Raia Fulani
JF-Expert Member
- Mar 12, 2009
- 10,883
- 2,765
Yah, navidhania na sidhani kama ndio havijakuwepo. Vipo. Mfano;
1. Nimetokea tu kuwaza kwa nini watu wanakufa. Napata jibu kuwa hakuna kifo cha bahati mbaya. Unaweza pia kuepuka vifo. Vifo kwa maana majaribio ya uhai wako kukutoka sio mara moja. Pengine tungeoneshwa tungeshangaa.
2. Tunaishi maisha mengi sana. Wewe kuamka na kwenda uendako na kurudi ulipotoka, haitoshi kusema ni mfumo mmoja wa maisha. Nitajaribu kutengeneza filamu huko mbeleni kuonesha hili. Mfano, umeoa na mkazaa mtoto mmoja kisha ikatokea mizengwe mkaachana. Umetoka hapo ukaoa na kuendelea na maisha. Sasa picha inaanza pale ambapo ingekuwaje mngeendelea na mwanamke wa awali. Mifano ni mingi kwa kila nyanja
3. Nawaza kwamba sisi binadamu wapo ambao katika akili zao kuna milango fulani iko wazi, na hawa wanaona beyond. Kuna muda nakaa naona kabisa kuna kitu kama pazia kwenye ufahamu wangu linapaswa kusogezwa nione mbele zaidi kuna nini. Kuna kitu nawaza ila maelezo yake ni adimu sana.
4. Mwisho, nguvu za kiumbe zipo katika viungo/viungio vya mwili. Misuli inasaidia tu