Kuna walioamua kutetea Uvivu wao kwa kusingizia Freemasons! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuna walioamua kutetea Uvivu wao kwa kusingizia Freemasons!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by maggid, Jun 15, 2012.

 1. m

  maggid Verified User

  #1
  Jun 15, 2012
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Ndugu zangu.,

  Ndio, kuna walioamua kutetea uvivu wao kwa kusingizia Freemasons.

  Nimepata kusoma kitabu cha Sir Andy Chande kiitwacho ' Knight In Africa'. Huko nyuma nilimsikia tu mtu anayeitwa Andy Chande, lakini, kupitia kitabu chake nikamfahamu zaidi alikotokea.

  Kupitia simulizi ya maisha yake unaona jinsi alivyo mchapakazi. Anatoa mifano mingi ya kazi alizofanya; kwenye biashara na hata utumishi wa taifa hili.

  Na jioni moja nilipomwona pale kwenye reception nyumbani kwa Balozi wa Sweden nikashawishika kuongea naye. Ucheshi niliouona kwenye maandiko yake upo pia kwa Andy unapozungumza naye. Kitabu chake kinasimulia pia historia ya nchi yetu. Kinatusaidia kuelewa tulikotoka, tulipo sasa na kuweza kufikiri juu ya wapi tuendako.

  Andy alikuwa pia rafiki wa Julius Nyerere tangu enzi za kudai uhuru wa nchi hii. Andy aliwahi kumkatalia Julius alipoombwa akagombee Ubunge Tabora kwenye uchaguzi wa kura tatu. Akatamaka; " I would save better as a business man rather than a politician".

  Famlia yake, kuanzia babu yake ni ya wafanyabiashara. Pale Bukene, Shinyanga, walianza na biashara ya kuuza magunia. Wakafanya pia biashara ya vinu vya kusaga na kukoboa. Baadae Andy na familia yake wakahamia Dar. Mbele ya Stesheni Kuu ya Tazara iliko sasa kampuni ya Azam ndipo kilipokuwa kiunga cha akina Chande. Walianza kwa kufyeka mapori. Hapo wakaweka vinu vya kukoboa na kusaga.

  Asubuhi moja enzi za Azimio la Arusha, mwaka 1967, Andy anasimulia kwenye kitabu chake, kuwa aliamka asubuhi moja kwenda kiwandani kwao. Yeye alikuwa meneja wa kiwanda hicho. Getini akawakuta askari wa FFU. Akaambiwa kuwa kuanzia siku hiyo kiwanda kimetaifishwa. Kikaitwa National Milling Cooperation. Aakaingizwa ofisini kwake akabidhi ofisi kwa Meneja mpya ambaye hakuwahi hata kukutana naye mitaani.

  Alipomaliza kufanya shughuli ya kukabidhi, Andy akumuuliza Meneja Mpya kama angependa aongozane naye akamtambulishe kwa wafanyakazi wengine. Andy akaambiwa imetosha, aende zake tu.

  Siku hiyo hiyo Andy akaitwa na rafiki yake Julius aende Ikulu. Hata alipoingia Ikulu, Andy alimwona Julius mwingine. Hakuwa mcheshi kama ilivyokuwa kawaida yake. Julius akamwambia Andy akae kitako na hapo hapo akamfahamisha maamuzi ya kutaifisha kiwanda chao na kuwa Shirika la Umma.

  Na cha ajabu, Julius akamwomba Andy awe Mwenyekiti wa Kwanza wa Bodi ya National Milling Cooperation!

  Andy akakubali! Na akaifanya kazi ile kwa nguvu zake zote.

  Inasikitisha kuona leo Andy anaanikwa kwenye magazeti ya udaku na kutolewa taswira hasi. Tena ni Andy huyu huyu ambaye aliwahi kuwa mmoja wa wajunbe wa Tume iliyokuwa ikipitia filamu zote zinazoingizwa Tanzania kuziangalia kabla umma haujaonyeshwa. Lengo lilikuwa kuhakikisha kuwa filamu hizo za kigeni haziathiri maadili, mila na utamaduni wetu.

  Leo Andy amekuwa mhanga wa baadhi ya vyombo vya habari vinavyokiuka maadili, mila na utamaduni wetu, kwa kumuanika hadharani, tena kwa kuweka picha zake, bila ridhaa yake, kuwa ni mwanachama wa jumuiya ya Freemasons, jumuiya ambayo, kwa kupotosha umma, media inadai wanachama wake wanaamudu mashetani!

  Naam, kuna waliamua kutetea uvivu wao kwa kusingizia Freemasons! Na hilo ni Neno La Leo.

  Maggid Mjengwa,
  Dar es Salaam
   
 2. M

  Marytina JF-Expert Member

  #2
  Jun 15, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,035
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  be appreciated
  yaan mtu akifanikiwa kwa kuchapa kazi basi atazushiwa masonia huru.

  Hata JF ni freemasonia.......reason ni kwa nini ipendwe namna hii wakati kuna site kibao.
   
 3. M

  MIGNON JF-Expert Member

  #3
  Jun 15, 2012
  Joined: Nov 23, 2009
  Messages: 2,587
  Likes Received: 1,563
  Trophy Points: 280
  Maggid napenda unavyoandika na unajitahidi kuelimisha kutumia kalamu yako, si leo wa la jana lakini umekuwa huchoki.
  Taifa linaangamia na haya ya karibuni yanafanya wenye kuwaza wakose usingizi. Loliondo halijapoa tayari kuna hili la dini ya kupata utajiri wa haraka, upuuzi mkubwa mno.

  Kanumba kwa umri na mafanikio aliyopata ni kuwa alikuwa anajituma na kufanya kazi kwa bidii,no doubt about that!

  Leo watanzania wanataka urahisi na wanafuata upuuzi wowote, naogopa imani ya dini yangu lakini kwa wajinga hawa ukianzisha bahati nasibu (makampuni ya simu na promosheni zao) unapata pesa, watu wanaamini ya kuwa unaweza ukawa tajiri kwa sekunde.
  DECI wamekumba za kutosha,watu walionywa na hawakusikia leo wanaugulia maumivu.

  Nimependa sana maelezo yako lakini watakusikia? Ama kweli wajinga hawamaliziki duniani!!!!!!!!!!!
   
 4. gollocko

  gollocko JF-Expert Member

  #4
  Jun 15, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 2,830
  Likes Received: 1,543
  Trophy Points: 280
  Ni kweli ndugu Majjid Freemason kwa sasa imeteka akili za watu hat kuhalalisha uvivu wetu,lakini huyu sir Andy Chande kwa nini asingiziwe yeye tu na sio wengine? au ina maana ni yeye pekee aliyelitumikia Taifa hili kwa mafanikio mpaka ahusishwe na hawa freemason.

  Jingine kipindi chote cha kuhusishwa kwake sijawahi kusikia amekanusha sasa sijui Majjid kwa nini unamsemea. Binafsi najua uwepo wa freemason ingawa siamini kama ndio wanaomletea mtu mafanikio.Ila si vyema kumkanushia mtu ingali mwenyewe anaweza kukanusha.
   
 5. MESTOD

  MESTOD JF-Expert Member

  #5
  Jun 15, 2012
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 4,641
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 160
  Matokeo ya mpumbavu ni majungu. Hata kama ukiwa freemason, bila kujibidiisha lazima utakuwa masikini tu! Hata hivyo, kwa wengi wetu masonic belief haijaeleweka ni kitu gani. Ni kuwa sijui ni kwa makusudi au bahati mbaya tumeanza kuambiwa negatives za masonic belief, hasa iki link na matukio mabaya ya vifo nk ya watu mashuhuri.

  Lakini kama ni kweli, ni wapi ibada za masonic (kama zipo) zinaweza kuelezwa na ziwe publicly open watu wakiri wenyewe?
  Vinginevyo kutetea masonry ni kujipambanua kwenye jamii kwamba wewe ni mwana freemasony ni kujitafutia maadui.
   
 6. s

  sanga malua JF-Expert Member

  #6
  Jun 15, 2012
  Joined: Dec 17, 2011
  Messages: 228
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  HIYO NDIO BONGO BWANA! Watu wanataka utajiri bila kufanya kazi kwa bidii juhudi na maarifa.wengine wanataka wagawiwe wasicho zalisha wapi na wapi.
   
 7. t

  tabu kuishi JF-Expert Member

  #7
  Jun 15, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 354
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Kama amejitangaza mwenyewe shida iko wapi?kwa hiyo unataka kutueleza nini juu ya wajenzi huru?au na wewe ndo wale2 lakini hamtaki mjulikane?kaka hiyo ni imani kama mtu ameamua kujiunga huko shida iko wapi?unachokitetea sana ni kipi? mbona mwenyewe asilalamike na kushitaki lakini cha ajabu wewe ndo uumie?Ni kweli wanaabudu shetani na mkuu wao ni shetani,kusoma kitabu ndo nini?sisi mbona tumesoma vingi acha hiko cha huyo mkuu wa A. mashariki soma na vya wakuu wenzake kutoka nchi mbali2,Hiyo siri ipo kwetu tu nchi zilizoendelea hakuna siri juu ya wajenzi huru
   
 8. Ungana

  Ungana JF-Expert Member

  #8
  Jun 15, 2012
  Joined: Jul 16, 2011
  Messages: 358
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sir Andy Chande anakubali kuwa yeye kweli ni mwanachama wa Freemasons,lakini shida ya waswahili ni kutaka kila mtu aishi wanavyoishi wao,ukiwa na simu mbili tu unaitwa fisadi,ukijenga unaitwa fisadi,ukimiliki gari unaitwa freemason,fuatilia thread hii hadi mwisho utakutana na watu wengi wenye akili za ovyo kiasi hicho!
   
 9. RR

  RR JF-Expert Member

  #9
  Jun 15, 2012
  Joined: Mar 17, 2007
  Messages: 6,719
  Likes Received: 206
  Trophy Points: 160
  Nakubaliana na wewe mwenyekiti maggid kwenye hoja watu kuwa wavivu, na kubaki kuwasingizia wale wachapa kazi ni waabudu shetani ama freemasons!
  Umepoteza mwelekeo pale unapokanusha kwamba Andy Chande sio freemason na pengine kusema freemason sio waabudu shetani.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 10. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #10
  Jun 15, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,798
  Likes Received: 36,825
  Trophy Points: 280
  siamini kama kuna iyo takatata mnayoita freemason. hii ni propaganda ya wazungu inayotumika kuwapotezea muda wajinga wazidi kuwa wajinga.
   
 11. M

  Mpanzi JF-Expert Member

  #11
  Jun 15, 2012
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 767
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45

  Akanushe nini? yeye ni Freemason, tatizo ni kwamba tunadanganywa kuhusu freemason, Fremason ni society kama ilivyo rotary, tofauti ni kwamba wao wana imani na system za Maisha, moja ya imani zao ni kwamba Mungu alipokuumba amekupa kila kitu na ni wajibu wako kutengeneza maisha, na hiyo ndio siri ya mafanikio ya wanajumuia wa Free mason, hawafanikiwi kwa kufanya kafara bali kwa kufanya kazi kwa bidii wakielewa kuwa wanawajibika kwa maisha yao.
  I hate magazeti ya udaku kwa kupandikiza uongo kwenye vichwa vya watanzania.
   
 12. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #12
  Jun 15, 2012
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,840
  Likes Received: 471
  Trophy Points: 180
  Freemason imekuwepo tangu enzi za kina nuhu, kama wewe unataka kuwaepuka uwe kama nuhu na mungu atakunusuru,Kumbuka wakati wa ujenzi wa mnara wa babeli ndiyo hao hao freemason, leo wanajinasibu eti wanajiandaa kutawala dunia kwa sera ya NEW WORLD ORDER, lakini hawataweza watakuwa kama wajenga mnara wa babeli mwisho wa siku ni lugha gongana.
  Acheni mungu aitwe mungu, freemason ni shetani kwa hiyo ukimuogopa shetani atakutawala na kukudanganya kuwa pesa na dhahabu ni zake kumbe ni uhuni mtupu.Ni siku za mwisho maandiko matakatifu yanasema watu watapenda mali kuliko utu, ndugu watauana na nchi moja itapiga nyingine, utasikia leo mungu wa kweli ni freemason hapo ujue kuwa mwisho umefika.Tulia hapo ulipo kama ni masikini baki masikini kwa kula jasho halali
   
 13. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #13
  Jun 15, 2012
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,840
  Likes Received: 471
  Trophy Points: 180
  Kawadanganye chekechea na mwanasesere
   
 14. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #14
  Jun 15, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,798
  Likes Received: 36,825
  Trophy Points: 280
  siamini kama kuna iyo takatata mnayoita freemason. hii ni propaganda ya wazungu inayotumika kuwapotezea muda wajinga wazidi kuwa wajinga.
   
 15. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #15
  Jun 15, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Kuna tatizo kubwa la uelewa wa watu kuhusu jumuiya ya freemasons. watu wanalazimisha kuihusisha na kazi za kishetani jambo ambalo si la kweli kabisa. hawa ni watu wa kawaida tu, tena wema wasiohusiana na ushetani wa aina yoyote. Sio dini, ni jumuiya tu au chama. Watu wenye akili na uwezo mkubwa wa kufikiri katika kujipatia kipato, hakuna mali wala utajiri unaotolewa na wanajumuiya hiyo bali ni uzushi wa watu wachache wenye uelewa finyu wa mambo.
   
 16. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #16
  Jun 15, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Hivi wewe ndugu unayeamini katika jadi na tamaduni za kikoloni,unayekumbatia utamaduni wa kigeni ulioletwa na wazungu na waarabu. Wewe uliyeamua kuasi imani ya mababu zako na kufuata vitabu vya watu, wewe ambaye unaimba nyimbo za kuusifu utukufu wa aliyeandikwa habari zake na mtu kama wewe, tena kwa kuhadithiwa. Hivi ni kipi kinachokuthibitishia kuwa dini unayoiamini ni ya kweli? hivi unaweza kututajia jina la babu yako mzaa babu? unadhani ni kwa nini hakubatizwa kama wewe?
   
 17. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #17
  Jun 15, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,325
  Likes Received: 1,792
  Trophy Points: 280
  Maggid,
  Malalamiko yetu mengi ya leo yanatokana na tabia yetu ya kuwa watu wavivu tusiopenda kujituma. Msingi mkuu wa shutuma za kidini na kubaguana ukiangalia sana ume base kule kule kwenye kupenda porojo na kuwa wavivu kupindukia. Kuchapa kazi kuna rewards zake na lazima tujifunze kutofautisha umuhimu wa kufanya kazi na hasara za kuunda taifa la wapiga soga. Kwa bahati mbaya watanzania wengi tumekuwa wapiga soga. Hakuna anayelazimishwa kuingia mfumo wowote wa kidini...ila tunachekesha kwa kupenda kusingizia udini na kunyoosheana vidole sababu tu ya kupenda kuwa wavivu.
   
 18. E

  EmeraldEme Senior Member

  #18
  Jun 15, 2012
  Joined: Mar 8, 2012
  Messages: 116
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Thanks Maggid kuelezea kuhusu freemassonry.
  Freemassonry ipo, ni jamii kama rotary as aforesaid by 1 member, lakini ni secret society ambayo members wake ni watu potentials na sio wavivu. Members wake ni ile cream ya watu and not otherwise. Mtu ambaye akisimama kwenye public lazima akubalike na auzike.
  Ibada zao ni usiku na sio mida ya kawaida, ukiwa massonic lazima uwe na mahali pengine pa kuabudu being it kanisani au msikitini. Na ni mojawapo kati ya sababu za kusemwa kuwa ni waabudu mashetani.
  Massons ukiwasoma wameshika nyanja zote za muhimu ili matakwa yao yaweze kutekelezwa.
  Subject kuwa Andy Chande ni massonic au lah, ni subject of proof from him alone, hakuna haja ya kumtetea maana he can as well stand on his own and say that he is not one of them kwenye media hiyo hiyo.
  Hata hivyo, habari zinasema kuwa Andy Chande ni one of them na the below link inaelezea kuwa Sir Andy Chande ali attain Grand master of service kwa massons, hebu isome halafu utuambie. https://www.google.com/#hl=ja&output=search&sclient=psy-ab&q=Andy+Chande&oq=Andy+Chande&aq=f&aqi=g-L3g-mL1&aql=&gs_l=hp.3..0i19l3j0i5i19.490.8177.0.8560.22.21.1.0.0.5.290.4795.2-19.20.0...0.0.ntr7yGwThZE&pbx=1&bav=on.2,or.r_gc.r_pw.r_qf.,cf.osb&fp=dfce8816fba7ba06&biw=800&bih=461

   
 19. palalisote

  palalisote JF-Expert Member

  #19
  Jun 15, 2012
  Joined: Aug 4, 2010
  Messages: 8,352
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 0
  OXFORD ENGLISH DICTIONARY

  Freemason
  1. A member of a certain class of skilled workers in stone, in the 14th and following centuries often mentioned in contradistinction to ‘rough masons', ‘ligiers', etc. They travelled from place to place, finding employment wherever important buildings were being erected, and had a system of secret signs and passwords by which a craftsman who had been admitted on giving evidence of competent skill could be recognized. In later use (16-18th c.) the term seems often to be used merely as a more complimentary synonym of ‘mason', implying that the workman so designated belonged to a superior grade. Obs.

  1376 in Conder Hole Craft 51 [A list of the city companies with the number of their representatives on the Council has: Free masons 2, Masons 4. But in the original handwriting the figure for the Masons is altered to 6, and the entry Free masons is expunged]. 1396 Charter Rich. II (Sloane 4595) in Masonic Mag. (1882) 341 Concessimus..archiepiscopo Cantuar. quod..viginti et quatuor lathomos vocatos ffre Maceons et viginti et quatuor lathomos vocatos ligiers..capere..possit. [1444 Act 23 Hen. VI, c. 12 Les gagez ascun frank mason ou maister Carpenter nexcede pas par le jour iiijd. ovesqe mangier & boier..un rough mason & mesne Carpenter..iiid. par le jour.] 1477 NORTON Ord. Alch. Proem. in Ashm. (1652) 7 Free Masons and Tanners. 1484 Churchw. Acc. Wigtoft, Linc. (Nichols 1797) 80 Paide to Will'm Whelpdale fremason for makyng of the crosse in ye chirchrth. 1495 Act 11 Hen. VII, c. 22 §1 A Freemason maister Carpenter Rough mason Brickleyer [etc.]. 1504 Bury Wills (Camden) 104 To John Dealtry, fremason, xs. 1526 Pilgr. Perf. (W. de W. 1531) 142 The free mason setteth his prentyse first longe tyme to lerne to hewe stones.

  1548 Act 2 & 3 Edw. VI, c. 15 §3 No Person..shall..lett or disturbe any Fre mason, rough mason, carpenter, bricklayer. 1594 BLUNDEVIL Exerc. Cont. (ed. 7) A. iv, In free Masons craft, in Joyners craft. 1608 TOPSELL Serpents (1658) 650 Who seeth not that it were far better the master work-men, free masons, and carpenters, might be spared, then the true labouring husbandman? 1662 EVELYN Chalcogr. (1769) 90 Encountring the difficulties of the free~mason. 1720 Lond. Gaz. No. 5907/4 Anthony Ashley..Free Mason. 1723 Ibid. No. 6195/6 John Lane..Free-Mason.


  2. A member of the fraternity called more fully, Free and Accepted Masons. Early in the 17th c., the societies of freemasons (in sense 1) began to admit honorary members, not connected with the building trades, but supposed to be eminent for architectural or antiquarian learning. These were called accepted masons, though the term free masons was often loosely applied to them; and they were admitted to a knowledge of the secret signs, and instructed in the legendary history of the craft, which had already begun to be developed. The distinction of being an ‘accepted mason' became a fashionable object of ambition, and before the end of the 17th c. the object of the societies of freemasons seems to have been chiefly social and convivial. In 1717, under the guidance of the physicist J. T. Desaguliers, four of these societies or ‘lodges' in London united to form a ‘grand lodge' , with a new constitution and ritual, and a system of secret signs; the object of the society as reconstituted being mutual help and the promotion of brotherly feeling among its members. The London ‘grand lodge' became the parent of other ‘lodges' in Great Britain and abroad, and there are now powerful bodies of ‘freemasons', more or less recognizing each other, in most countries of the world.


  1646 ASHMOLE Mem. (1717) 15 Oct., [At] 4 Hor. 30 Minutes post merid., I was made a Free-Mason at Warrington in Lancashire, with Colonel Henry Mainwaring. 1686 PLOT Staffordsh. 316 Admitting Men into the Society of Free~masons, that in the moorelands of this County seems to be of greater request, than any where else. Ibid., A Fellow of the Society, whom they otherwise call an accepted mason. 1688 R. HOLME Armoury III. 393/2, I cannot but Honor..the Masons..the more as being a Member of that Society called Free-Masons. 1691 AUBREY Memorandums 18 May in Conder Hole Craft (1894) 4 This day is a great convention at St. Pauls church of the fraternity of the free [erased, and accepted written above] Masons; where Sir Christopher Wren is to be adopted a Brother.


  1709 STEELE Tatler No. 26 3 They have their Signs and Tokens like Free-Masons. 1723 (title) The Constitutions of the Free-masons..for the Use of the Lodges. 1753 Scots Mag. Sept. 425/1 The society of free and accepted masons caused a..triumphal arch..to be erected. 1816 ‘QUIZ' Grand Master VII. 174 ‘I'd turn a Turk, or MethodistChristian, Freemason, even Jew!'

  3. attrib. (of or pertaining to freemasons), as freemason knock, secret, work.
  1807-8 W. IRVING Salmag. (1824) 220, I distinguished his *free-mason knock at my door.

  ------------------------------------------------------------------

  1785 BURKE Sp. Nabob of Arcot 33 The true *free-mason secret of the profession of soucaring.

  ------------------------------------------------------------------

  a1490 BOTONER Itin. (Nasmith 1778) 268 De *fremason-work operata.

  ------------------------------------------------------------------


  Hence Freemasonic a., of or pertaining to freemasons; Freemasonism (Stand. Dict.) = FREEMASONRY.
  1831 Westm. Rev. XIV. 156 A free-masonic order who converse by signs, innuendos, and slang. 1859 THACKERAY Virgin. II. xxxviii. 317 That mysterious undefinable freemasonic signal, which passes between women, by which each knows that the other hates her. 1861 SALA Dutch Pict. vi. 85 There she is at her post, with a wonderful free~masonic understanding with the doctor.


  Copyright © Oxford University Press 2000

   
 20. Wa Ndima

  Wa Ndima JF-Expert Member

  #20
  Jun 15, 2012
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 1,512
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Freemasons doesnt exist, period
   
Loading...