Kichekesho cha karne: Ibada ya kumuingiza Mr. Nice kwenye U Freemason

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,634
697,845
Vyuma vikikaza sana watu huerevuka zaidi na kutafuta kila namna ya kutoka kimaisha ama la walau watoto waende chooni
Kuna werevu m'baya usio na baraka za mamlaka, huu huitwa utapeli nknk na kuna werevu m'baya lakini wenye baraka za mamlaka, huu nao ni utapeli kama utapeli mwingine tuu lakini umepakwa rangi za kuvutia sana.. Mfano wake ni haya makanisa ya mitume na manabii
Kuna walalahoi wamejionea namna mitume na manabii wanavyotajirika kupitia waumini wajinga sana.. Sasa nao wameamua kuja kivingine

Kuna dini iliyopewa jina la mpinga Kristo (Freemason/ wajenzi huru).. Kwa ujinga uleule wa waumini wa mitune na manabii huku nako kuna upotoshaji mkubwa sana kuhusu hii imani ya The Masons/ Freemason!

Mwanzoni walikuwa wanabandika matangazo yao mitaani na kujitangaza mitandaoni .. Lakini sasa wamepanda Viwango.. Wanaonesha na ibada zao kwa kuwatumia watu waliowahi kuwa maarufu na baadae kufilisika kabisa ili kuwavuta majinga wengine

Hapa kwenye ibada wanaonekana watu wawili
Kasisi wa Freemason na muumini mpya (Lucas Mkenda) aka Mr. Nice
Hawa wako mbele ya sanamu la kishetani (satanism statue) na kasisi anaigiza kumuingiza Mr nice kwenye hiyo imani mpya

Kichekesho cha karne
.Freemason ibada zao hutawaliwa na usiri mkubwa na hawarekodiwi.. Na ukitokea wakirekodiwa ni kwa matumizi yao binafsi hawawezi kamwe kurusha mitandaoni
.Freemason hawavai kichovu kana hawa waigizaji hapa.. Kasisi kavua viatu hana socks Muumini naye kavua viatu ila yeye kavaa socks
Mimbari ya Freemason ni kubwa na ya gharama kubwa na nadhifu sana.. Wanaoisogelea hawavui viatu
. Ibada zao sio za watu wawili na za dakika tano, huwa ni ibada maalum yenye watu maalum waliovalia suti kali nadhifu na za gharama
. kuna vitambaa maalum vyenye nembo yao huvaliwa kuzunguka kiunoni

Wana formalities nyingi zilizopangiliwa vizuri na kwa utaratibu maalum na wa kipekee mno

Hiki kituko cha Mr Nice na huyo tapeli wake juha kilichorekodiwa kwa simu na kurushwa tiktok huku kukiwa na nambari za simu ni udhalilishaji mkubwa wa imani zinazoheshimiwa na za kaliba za juu mno
Kama ugumu wa maisha ndio umemfanya Mr. Nice ashiriki huu upuuzi ina maana anaweza kufanyishwa kitu kingine kibaya zaidi na cha aibu kubwa mradi tu apate chochote!

Ni lazima atambue wakati ni ukuta huwezi kushindana nao! Aliinuliwa akaishi maisha yake bila haya maujinga yake! Ana nafasi ya kusimama tena kama kipaji chake kilikuwa halisi lakini sio kwa kutumia shortcuts kama hizi..!
Na kama alitaka kutengeneza kiki aliyemshauri kamuingiza cha jiji
 
Na kama alitaka kutengeneza kiki aliyemshauri kamuingiza cha jiji View attachment 2906476
"Kama ugumu wa maisha ndio umemfanya Mr. Nice ashiriki huu upuuzi ina maana anaweza kufanyishwa kitu kingine kibaya zaidi na cha aibu kubwa mradi tu apate chochote!"

Ubinadamu ni kazi/Humanity is a work.
 
Ahahah...ujue wengi mnaruka stage kukimbilia kwenye umasikini lakin kiuhalisia ujinga ndio mbaya. Umasikini ni matokeo tu .
Kwahiyo unataka kusema
Umasikini ni matokeo ya UJINGA

yaan UJUAJI + UJINGA = UMASIKINI

Je ni kweli bora ukose MARI upate AKILI
Yaan utumie AKILI upate MARI kuliko upewe MARI halafu ukose AKILI kama LUCAS MKENDA
 
Back
Top Bottom