Kunani Zanzibar mbona habari za ufisadi na Malaria hazivumi, Tanganyika vipi?

lakini kiongozi wa nchi ni rais kikwete! au na yeye hana maadili ya dini?
CC: MJEPU, Mingoi

Mmh sidhan kama anamaadal angelikuwa ni rais anajimbua angekemea huu ufisad, alisema atataja orodha ya wauza unga hd leo, Rais haangalii matatizo ya Nchi yake kila cku kusafir nchi za nje, sasa hapo utasema kunaRais ktk nchi hii Rais dhaifu sn
 
Last edited by a moderator:
Ufisadi wa EPA ulianzia BoT wakishirikiana na wafanyabiashara.Hakuna sehemu iliyomuhusisha afisa wa MoF.La Saada Mkuya na ESCROW akaunti ebu fanya jitihada kama GT ulete ushahidi kuliko kuishi kwa kudhani dhani.

Mingoi: Ukitetea kitu basi jaribu hata kuwa na utetezi unaoelekea na ukweli japo utabaki uongo.

Kwanza Wizara mama ya BoT ni MoF, kwahiyo BoT na MoF wana uhusiano wa moja kwa moja.

FACT 1. Wakati wizi wa EPA unatokea BoT, MoF alikuwa Zakhia Meghji

FACT 2. Wakati suala la EPA linafika kwa mara kwanza bungeni, Zakhia Meghji alikataa jambo hilo lisijadiliwe bungeni kwasababu eti pesa hizo za EPA zilitumika kwaajili ya usalama wa Taifa

FACT 3. Baadaye Waziri Meghji alikuja kukubali bungeni kuwa alidanganywa na governor wa BoT, kwamba pesa za EPA zilitumika kwaajili ya usalama wa Taifa

FACT 4. Baadaye Rais JK akamfukuza kazi Meghji ya uwaziri wa fedha kwaajili ya sakata la EPA.

SWALI. Kama hakuna afisa wa MoF aliyehusika direct or indirect kwanini Meghji alifurushwa kazi?

Ushahidi gani unaotaka wa wizi wa Escrow ndugu yangu? unayo macho lakini huoni, unayo masikio lakini husikii. I pray kwamba Marekani/Ulaya waendelee kukaza uzi tuone kama huyo Saada Mkuya wako atasalimika na pesa za Escrow?!

Mtu huonekani wewe ni GT kwa kuandika neno GT. Bali maandishi yako ndiyo yataonesha kuwa wewe kweli ni GT.

Na kwa maandishi yako hapo juu sioni kwamba wewe ni GT!
 
Wazanzibari wanakula kimya kimya. Hawalipuanii kama huku. Wao ni mwendo wa kumezeana tu
 
Kwani Kikwete ndio muasisi wa ufisadi? mkuu MOSSAD II wewe jitoe tu ufahamu lakini mafisadi wanajulikana kwa nasaba zao mpaka imani zao.Fanya tafiti uje na majibu

Alhaj Aman Abeid Karume mtoto wa Sheikh Abeid Aman Karume amefanya ufisadi wa kutisha Zanzibar.
1. Amegoma kutumia Ikulu ya Zanzibar na aliamua nyumba yake binafsi itengenezwe kwa kodi ya wananchi ili nyumba hiyo iwe na hadhi sawa na Ikulu. Ile ni nyumba binafsi ambayo anaishi hadi sasa, ikakarabatiwa ika kali kuliko hata ikulu ya Zanzibar.

2. Amepora jengo lililokuwa linatumiwa na watoto yatima kwa madai kuwa jengo hilo lilikuwa mali binafsi ya babake wakati sio kweli

3. Amepora majumba kibao Zanzibar na kugeuza mali zake binafsi

Karume anayepora majumba ya serikali na Mkapa aliyejiuzia Mgodi waKiwira kwa Mil 70 tu tofauti yao iko wapi?
Zanzibar kuna ufisadi wa hali ya juu sema hautangazwi tu.
 
Last edited by a moderator:
Mingoi: Ukitetea kitu basi jaribu hata kuwa na utetezi unaoelekea ukweli japo utabaki uongo.

Kwanza Wizara mama ya BoT ni MoF, kwahiyo BoT na MoF wana uhusinao wa moja kwa moja.

FACT 1. Wakati wizi wa EPA unaotkea BoT MoF alikuwa Zakhia Meghji

FACT 2. Wakati suala la EPA linafika mara kwa bungeni, Zakhia Meghji aliktaa jambo hilo lisijadiliwe bungeni kwasababu eti pesa hizo za EPA zilitumika kwaajili ya usalama wa Taifa

FACT 3. Baadaye Waziri Meghji alikuja kukubali bungeni kuwa kwamba alidanganywa na governor BoT, kwamba pesa za EPA zilitumika kwaajili ya usalama wa Taifa

FACT 4. Baadaye Rais JK akamufukuza kazi Meghji wa uwaziri wa fedha kwaajili ya sakata la EPA.

SWALI. Kama hakuna afisa wa MoF aliyehusika direct or indirect kwanini Meghji alifurushwa kazi?

Ushahidi gani unaotaka wa wizi wa Escrow ndugu yangu? unayo macho lakini huoni, unayo masikio lakini husikii. I pray kwamba Marelani/Ulaya waendelee kukaza uzi tuone kama huyo Saada Mkuya wako atasamilika na pesa za Escrow?!

Mtu huonekani wewe ni GT kwa kuandika neno GT. Bali maandishi yako ndiyo yataonesha kuwa wewe kweli ni GT.

Ni kwa mandishi yako hapo juu sioni kwamba wewe ni GT!

Inaonekana hata ufahamu wa jinsi ya akaunti ya EPA ilivyo hauna.Unasikia tu ikitajwa tajwa.Lakini kaa ukijua wizi wa pesa za EPA ni mpango wa watumishi wa BoT na wafanyabiashara waliogushi nyaraka na kuchota pesa.Suala la kuwa MoF ni wizara mama halihusiani na malipo yeyote ya akaunti ya EPA au unataja kusema EPA ni mjukuu wa MoF? Kwa taarifa yako wizi wa EPA ulianza tangu mwishoni mwa miaka ya 80.Wahindi walikuwa wanachukua pesa na kuzizungushia kabla michongo haijawafikia wakina Maranda na Lukaza wakatia togwa mafuta ya taa.
Mwisho utakuja na dhana kuwa NMB nao walihusika kwa kuwa pesa zilihamishiwa kwao toka NBC.Kijana usiwe mvivu wa kufuatilia mambo na usipende siku zote kumezeshwa kauli za vijiweni na wanasiasa.
 
Alhaj Aman Abeid Karume mtoto wa Sheikh Abeid Aman Karume amefanya ufisadi wa kutisha Zanzibar.
1. Amegoma kutumia Ikulu ya Zanzibar na aliamua nyumba yake binafsi itengenezwe kwa kodi ya wananchi ili nyumba hiyo iwe na hadhi sawa na Ikulu. Ile ni nyumba binafsi ambayo anaishi hadi sasa, ikakarabatiwa ika kali kuliko hata ikulu ya Zanzibar.

2. Amepora jengo lililokuwa linatumiwa na watoto yatima kwa madai kuwa jengo hilo lilikuwa mali binafsi ya babake wakati sio kweli

3. Amepora majumba kibao Zanzibar na kugeuza mali zake binafsi

Karume anayepora majumba ya serikali na Mkapa aliyejiuzia Mgodi waKiwira kwa Mil 70 tu tofauti yao iko wapi?
Zanzibar kuna ufisadi wa hali ya juu sema hautangazwi tu.

Mkuu Mzito Kabwela hata Nyerere amekaa Msasani zaidi ya miaka 10 akiwa rais. Labda Karume aliamua kufuata mfano wa baba wa taifa kama ambavyo wanasiasa wengi wanasisitiza.
 
Last edited by a moderator:
Hakuna rasilimali za kukwapua Zanzibar.Hawana dhahabu,hawana gesi,hawana Tanzanite,hawana ardhi kubwa,hawana viwanda kifupi Zanzibar hakuna la maana zaidi ya kelele nyingi.
 
kwa kweli mleta mada umejitahidi kufikiria ila mi mchango wangu ni kuwa
hapa kwetu bara ndio pekee fisadi anatetewa sana na ndio napendwa na raia
_
_
_
_
 
Hakuna rasilimali za kukwapua Zanzibar.Hawana dhahabu,hawana gesi,hawana Tanzanite,hawana ardhi kubwa,hawana viwanda kifupi Zanzibar hakuna la maana zaidi ya kelele nyingi.

Mkuu Ngongo ufisadi si lazima dhahabu na gesi. Ebu angalia rushwa polisi,hospitali,manunuzi hewa ya vifaa vya maofisini,matumizi mabaya ya rasilimali za umma,watumishi wanatumia nafasi zao kupora haki, ardhi na mengineyo mengi.
 
Last edited by a moderator:
Tuipe Zanzibar sifa zake na tuige mazuri yake.
Leo Pemba ni "Malaria free" lakini huku kwetu wataalamu wanazalisha mbu (rejea mbu wa Muhimbili) ili maambukizi na vifo viongezeke ili pesa za wafadhili waendelee kuzila kupitia warsha,kongamano,semina na mikakati mingi inayopangwa mahotelini.
 
Tanganyika ilishakufa hata wewe umekuta hadithi tu lakini wanasiasa wanakutia ujinga.

Huyo jamaa Tanganyika anayoidai hata haijui na hajawahi hata kuiona. Ni kajazwa sponji kwenye ubongo na akina Mbowe tu.
 

Ufisadi upo sana Zanzibar sema wanakula na kupuliza tofauti na huku halafu mafungu menyewe cheche tu.

Kabla ya SUK,Maalim Seif alikuwa anadai ana ushahidi wa kutosha juu ya ufisadi wa familia ya Karume Jr kwamba wamejiuzia majengo ya serikali kwa bei chee then wameyauza kwa bei juu.

Cha ajabu baada ya kulambishwa mnuso,jamaa akakanusha mwenyewe eti KarumeJr ni mtoto wa mwanamapinduzi na ni mzalendo hawezi kufanya hizo makitu.

In short hakuna kina Kafulila huko wakuchimbua madudu lakini hata hilo jengo jipya la Baraza la wawakilishi watu walipiga pesa.
 
Huwa najiuliza, iweje upande wa bara tu, mara EPA,Richmond, escrow, ufisadi mwingi. Mbona Zanzibar haya mambo machafu hayasikiki?

Zanzibar hakuna mali za kufisidi na hata zinapotokea kwa vile nchi yenyewe ni ndogo, kila mtu anamuona mwenzie nini anafanya na hivyo ni rahisi kumshtukia. Wezi wapo Tanganyika, nchi ni kubwa na miradi ni mingi! Na inahijumiwa kikweli kweli ndiyo maana ccm hawakubali kuachia madaraka under whatever pretence!
 
Hapa haitetewi Zanzibar bali ukweli unawekwa bayana.Huku bara tusipochukua hatua UFISADI unaweza kugeuka kuwa tunu ya taifa.

huku zanzibar wanajikulia pesa nyingi tu lakini mfumo wa kutwaifishwa hakuna kutokana aliyejuu yuko juu
Amani aliondoka na pesa ikafika hatua serekali ya sheni ilipoingia ilikua hamna kitu, pia vile vile hela inayokuja zanzibar ni lazima ipite tanzani kutokana na mfumo wa serekali tulionao. Hakuna wa kusema kwa sababu ukiona kiongozi wa zanzibar amechukua 5% basi wa bara 55%, apo hamna wa kusema
 
Swali hili niliweke hapa ili tufahamu tatizo liko wapi. Ni kuhusu ufisadi. Ufisadi unaitesa sana Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na mara chache sana kusikia na pengine hali kama hiyo haitokei kwenye Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Kwa nini hali hii iko hivyo?

cc Pasco, FaizaFoxy, laki si pesa MSALANI Nyani Ngabu
 
Hili limeshajadiliwa mbona, wazanzibar wanaridhika ndio maana wanataka wajitoe kwenye kudhalilishwa Hakuna hata hela moja inayoenda kwenye majimbo zanzibar, zote wanakula wabunge lakini huwasikii kulalamika kwenye mitandao ya kijamii, unafikiri hawajui?

Laa hashaa wanajua ila wameridhika. Kutokana na kuridhika huku ndio wako tayari wawe na kipato kidogo lakini kiende kwenye shuhuli za maendeleo na sio kikubwa kinachoenda kwenye mikono.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom