Ndugu wana JF, leo jioni kabla Naibu Spika Job Ndungai hajahairisha shughuli za bunge hadi kesho asubuhi amesema wabunge kadhaa wamemwandikia vikaratasi wakimwuliza kuhusu vazi la wabunge wanapokuwa bungeni na akasema kuna wengine wanavaa kombati. Aliwasomea kanuni fulani kuhusu vazi linalovaliwa bungeni na akawaomba wabunge wote wasome hiyo kanuni na wapime wenyewe na wasisubiri kutolewa nje.
Maswali:
1. Wabunge hao wanaovaa kombati bungeni ni za jeshi gani?
2. Kama wanavaa kombati, ni leo tu wamezivaa au ni leo tu kuvaa kwao kumekiuka kanuni za bunge?
3. Huku siyo kwenda mbali na pengine nia yake si njema?