Kuna wanaume wanapitia mambo magumu na still wanavumilia!

Hiki ni kisa ambacho nilishuhudia mwenyewe miaka kadhaa iliyopita kwenye nchi Fulani!

Ipo hivi jamaa alioa single mother na alishakuwa na mtoto mkubwa pia,sasa katika maisha ya ndoa jamaa akabahatika kuzaa na yule mwanamke watoto wawili.

Sasa baada ya hapo wanandoa hao wakaanza kugombana Mara kwa Mara hadi ikatokea kila mmoja akaanza kulala chumba chake na kila mtu akaanza kujipikia chakula chake mwenyewe ndani ya nyumba moja.

Na ikafikia time kila mtu anatoka kivyake na kurudi kivyake no kuuliza maana walikuwa hawaongei.

Mara paap! Mkeo akapata ujauzito wa mwanaume mwingine na mimba ikakua na mtoto akazaliwa.

Kidume yupo tu anashuhudia mkewe kapata mtoto! Jamaa alipoanza kuleta fujo mkewe akampigia simu mtoto wake yule wa kwanza maana ni mkubwa akaja kumtuliza baba yake wa kambo kibabe na mtoto akaamua aishi hapo hapo ili kumlinda mama yake asipate madhara yoyote kutoka kwa baba wa kambo.

Mara paap!mimba ya pili na kidume akaanza kuja kabisa home kwa jamaa kutoa matumizi na mwenyewe mke akishuhudia bila chenga.

Kuna wanaume wanapitia changamoto kubwa sana kwa wanawake hadi uzi huu unaruka hewani jamaa bado yupo tu hajahama kwenda popote na mkewe ameshazalishwa watoto wawili mbele ya macho yake!!


Sent by Diaspora
Nikija kufikia hatua hii ya ujinga ulio komaa ntaomba nikatwe kichwa mbele ya umati maaana huu ni us**nge

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hao ndio wanaosingiziwa wamerogwa na wake/wanawake zao, kumbe hakuna lolote ni udhaifu wao wenyewe
 
Back
Top Bottom