Kuna umuhimu?

Kwa enzi za zamani kuambiana wapenzi wa zamani ingekuwa sawa lakini kwa sasa utapata pressure na ukweli hatakwambia wote na circulation inaweza kujumuisha ndugu zake/zako ukapandwa na pressure na mapenzi yakaisha hapohapo
 
Mkuu,
Nadhani japo tumejadili sana hii ishu, kuna kitu tumeki overlook.
Ni mambo gani ya ku declare.Nadhani kuna mambo ya kimsingi sana mtu anapaswa kuyasema kwa mwenzie hasa kama kuna dalili ya kuwa na uhusiano wa muda mrefu.Kwa uchache nitayataja na nitaomba wengine waongezee kwenye listi:
1. Alishazaa - ( wote mwanamke na mwanaume)
2. Kuwa na hali ya kutoweza kuzaa ( wote)
3. Magonjwa hatarishi kama UKIMWI ( wote)
4.Kuwa na ndoa nyingine ( wote)
sijui kama ni kitu cha maana kutaja ulishalala na watu wangapi kabla ila kama ni lazima ( wote)
5.Kuwa na perversive tendencies ( tigo, chumvini,kupiga chabo etc) -( wote)
6.Ulishatoa mimba au kusaidia kutoa mimba ( wote)


ongezeeni kwenye listi

WoS,

Hebu fafanua hapo..duh..nilikuwa sijui kama ni kosa..maana wakikusikia wenyewe..utahama JF-lol!
 
nami nichangie hoja,yaani kama kuna kitu kinaweza leta shida kwenye uhusiano mpya ni kueleza kule ulikopita,maana ukukutana na mtu mwenye gubu na kinyongo siku mkitibuana tu ndo maana fulani alikuacha unafikiri mimi nitakuweza,Cha msingi tusipende kujua wenzi wetu walipita wapi kabla yetu.
 
Sipati picha itakuwaje Mkeo akikwambia kuwa in the past alishananiiwa na Kaka yako au mdogo wako kabla hamjafahamiana!
 
sioni kama kuna umuhimu wowote... kwani nobody will tell the entire truth.... tena yaliyopita yamepita, why shd i start counting my ex's.... eh jamani, unless obama is one of them, i wd want u to know...ahahahhaha lol
 
sioni kama kuna umuhimu wowote... kwani nobody will tell the entire truth.... tena yaliyopita yamepita, why shd i start counting my ex's.... eh jamani, unless obama is one of them, i wd want u to know...ahahahhaha lol

Shishi jamani Michelle akijua itakuwaje?
 
hakuna haja maana hata mkiambizana havina mchango wowote kwenye mapenzi yenu wala nini!! nyie endeleni na ustaarabu wenu na pale mlioanzia basi,mengin hayana umuhimu!
 
Jamani niseme ukweli hapa. Kama kuna kitu huwa nasikia kinyaa ni kujua huyu demu analiwa/ameshaliwa na fulani. Sikatai najua demu wangu alikuwa anadunguliwa kabla yangu na mimi kadhalika lakini haya ya kujua alikuwa ni nani sitaki kabisa kumjua. Nasema sitaki kujua kabsaaaaaaaaa. Naweza mwacha bure mamsap bure. Ya nini kujijeruhi bure. Kama mmekubaliana kuishi pamoja ka mme na mke ya nini kudodosa ya kale?
Huko nyuma nikigundua gf ana/alikuwa na fulani (yaani ninaye mfahamu kwa sura) biashara inaisha hapo hapo. Usiulize anza moja, jua kua kabla ya wewe alikuwa na mwingine! Kubalianeni kuanza upya finish!!!!!!!!!!!11
 
Ni muhimu sana kuelezana ukweli mlikopita huko nyuma. Ila unafanya 'taimingi' wakati mko kwenye peak flan. Na past yako kama unahisi itamuumiza mwenzio ingiza na uongo kidogo kupunguza makali. Baadaye mkioana kama bado hajagundua, si vibaya ukimalizia sehemu ya mwisho (ukweli ulioficha) ya hadithi yako.
 
Mkiambiana halafu iongeze nini kwenye uhusiano wenu?Nijuavyo mimi, wanawake wanaweza kustahimili kujua waliowatangulia, ila wanaume inawasumbua sana na inaweza kuja kuwa source of conflict baadae!

Ni kweli kabisa sie manjemba tukiambiwa mwanamke aliwahi kuwa na wanaume 100 basi hicho ni kikwazo kikubwa cha kusonga mbelea katika mapenzi hayo ambayo ni machanga.

Wataalmu wa mambo wanadai waname hupenda kutaja namba kubwa ili waonekana wana ujuzi na wanawake hutaja namba ndogo ili waonekane si wajuzi kiasi hicho ;) hivyo kwa akina dada kama njemba inataka kujua ni wanaume wangapi uliowahi kuwa nao basi wawili :) wanatosha kabisa kuwataja na wengine ni siri yako wewe na Mungu wako.
 
Ni muhimu sana kuelezana ukweli mlikopita huko nyuma. Ila unafanya 'taimingi' wakati mko kwenye peak flan. Na past yako kama unahisi itamuumiza mwenzio ingiza na uongo kidogo kupunguza makali. Baadaye mkioana kama bado hajagundua, si vibaya ukimalizia sehemu ya mwisho (ukweli ulioficha) ya hadithi yako.

Ukishasema uwongi ni bora kuuacha uwongo huo kama ulivyo maana Trust kwenye relationship ni kitu muhimu sana. Njemba nyingine zikishaoa halafu aambiwe by the way nilipokwambia kwamba nimetembea na wanaume wawili nilikudanyanya ukweli ni kwamba nimetembea na wanaume 40 hicho kinaweza kikawa chanzo cha ugomvi mkubwa ndani ya ndoa hiyo na si ajabu kuvunjika kwa ndoa. Njemba inaweza kabisa kudai kwamba kama ingeujua ukweli halisi basi isingeamua kukuoa na kuanza kuuliza ni kipi kingine ulichomdanganya. Trust ikipotea kati ya mke na mume basi ndani ya nyumba hakuna amani tena.
 
Back
Top Bottom