoi: Ukitetea kitu basi jaribu hata kuwa na utetezi unaoelekea ukweli japo utabaki uongo.
Kwanza Wizara mama ya BoT ni MoF, kwahiyo BoT na MoF wana uhusinao wa moja kwa moja.
FACT 1. Wakati wizi wa EPA unaotkea BoT MoF alikuwa Zakhia Meghji
FACT 2. Wakati suala la EPA linafika mara kwa bungeni, Zakhia Meghji aliktaa jambo hilo lisijadiliwe bungeni kwasababu eti pesa hizo za EPA zilitumika kwaajili ya usalama wa Taifa
FACT 3. Baadaye Waziri Meghji alikuja kukubali bungeni kuwa kwamba alidanganywa na governor BoT, kwamba pesa za EPA zilitumika kwaajili ya usalama wa Taifa
FACT 4. Baadaye Rais JK akamufukuza kazi Meghji wa uwaziri wa fedha kwaajili ya sakata la EPA.
SWALI. Kama hakuna afisa wa MoF aliyehusika direct or indirect kwanini Meghji alifurushwa kazi?
Ushahidi gani unaotaka wa wizi wa Escrow ndugu yangu? unayo macho lakini huoni, unayo masikio lakini husikii. I pray kwamba Marelani/Ulaya waendelee kukaza uzi tuone kama huyo Saada Mkuya wako atasamilika na pesa za Escrow?!
Mtu huonekani wewe ni GT kwa kuandika neno GT. Bali maandishi yako ndiyo yataonesha kuwa wewe kweli ni GT.
Ni kwa mandishi yako hapo juu sioni kwamba wewe ni GT!
Alhaj Aman Abeid Karume mtoto wa Sheikh Abeid Aman Karume amefanya ufisadi wa kutisha Zanzibar.
1. Amegoma kutumia Ikulu ya Zanzibar na aliamua nyumba yake binafsi itengenezwe kwa kodi ya wananchi ili nyumba hiyo iwe na hadhi sawa na Ikulu. Ile ni nyumba binafsi ambayo anaishi hadi sasa, ikakarabatiwa ika kali kuliko hata ikulu ya Zanzibar.
2. Amepora jengo lililokuwa linatumiwa na watoto yatima kwa madai kuwa jengo hilo lilikuwa mali binafsi ya babake wakati sio kweli
3. Amepora majumba kibao Zanzibar na kugeuza mali zake binafsi
Karume anayepora majumba ya serikali na Mkapa aliyejiuzia Mgodi waKiwira kwa Mil 70 tu tofauti yao iko wapi?
Zanzibar kuna ufisadi wa hali ya juu sema hautangazwi tu.
Hii post sijui imekaa kuitetea zanzibar, naona sielewi
Hakuna rasilimali za kukwapua Zanzibar.Hawana dhahabu,hawana gesi,hawana Tanzanite,hawana ardhi kubwa,hawana viwanda kifupi Zanzibar hakuna la maana zaidi ya kelele nyingi.
Tanganyika ilishakufa hata wewe umekuta hadithi tu lakini wanasiasa wanakutia ujinga.
Huwa najiuliza, iweje upande wa bara tu, mara EPA,Richmond, escrow, ufisadi mwingi. Mbona Zanzibar haya mambo machafu hayasikiki?
Hapa haitetewi Zanzibar bali ukweli unawekwa bayana.Huku bara tusipochukua hatua UFISADI unaweza kugeuka kuwa tunu ya taifa.