Hii Tabia ya kutohudhuria Misiba inatokana na nini?

Sir John Roberts

JF-Expert Member
Mar 1, 2017
9,650
15,970
Naomba kuuliza hapa jirani yangu kama nyumba 10 kutoka kwangu kuna msiba tangu juzi majirani tunajumuika pamoja na wafiwa na ndugu wengine wa mbali ila chaa ajabu kuna jirani mmoja hapa ni pua na mdomo na kwenye msiba yani mageti yanatizamana lakini haonekani yani anapita tu juu juu .sana sana mkewe tunaona ndio yupo karibu.

Watu wengi tunajiuliza hapa huyu jamaa vipi hii tabia ya watu kuwa hawana time na msiba hivi mnaionaje jamani na tatizo linakua ni nini haswa.?

Karibuni kwa mitazamo yenu wana jukwaa.
 
Sio kwa msiba sasa mtaa mmoja
Kwahiyo kama mtu una ratiba nyingine ucancel ukashinde msibani? Kuna watu wana ratiba ngumu mno, kupata muda wao n ngumu sana ila kama jamaa msibani kaonekana hata kama sio mkaaji na mkewe yupo anashiriki sioni tatizo, ingekuwa mkewe nae haonekani kabisa hapo kidogo ningeona kuna shida. Ni mawazo yangu sio lazima yawe sahihi.
 
Nimeipenda hii post Nilionyesha post hii kwa familia yangu na wao pia wamependa post hii. tumenunua projekta na tukaonyesha post hii kwa mtaa mzima na pia wameipenda post hii. Maisha yetu yamebadilika kwa sababu ya post hii. Tunashukuru kwa post hii,asante sana kwa post hili..
 
Kuwepo kwa mkewe ni uwakilishi tosha.

Aliekufa amekufa, haimaanishi mtaa mzima uache shughuli zao sababu ya kifo cha mtu mmoja.

Kuna baadhi ya mazishi huchukua mpaka wiki, sasa ungetaka familia nzima ikae mazikoni kwa wiki nzima??
Kifo kipo na maisha yanapaswa yaendelee pia.

Halafu ni vyema kufuata kilichokupeleka na sio kuwa monitor wa msiba wa kuangalia mahudhurio ya nani amekuja na nani hajaja.
 
Naomba kuuliza hapa jirani yangu kama nyumba 10 kutoka kwangu kuna msiba tangu juzi majirani tunajumuika pamoja na wafiwa na ndugu wengine wa mbali...
Ahsante kwa kuwasilisha swala hili.

Kabla hatujaanza kuchangia , tufahamishe kama ujirani wenu upo katika kundi lipi?mpo kwenye makazi ambayo wote ni wapangaji?,au ni majirani mnaoishi katika nyumba mlizojenga wenyewe?

Nahisi jirani yako anamitazamo tofauti.
 
Back
Top Bottom