Kuna walioamua kutetea Uvivu wao kwa kusingizia Freemasons!

Ni yale yale ya Popobawa kuonekana mbagala tena kwa mama muuza vitumbua (si kwa CEO wa TBL). Adui mkubwa wa maendeleo ni UJINGA. Angalia composition ya watu wanaoshadidia haya mambo yasiyokuwa na proof yoyote. SAWA freemasons, so what? ingekuwa wale wote wanaofanya mambo ya hovyo hovyo kama kuua albino, kuliibia taifa na mambo yaliyo ya hatari kwa ustawi wa jamii yetu wanayafanya hivyo ili kukidhi matakwa ya freemasons ingekuwa issue. Sawa neno freemason lipo na pengine wapo, kwa hiyo? Vijana chapeni kazi.
 
Kuna hili gazeti linaitwa TAZAMA, ni aibu tupu, wameshindwa kutafuta habari badala yake wameshupalia porojo za Freemason! Huu ni ujinga (ignorance) na aibu ya watanzania wote.
 
Ni kweli ndugu Majjid Freemason kwa sasa imeteka akili za watu hat kuhalalisha uvivu wetu,lakini huyu sir Andy Chande kwa nini asingiziwe yeye tu na sio wengine? au ina maana ni yeye pekee aliyelitumikia Taifa hili kwa mafanikio mpaka ahusishwe na hawa freemason.

Jingine kipindi chote cha kuhusishwa kwake sijawahi kusikia amekanusha sasa sijui Majjid kwa nini unamsemea. Binafsi najua uwepo wa freemason ingawa siamini kama ndio wanaomletea mtu mafanikio.Ila si vyema kumkanushia mtu ingali mwenyewe anaweza kukanusha.

Andy Chande kakiri mwenyewe kuwa ni kiongozi wa wajenzi huru tawi la afrika mashariki..soma kitabu"KNIGHT IN AFRICA"..journey from bukene
 
Kuwa member wa freemason sio kashfa,ni uhuru wa mtu na sidhani kama Chande linamkera la yeye kuitwa mmasonia,kuhusu uchapa kazi wake hilo halina ubishi. Cha msingi wabongo wajue kuwa sio kuwa freemason ndo shortcut ya kutajirika,huu ni upuuzi,hata akina Rockeffeler,Lee na wengineo wanaotajwa kuwa na wanajumuia hiyo ni wachapakazi hodari ndo maana wamefanikiwa
 
Kama amejitangaza mwenyewe shida iko wapi?kwa hiyo unataka kutueleza nini juu ya wajenzi huru?au na wewe ndo wale2 lakini hamtaki mjulikane?kaka hiyo ni imani kama mtu ameamua kujiunga huko shida iko wapi?unachokitetea sana ni kipi? mbona mwenyewe asilalamike na kushitaki lakini cha ajabu wewe ndo uumie?Ni kweli wanaabudu shetani na mkuu wao ni shetani,kusoma kitabu ndo nini?sisi mbona tumesoma vingi acha hiko cha huyo mkuu wa A. mashariki soma na vya wakuu wenzake kutoka nchi mbali2,Hiyo siri ipo kwetu tu nchi zilizoendelea hakuna siri juu ya wajenzi huru

Ni miongoni mwa wala Chips-Mayai huyu. akili imegota kwenye kiwango cha chini kinachomstahili mbongo wa elimu ya shigongo.
Majjid umenena vyema
 
Na Maggid Mjengwa,

TUNAWAPITISHA watu wetu kwenye njia yenye giza. Kwenye njia yenye matope. Kwanini?
Kwenye moja ya mashairi ya Marcelino Dos Santos wa Msumbiji anasema; " We Must Plant". Kwa maana ya tuna lazima ya kupanda. Dos Santos hazungumzii kupanda mbegu za mahindi au mtama, bali kupanda fikra za kimapinduzi kwa wanajamii. Fikra zitakazowasaidia kutoka katika hali iliyopo na kwenda kwenye hali nyingine iliyo bora zaidi.


Na Socrates, mwanafalsafa wa Uyunani ya kale alipata kuonekana akimulika kurunzi mchana wa jua kali. Inaandikwa, kuwa Socrates yule alizunguka sokoni na kurunzi (tochi) yenye kumulika. Watu walimwuliza, kulikoni? Socrates akawajibu; ”Kwenye nuru hii , kuna walio gizani.”


Kwa Socrates lilikuwa ni tendo la kifalsafa lenye kuelezea hali halisi. Hata katika dunia hii ya kisasa, bado tuna miongoni mwetu, walio gizani mchana wa jua kali. Angalia ya kwa ’ Babu’ wa Loliondo. Ndiyo, kuna wanaohitaji kumulikiwa mwanga.


Uvumi wa Freemasons unaosambaa sasa kwenye jamii ni dhana ya kufikirika kama ilivyokuwa kwa Babu wa Loliondo. Ya Babu wa Loliondo yalianza kwa uvumi wa magazetini na hatimaye kugeuka kuwa moja ya majanga ya kitaifa.


Leo Watanzania tunajua, kuwa pamoja na kutangazwa sana, Babu wa Loliondo hajamtibu hata mgonjwa mmoja. Badala yake, amechangia kwenye vifo na mateso ya wengi. Hakika, ni sisi Watanzania ndio tuliokuwa ' wagonjwa' wa kuendekeza abracadabra za Babu wa Loliondo.


Na uvumi huu wa sasa wa Freemasons ni abrakadabra nyingine tunayolishwa Watanzania. Ni habari za kupotosha jamii, ikiwamo jamii kuaminishwa kuwa wanachama wa jumuiya ya Freemasons ni watu matajiri na kuwa anayejiunga na Freemasons atapata utajiri wa haraka.


Kwamba Freemasons inahusishwa pia na nguvu za giza ikiwamo imani za kimashetani. Walioanzisha upotoshaji huu wanajua kuwa hiyo Freemasons ni jumuiya ya kimataifa kama ilivyo kwa Rottery na Lions Club ambazo uanachama wake haupo wazi kwa yeyote yule bila kupitia wanachama wenyewe. Lakini haimaanishi kuwa wanachama wa jumuiya hizo wanajipatia utajiri wa haraka kwa kushiriki ‘ abrakadabra’ .


Leo hii hapa Tanzania kuna vijana wanaoshinda vijiweni wakiwaza tu namna ya kujiunga na Freemasons badala ya kufanya kazi. Na Freemasons pia imekuwa njia ya baadhi ya wanajamii kutetea uvivu wao. Freemasons inatumika pia kuwaandama wenye kufanya kazi kwa bidii na kujipatia mafanikio. Maana, leo hata anayenunua pikipiki mpya ataitwa ‘ Freemason!’


Ni wakati sasa kwa Serikali kutoa tamko juu ya hili la uvumi wa Freemasons. Iweke wazi kuwa jambo hili linakuzwa na kuwa kuna upotoshaji unaofanywa kwa makusudi. Maana, uvumi huu ukiachwa uendelee unaweza kutuletea madhara makubwa huko twendako.


Tunajua, kuwa leo wamejitokeza matapeli wanaowahadaa wanajamii kuwa wao ni Freemasons na kuwa wanaweza kuwasaidia wengine kujiunga na mtandao huo. Wamejitokeza pia waganga wa kienyeji wenye kufanya utapeli kwa kutangaza kuwa wana uwezo wa ‘ kiganga’ wa kuwasaidia wateja wao kujiunga na Freemasons. Wapo wanajamii wanaopoteza fedha na mali zao kwa kutapeliwa juu ya hili la Freemasons. Ndiyo maana, kuwa ni wajibu wa Serikali kuingilia kati kuwanusuru watu wake.


Ndiyo, watu wetu wako kwenye giza. Kuna upumbavu unaendelea kwenye jamii. Ni wajibu wa Serikali yao kuwasaidia kwa kuwamulikia mwanga. Na kuna tofauti ya ujinga na upumbavu. Marehemu Mzee Jongo alipata kutamka;” Kusoma si kuufuta ujinga, bali ni kuupunguza”.


Kila mwanadamu ana ujinga wa jambo moja au mia moja. Kuwa na ujinga wa jambo si kosa, hata profesa anaweza asijue namna ya kuchochea kuni za kuchomea mhindi mbichi. Kijana wa darasa la saba anaweza kuwa hodari wa jambo hilo kumshinda profesa.


Lakini upumbavu ni ile hali ya mwanadamu kufanya jambo isivyotakiwa huku akiwa na uelewa wa namna ya kufanya inavyotakiwa. Huo ndio upumbavu. Na ndiyo maana binadamu kuitwa mpumbavu ni tusi. Kuitwa mjinga si tusi, kila mmoja ana ujinga wake. Kuwa na ujinga wa jambo fulani ni kutoelewa jambo hilo. Ni nani anayeelewa kila jambo?


Na mwanadamu unafanyaje unapoamka na kukuta dunia unayoishi ardhi yake imeanza kumegeka na kuchotwa na bahari? Kuna niliyemwuliza swali hilo. Naye akanijibu; ” Huo ndio utakuwa mwisho wa dunia!” Aliyenijibu alikuwa amechoka kufikiri. Nilidhani amgetamka, kuwa angeanza kujifunza kuogelea. Maana, kwa kuogelea majini angeweza kukutana na kisiwa, au nchi kavu.


Wanadamu tumejaliwa akili ili tuweze kufikiri. Na kufikiri ndiko njia mojawapo ya kuiteka kweli. Kufikiri kunahamisha milima na hata kuiweka kando kuruhusu mwanga upite. Inakuwaje basi mwanadamu anapoacha kufikiri? Haya ya ya kuendekeza abrakadabra za Freemasons ni kielelezo cha Watanzania, kama ilivyokuwa kwa Babu wa Loliondo, kuamua kuacha kufikiri. Ndiyo, kuna waliojifunika vilemba vya ujinga. Wako gizani, wanahitaji mwanga.


Kuna wakati Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, aliingilia kati na kusitisha abrakadabra ya DECI iliyokuwa ikiitafuna jamii. Pinda aliwanusuru wengi. Ni wakati sasa kwa Waziri Mkuu wetu Pinda kuingilia tena kati na kulitolea tamko hili la abrakadabra ya Freemasons. Kufanya hivyo atawanusuru wengi.

0788 111 765
http://mjengwablog.com
 
Haya yote ni matokeo ya jamii iliyokata tamaa, jamii ambayo haitaki kujishughulisha, mifumo mibovu inazidi kuchangia kwa kiasi kikubwa kuondoa matumaini kwa wananchi, matokeo yake ndio haya sasa,watu hawataki tena kushughulisha akili zao, watu wanataka utajiri wa haraka haraka hata bila ya kufanya kazi, vyombo vya habari pia vimesaidia sana kukuza hili suala na kulipotosha, hasa yale magazeti ya udaku, maana siku hizi hata ukicheka, basi unaweza kuambiwa unacheka "ki - freemasons", bado tuna safari ndefu sana, si ajabu kuona wapo walio gizani mchana wa jua kali
 
Vyombo vya habari hususani vya udaku ambavyo hukimbiliwa na watu wasio wachambuzi ndiyo kundi kuu haswa lililolengwa ilikuweka soko sawa na huku wakisahau social responsibility.

Kwa watu makini hawakujishulisha na babu wa loliondo na hata hili la freemasons kwao litapita ila janga kubwa ni kwa wale walio wengi ambao wamejengwa na mfumo dhaifu wa kiutawala wao kila tukio wapo mbele bila kujali ni nini haswa kilichomo.
 
Mwenyekiti leo umesema kweli.mimi nimeishi nje ya tz miaka kibao hili la freemasons nimekuja kulisikia kwa urefu ni hapa home tu tz,lakini wenzetu hawana muda huo kabisa wakuwaza vitu ambavyo havipo,kweli wavivu ndio sana wanashabikia huu upuuzi
 
Inanisikitisha sana vijana tunapotea mimi binafsi nina ushahidi rafiki yangu kaacha masomo chuo sababu hiz hiz za freemason etih! unafuu wa maisha! kweli tunahitajika kujielimisha na kuachana na upumbavu huu!
be appreciated
yaan mtu akifanikiwa kwa kuchapa kazi basi atazushiwa masonia huru.

Hata JF ni freemasonia.......reason ni kwa nini ipendwe namna hii wakati kuna site kibao.
 
Sielewi huyu jamaa anajaribu kuipotosha jamii kwa maslahi ya nani! Ni upuuzi kusema hiki hakipo wakati kipo na kinaonekana kwa macho. Inawezekana Mjengwa anafanya makusudi kujifanya hajui anachokijua huku nafsi yake ikimsuta. Naamini anafahamu vizuri ukweli kuhusu uwepo wa Freemasons kuliko hata hawa wanaovamia ovyo. Siamini kama Mjengwa hajui kuwa jumuiya ya freemasons imekuwa ikitoa misaada mbalimbali jamii hasa mashuleni, siamini kama hajui kuwa Freemasons walitoa mchango wao kwa waathirika wa MV Bukoba. Siamini kama hatambui kuwa rais mstaafu BWM amewahi kualikwa na kushiriki vikao vya freemasons. Leo jukumu letu lilikuwa ni kuwaelewesha watu wajue kuwa Freemasons hawagawi utajiri kama wanavyodhani, hawaabudu shetani nk
 

MWANDISHI Mtanzania, Profesa Euphrase Kezilahabi, anaandika juu ya bwana aliyefika kwenye ngoma asiyoijua. Akashtuka alipowaona wapiga ngoma, akauliza;
" Nyinyi ni nani?"
" Sisi ni wapiga ngoma", mmoja kati yao akamjibu.
" Kwa nini mpo mahali ambapo hamtegemewi kuwa?"
" Hapa ni wapi?" Wapiga ngoma walimwuliza bwana yule. Naye akajibu;
" Kama ningejua nisingekuwa hapa kuonyesha siri ya ufundi wangu! Na hiyo ngoma yenu inaitwaje?"
" Tutajua Manju Mkuu atakaposimama katika kitovu cha duara", mmoja wao alijibu.
" Hivi sasa tunajifunza wimbo wetu wa kwanza."
" Na wachezaji wako wapi?", aliuliza bwana yule.
" Yeyote yule anayeweza kufikiri". Mwingine alijibu: "Lakini wale wachezao vizuri ni wale wanaovuka mpaka huo na kuingia katika ulimwengu huru. Hao hatunao wengi. Tulio nao wengi ni wanafiki wanaojidai kujua. Wanatufaa, maana tunawatumia kama wachekeshaji". (Rejea Prof. Euphrase Kezilahabi, Nagona, uk.39)

Naam, maandiko hayo ya Profesa Kezilahabi yamenivutia kuendelezea makala haya niliyoanza nayo juma la jana. Maana, ni maandiko yenye kutuma ujumbe wenye maana kubwa kwetu.
Baadhi ya wasomaji wangu wamenitaka nifafanue zaidi kuhusu hili la Freemasons, na kuna waliotaka kujua maana ya neno ‘abrakadabra'.

Hakika, kama anavyoandika Profesa Kezilahabi, nawaona Watanzania wengi leo tunacheza ngoma tusioijua. Na baadhi yetu; hususan wanahabari, wanacheza vibaya zaidi, maana, hawajavuka mpaka na kuingia katika ulimwengu huru.

Ndio hawa, kila kukicha, wanaeneza uzushi na uvumi wa hili na lile. Jamii bado ina imani na wanahabari, hivyo, haraka sana wanahabari huchangia kuipotosha jamii.

Hili la Freemasons ni moja ya upotoshaji huo. Sasa limefanywa kuwa ni 'abrakadabra'. Mwandishi yeyote makini, akikaa chini na kusoma vitabuni na hata mtandaoni juu ya habari za Freemasons, basi, hawezi kuja na simulizi za ajabu ajabu juu ya Freemasons kama tunazozishuhudia sasa katika jamii yetu.

Kimsingi, Freemasons tunayoisoma vitabuni imekuwepo tangu karne ya 14. Ni jumuiya ambayo wanachama wake wapya huingia kwa kutambulishwa na wanachama waliopo. Iko katika nchi nyingi duniani. Imejengeka katika misingi ya imani ya Kikristo, na inatokana na kundi la wajenzi katika jamii wa tangu karne ya 14.

Tunasoma, kuwa enzi hizo, wajenzi hao wa majengo hawakutaka kumilikiwa na wenye kujenga majengo yao. Walikuwa wakijenga, na wakimaliza wanakwenda kujenga mahali pengine walipotaka. Na waliweza pia kukatisha kujenga kama hawakupatana na mwenye jengo. Ndio asili ya kuitwa Freemasons ambayo ina tafsiri ya Wajenzi Huru

Na enzi hizo kando ya sehemu ya ujenzi lilijengwa banda la wajenzi. Ikawa kama karakana yao. Banda hilo lilijulikana kama lodge. Ni neno ambalo linatumika hadi hii leo ikiwa na maana ya sehemu ya wageni kukaa kwa malipo.

Freemasons, kama jumuiya, imekua na hata ikawa si ya Wajenzi Huru tu; bali jumuiya yenye taratibu zake ambazo imewaingiza hata wasio wajenzi, bali watu wa kada nyingine walioingia humo. Ni pamoja na wafanyabishara.

Hivyo basi, Freemasons haikuanza leo, na taarifa zake ziko vitabuni na hata mitandaoni. Bahati mbaya kwa nchi yetu abrakadabra imeingizwa katika simulizi ya hao Freemasons kiasi cha jamii kuaminishwa kuwa ni kitu cha ajabu sana. Kwamba ni imani ya kishetani na inahusishwa na utajiri wa haraka.

Na sisi Watanzania ni watu wa ajabu pia. Tujiulize; hivi kama hiyo Freemasons ingekuwa ni mahali pa kuingia na kujipatia utajiri wa haraka, si tungeona watu wa dunia hii wakipanga foleni ndefu kujiunga na mtandao huo? Kwani katika dunia hii masikini wako Tanzania tu?

Tunasahau kuwa, katika dunia hii kuna masikini wengi na wenye elimu pia. Wakati masikini wenzetu wanavyopambana kwa kutumia elimu yao kujikomboa kutoka kwenye umasikini wao, sisi tumekalia kuimba na kucheza ‘ngoma tusiyoijua'. Kila kukicha Freemasons, Freemasons!


Na wengine tungeamua kuwa watu wa hovyo hovyo tungejipatia fedha za bure tu. Maana, kwa kuandika habari za Freemasons juma la jana , basi, nimepokea simu nyingi za watu wenye kutaka kujiunga na mtandao huo kupitia kwangu!


Kwamba wako tayari kunitumia malipo ya uanachama! Niliwajibu kuwa mimi si mwanachama wa Freemasons, na kwamba nimeandika tu, na nikawaambia kuwa wanavyozidi kunipigia simu wanazidisha umasikini wao, maana wanatumia fedha zao.
Naam, Bwana Yesu alipotembelea Mto Galilaya, aliwakuta wavuvi wakivua samaki, miongoni mwao alikuwa Simoni. Yesu akasema:"Simoni, acha kuvua samaki, enenda ukavue watu."
Hakika, na watu wetu wamezama kwenye mambo ya abrakadabra. Wanahitaji maarifa ya kuwatoa hapo walipo. Wanahitaji elimu pia. Maana, mengi ya tunayoyashuhudia sasa ni abrakadabra.


Neno abrakadabra humaanisha kuwa ni mambo ya hila na ghilba. Ni neno la ‘kimazingaombwe'. Maana, dunia hii mazingaombwe yapo, ni sanaa. Anayekutamkia abrakadabra au ndumba nangae hana cha maana alichokutamkia bali anaichota akili yako kimazingaombwe. Anakudanganya.
Na wanaodanganywa ni Watanzania waliojifunika au kufunikwa vilemba vya ujinga! Na wanaojitokeza sasa ni ‘manabii wa siku za mwisho'. Wanatujenga hofu. Nao wanatajirika kwa hofu na ujinga wetu.
"Simoni, acha kuvua samaki, enenda ukavue watu."


Ndio, samaki wako huru majini, lakini kuna wanadamu wengi walio bado kwenye utumwa wa fikra. Bado wanaogelea kwenye povu la ujinga. Wako gizani kwenye nuru inayoangaza mchana. Wanahitaji kuvuliwa kutoka dimbwi la ujinga.


Mwanafalsafa, John Rawls, anasema: "Hata kama utakalo ni haki yako ya asili, lakini kama hilo utakalo halina faida kwa walio wengi, basi, si haki yako kulifanya. Hakika, wale wenye kusambaza uvumi na uzushi wa hili na lile katika jamii wanapaswa kukemewa na hata kulaaniwa.


Maan; hata kama ni haki yao kujitafutia riziki, lakini kwa vile kusambaza uzushi na uvumi ni mambo yasiyo na faida kwa walio wengi, basi, si haki yao kuyafanya hayo. Hivyo basi, tuangalie hata taratibu za kisheria za kuwashughulikia watu hawa. Mjadala huu utaendelea.

Maggid Mjengwa,
Mjengwa Blog::Habari,Picha,Matangazo

 

Similar Discussions

Back
Top Bottom