Kuna vitu huwa vinakera sana na kushangaza kwa baadhi ya wafanyabiashara wanavyofanya biashara zao

Half american

JF-Expert Member
Sep 21, 2018
25,916
67,957
Habari wakuu,

Bila shaka umekuwa na siku njema na unatafakari namna mipango ya siku inavyokwenda. Pole sana kwa wenye changamoto ni sehemu ya maisha yetu ya kila siku. Bila kupoteza muda niende moja kwa moja kwenye mada.

Mteja ni mtu muhimu sana katika biashara yoyote, lengo la kuanzisha biashara ni kupata wateja watakaonunua bidhaa au huduma yako. Biashara yoyote isipopata wateja bora na wa uhakika, ni wazi kuwa haiwezi kufanikiwa. Ukishatengeneza wateja hivyo vingine kama hela na faida vitakuja kutoka kwa hao wateja.

Nguvu yoyote unayoweka kwenye biashara yako hakikisha ni kutengeneza wateja, yaweza kuwa wateja wapya na kuhakikisha wateja wanaendelea kununua kwako. Wateja ndio uhai wa biashara yoyote, hivyo kipaumbele cha kwanza kwenye biashara lazima kiwe kumridhisha mteja.

Kuna baadhi ya mambo yanashangaza sana yanayofanywa na wafanya biashara na kuacha maswali kwa mteja. hii ndio namna ya kumridhisha mteja? Kukuza biashara na kuteka soko? Haya ni baadhi ya mambo machache ambayo nimekutana nayo kwenye biashara za watu nikaishia kushangazwa nayo/kero:~
  1. Mfanya biashara anasusa/anakataa kukuhudumia kwa sababu amezoea kukuona ukipata huduma kwa jirani yake. Anakusindikiza na maneno uende kununua/kupata huduma ulipozoea kwenda mara kwa mara hapa usikanyage. Unabaki unajiuliza hivi huyu kweli anafanya biashara au anataka mazoea? hii ni kero wafanyabiashara wa hivi wabadilike.
  2. Unafika dukani mhudumu anachukua hela yako kwanza alafu anajizungusha zungusha na mambo yake mengine bila kukupa huduma. Mara ashike simu, aendlee kupanga vitu n.k. Hiki kitabia kinakera sana ni kupotezeana muda wengi wanachukua hela kwanza kabla ya huduma kwa sababu ya uaminifu lakini huu utaratibu kwa baadhi ya wahudumu umegeuka kero. Mda mwingine unachohitaji hana lakini anang,ang,ania hela. Kama una mambo mengi na huwezi kutoa huduma kwa wakati ni bora kutokupokea hela ya mteja ili iwe rahisi kwake kuokoa muda kwa kutafuta huduma kwingine. Jali muda wa mteja.
  3. Kuna wale ambao hawajawahi kuwa na chenchi tangu biashara ifunguliwe, wanapenda ukienda na hela itumike yote na kulazimisha mteja kuchukua vitu ambavyo havikuwa kwenye bajeti. Ukiacha baadae anakataa na kusema alishakurudishia, huu ni utapeli. Ahsante kwa huduma ya lipa kwa simu kidogo inapunguza hizi kero licha ya gharama.
  4. Kuna wale wataalamu wakukiuka makubaliano. Mnakubaliana kuwa ulipie bidhaa mfano nguo,viatu, ndala n.k ukamjaribishie uliemnunulia kama haitokuwa size yake basi utairudisha kubadilisha. Unaporudi kufanya hivyo anakataa na kudai hukununua kwake.
  5. Kupandisha bei kiholela holela hasa kwa bidhaa ambazo bei ipo wazi na kulazimisha mteja anunue wakati anaweza kuipata kwa bei stahiki kwa mwingine. Akigoma kabisa kununua unamporomoshea matusi kana kwamba hela ulimpa wewe. Biashara ni makubaliano, mmeshindwana bei muache mteja aende kwa amani sio kuanza kumtolea lugha chafu.
  6. Kuchelewesha bidhaa bila sababu zinazoeleweka. Hii ipo sana kwa wale wanaofanya wasambazaji wa bidhaa . Unamuagiza bidhaa na mda mwingine unalazimika kulipia kabisa(hapa wengi ndipo tunapokwazika inakuwa ngumu kuagiza kwingine kwa sababu umeshalipia). Unaagiza bidhaa unaambiwa itafika baada ya masaa kadhaa ndani ya siku ila inakuwa tofauti unaletewa baada ya siku 2 au zaidi, huu ni usumbufu tunakwama.
  7. Majibu ya hovyo, kuna muda tunawasingizia wachawi ila wachawi wa biashara zetu ni sisi wenyewe.
  8. Kuna wale mnaowaweka wenza wenu kwenye biashara(mke) alafu ukiona hata anazungumza jambo la kawaida na mteja unamkasirikia mteja kwa sababu ya wivu. Kuna ulazima gani wa kumuweka mkeo kama unajijua una wivu? wengine biashara ni bar na muuzaji ni mke alafu wateja wakilewa wakamchangamkia mkeo unaleta shida, si umfungulie kanisa?
Nadhani haya sikutani nayo peke yangu, unaweza kuendelea kwa kuorodhesha unayokutana nayo kwa wafanyabiashara ndani ya jamii yako.

NAWASILISHA.
 
Habari wakuu

Huduma Bora na nzuri kwa mteja Tz haijawahi kuwepo!
 
Mie KUNUNA tu yaan unaenda DUKANI unamkuta mtu KANUNA kila ukimuongelesha anakujibu kama vile mna UGOMVI au anakupa msaada yaan MTEJA unaonekana msumbufu

Sasa ulilazimishwa kufungua DUKA si ufunge
Mm huwa nawatukana tu na Bidhaa kuniuzia utaniuzia tu kilazima lbda iwe sehemu amabayo siwezi kuifikia
 
Hii ilikuwa NJOMBE tulikuwa tunasamabaza Bidhaa fulani hvyo tukawa tunachukua ORDER mara ya kwanza
wanakuuliza wewe unaitwa nani mtoto wa nani
Na hapo Biashara unamuachia mari kauli sio kama anakupa ela dah ! Tulipambana hvyohvyo kibishi
wanasema huyu wa nyumbani wanakupokea vizuri. Ukabila mbaya sana kwenye biashara
 
Back
Top Bottom