carter
JF-Expert Member
- Jan 23, 2009
- 3,664
- 4,273
kwani kanzu inastahili bungeni?
Kanzu ni kanisani na msikitini au kwenye matukio yanayoendana na shughuli za kanisani au msikitini....
jibu la swali lako mkuu waweza lipata hapo.
kwani kanzu inastahili bungeni?
I am trying to imagine kama baadhi ya wabunge wa CCM wataamua kuingia bungeni na mashati ya kijani na suruali nyeusi. I mean sare ya CCM! Sijui wataonekanaje? Naamini kitakuwa ni kituko. Similarly, nadhani si vibaya kwa CHADEMA nao kuamua kuvaa mavazi ambayo hayana identity ya vyama vyao japo bungeni wanawakilisha vyama vyao.
Unajua mle bungeni wanadhani watanzania ni kama enzi za miaka ya Nyerere ambako watu walikuw ahawafuatilii na kujua kanuni zinasemaje kuhusu kila jambo.
Job Ndugai anasema vile, Mheshimiwa Magobe umesema kanuni fulani. Mimi nakusaidia tuweke kanuni za Bunge zinasemaje halafu akina Ndugai na wenzake mle bungeni waje waone JF tunavyojikita kujadili kanuni na si mipasho kwa sababu ya kumshabikia au kumponda Ndugai.
Kanuni kuhusu mavazi bungeni ni Kanuni namba 146 inayosema hivi, na nimeikopi na kupaste tu.
**************
Ibara 146:
(1) Mbunge anayeingia kwenye Ukumbi wa Bunge atawajibika kuvaa mavazi ambayo ni safi na yenye kuhifadhi heshima yake, hadhi ya Bunge na utamaduni wa nchi, kama ilivyoainishwa katika Kanuni hii.
(2) Vazi Rasmi la Spika na Naibu Spika litakuwa ni joho lenye kuonesha rangi za Bendera ya Taifa, Nembo ya Taifa na baadhi ya mazao makuu nchini, lililoshonwa maalumu kwa ajili hiyo, ambalo litavaliwa juu ya vazi lolote ambalo ni vazi rasmi kwa Wabunge.
(3) Vazi rasmi kwa Wabunge litakuwa lolote kati ya yafuatayo:-
(a) Kwa Wabunge wanawake:-
(i) vazi lolote la heshima yaani ambalo si la kubana mwili, lisiloonesha maungo ambayo kwa mila na desturi za kitanzania hayapaswi kuoneshwa na ni refu kuvuka magotini;
(ii) gauni la kitenge au blauzi inayovaliwa na kitenge au sketi ya rangi yoyote;
(iii) kilemba cha kadri au mtandio;
(iv) suti ya kike; na
(v) vazi linalovaliwa wakati wa eda.
(b) Kwa Wabunge wanaume:-
(i) suti ya Kiafrika au safari ya mikono mirefu au mifupi yenye ukosi au shingo ya mviringo na yenye fulana au bila fulana ndani, ya rangi moja, isiyokuwa na nakshi, pamoja au bila baragashia;
(ii) vazi la kimwambao yaani kanzu rasmi na nadhifu, koti, baraghashia na makubadhi au viatu;
(iii) suti kamili ya kimagharibi ya rangi kadri isiyomeremeta;
(iv) koti aina ya blazer na tai, pamoja na suruali yoyote ya heshima; au
(v) tarbushi na kilemba cha Singasinga, au kilemba chochote kinachovaliwa kwa mujibu wa masharti ya imani au mila.
(4) Vazi Rasmi la Katibu na Wasaidizi wake Bungeni litakuwa kama ifuatavyo:-
(a) Kwa Makatibu wanaume:
(i) suti kamili ya kiafrika au safari, yenye ukosi au shingo ya mviringo na mikono mirefu au mifupi ya rangi nyeusi au bluu; au
(ii) suti kamili ya kimagharibi ya rangi nyeusi au bluu na shati jeupe na tai.
(b) Kwa Makatibu wanawake:
Suti ya rangi nyeusi au ya bluu na shati jeupe na tai.
(c) Makatibu na Wahudumu watavaa mavazi maalumu wakati wa shughuli maalumu za Bunge.
(5) Mpambe wa Bunge na Wasaidizi wake ndani ya Ukumbi wa Bunge watavaa mavazi rasmi ambayo yataamuliwa na Spika.
(6) Spika anaweza kwa sababu maalumu, kumruhusu mtu mwingine anayehusika na shughuli za Bunge kuvaa viatu ambavyo sio rasmi.
(7) Mbunge yeyote anaweza kutoa taarifa Bungeni iwapo Mbunge mwingine ataingia kwenye Ukumbi wa Bunge akiwa na mavazi yasiyoruhusiwa kwa mujibu wa Kanuni hii.
(8) Spika atakaporidhika kuwa Mbunge aliyetolewa taarifa kwa mujibu wa fasili ya (7) ya Kanuni hii hajavaa mavazi rasmi ataamuru Mbunge huyo atoke nje ya Ukumbi wa Bunge.
(9) Mbunge aliyetolewa nje kwa mujibu wa fasili ya (8) ya Kanuni hii hataingia ndani ya Ukumbi wa Bunge hadi pale atakapokuwa amevaa mavazi rasmi.
ungetoa hoja wasijadili mambo kwa itikadi za vyama badala yake wajali maslahi ya taifa hapo ungekuwa umeboresha zaidi..acha kuwaogopa magamba.Nadhani bungeni wanawakiiisha wananchi wa majimbo yao, sio chama. Kwani kwenye jimbo kuna watu wenye itikadi tofauti. This being said, naungana na wewe CHADEMA, CCM, CUF etc wasivae mavazi ambayo yana identity ya vyama vyao wanapokuwa Bungeni.
Ndugu wana JF, leo jioni kabla Naibu Spika Job Ndungai hajahairisha shughuli za bunge hadi kesho asubuhi amesema wabunge kadhaa wamemwandikia vikaratasi wakimwuliza kuhusu vazi la wabunge wanapokuwa bungeni na akasema kuna wengine wanavaa kombati. Aliwasomea kanuni fulani kuhusu vazi linalovaliwa bungeni na akawaomba wabunge wote wasome hiyo kanuni na wapime wenyewe na wasisubiri kutolewa nje.
Maswali:
1. Wabunge hao wanaovaa kombati bungeni ni za jeshi gani?
2. Kama wanavaa kombati, ni leo tu wamezivaa au ni leo tu kuvaa kwao kumekiuka kanuni za bunge?
3. Huku siyo kwenda mbali na pengine nia yake si njema?
we kweli chili nenda india ukaliwe hapa si fani yako.Tatizo hayo magwanda yao hawafui matokeo yake yananuka sana kiasi cha kuhatarisha usalama wa afya wa wabunge wengine bungeni
..muongozo wa spika..kuna waheshimiwa wamevaa kombati.. sasa hapo sijui hzo kombati ni za jeshi lipi...agh!!Hao wabunge waliomuandikia vijikaratasi walishindwa nini kusimama hapo bungeni hadharani kutoa dukuduku lao mpaka waandike vinote huko uchochoroni, mbona wakisimama kutukana hawaoni shida wala kujificha?