Kuna umuhimu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuna umuhimu?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by kisale, Apr 2, 2009.

 1. kisale

  kisale Senior Member

  #1
  Apr 2, 2009
  Joined: Mar 3, 2009
  Messages: 111
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Je!kuna umuhimu wowote kwa wachumba,au wapenzi kuelezana historia zao za kimapenzi za kipindi cha nyuma kabla hawajakutana?kwa mfano labda Belinda umepata mpenzi mpya,kuna umuhimu wa kumwambia ulishawahi kuwa na wanaume 16 tangu kuzaliwa,au mwanaume kukuambia alishawahi kuwa na wanawake 60 tangu kuzaliwa.Je!kuna umuhimu wa kuelezana hizo historia zenu za nyuma?na kama zipo experience inaonesha uongo unatawala mno,hakuna mwanamke aliye tayari kumwambia mpenzi wake alishawahi kuwa na mahusiano na wanaume 22 mpaka walipokutana,na wanaume vivyo hivyo.Je kuna umuhimu wa kujua historia ya mapenzi ya mwandani wako?
   
 2. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #2
  Apr 2, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Mkiambiana halafu iongeze nini kwenye uhusiano wenu?Nijuavyo mimi, wanawake wanaweza kustahimili kujua waliowatangulia, ila wanaume inawasumbua sana na inaweza kuja kuwa source of conflict baadae!
   
 3. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #3
  Apr 2, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Kisale habari.
  Sidhani kama kuna umuhimu wowote ingawa kuna wanaopenda kujua anajihusisha na mtu gani. Ila kwa mawazo yangu kuelezana past kuna madhara yake hasa pale kama mwenzi wako ni mtu wa vinyongo anaweza akaja akakuhunt na hiyo past yako hadi ujute kwa nini ulimwambia. Mimi nadhani mkianza mahusiano mapya ni bora msiyakumbuke ya zamani amueni kuanzia hapo mlipo.
   
 4. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #4
  Apr 2, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Kabisa WoS wengine wana magubu hukawii kusikia ndio maana uliachwa na flani au sishangai kama uliweza kuachwa na hao 6 walionitangulia mie ntakuweza wapi? Wanaume hawastahili kabusa kujua umetembea na wangapi. Unless waambiwe na mtu wa nche na hata wakiambiwa akikuuliza usikiri wala kukana mwambie tu @ Nisingependa kuzungumzia past yangu because my past doesnt exist anymore@
   
 5. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #5
  Apr 2, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  hata kwenye ndoa utasikia mwanaume anakuuliza... niambie nani huwa anakufuatafuata! Sijui ili iweje!
   
 6. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #6
  Apr 2, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 161
  Trophy Points: 160
  Kuna siku tulihitilafiana na mke wangu na it was bitter, sasa katika kujibishana maneno akasema, "..kama ni wanaume nimeona wangapi?...". Hiyo statement ilinikera sana hivyo nilichukua karatasi na kalamu nikaorodhesha majina ya wanawake/wasichana niliyowahi kukutana nao, then nikampatia! halafu chini nikamwandikia na yeye anipe list kisha nikachomoka nyumbani na kuelekea kwenye nyumba za vinywaji. Niliporejea sikumkuta and it took us about six months to settle the fracas -Ndoa ilibakia kidogo kukatika.

  Inatia sana doa kujua mwenzi wako alishawahi kunananiii au kunanniiwa na so many people!!!
   
 7. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #7
  Apr 2, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Pole Baba_Enock mh hiyo statement ya wifi huwa ni kali sana kwqa kina baba wengi huwafanya wajisikie dhohoful hali. Wajua mara nyingi wanaume hupenda wajisikie wao ndio wao hasa kwa mkewe kitu ambacho si kibaya. Anataka awe na hakika kuwa yeye ndio kila kitu kwa mkewe sasa ukimtamkia kuwa wapo wengine wenye uwezo kama wake mh tunaua self esteem yake hata ile manhood yake anahisi imekuwa abused.
   
 8. D

  Dina JF-Expert Member

  #8
  Apr 2, 2009
  Joined: Sep 18, 2008
  Messages: 2,824
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Mimi sioni umuhimu wake kwa kweli, kama mmeshakubaliana ni bora muanze upya. Manake hizo historia mlizoambiana ni kweli zitawa-haunt mpaka mchukie uamuzi wenu wa kukaa kitako na kuhadithiana hayo mahistoria..
   
 9. J

  Joyceline JF-Expert Member

  #9
  Apr 2, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 1,010
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  hakuna umuhimu wowote mnapoanza uhusiano mpya , ya kale yote yamepita mnaanza upya ni maisha yenu wawili walowatangulia hawawahusu tena. halafu wanaume atakuwa anafikiria ukute ana matatizo mbona hao wote wamemuacha na kama ni mwenye gubu lazima ulijue jiji, mimi sitaki kujua na wewe usiniuliza basi.
   
 10. Shishi

  Shishi JF-Expert Member

  #10
  Apr 2, 2009
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,244
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  eti eh??? mijibaba in mambo hii....
   
 11. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #11
  Apr 2, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  B_E
  Ulivyokuwa unaandika hiyo listi yako ulikuwa unajisikiaje?
  Kama yeye hakuandika yake wewe ulikuwa unafukutwa hasira ya nini?
   
 12. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #12
  Apr 2, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Ndio hapo sasa..... afu ukishamwambia anakwambia wewe hapo unawapa green indicators amah!
   
 13. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #13
  Apr 2, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Jamani Sisy mwenzako alikuwa anaandika ili amwonyeshe wifi kuwa wewe unanidharau jua kuna walioniona wa maana na kukuthibitishia list hii hapa. ni wazi kuwa wifi alihisi naye kaambiwa hata mie nshaona wengi na mara nyimgi kwa tafsiri yetu kina mama tunamalizia kabisa..... tena wazuri kukushinda.
   
 14. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #14
  Apr 2, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  what if ukimwambia " kwani na wewe unawatongozaga akina nani?" atajibu

  nini?
  ni bora ukimjibu." hakuna mtu ananifuataga" utasikia " haiwezekani, unanificha tu..... plsss niambie basi nijue tu wala sifanyi kitu!"
   
 15. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #15
  Apr 2, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 161
  Trophy Points: 160

  WofS,

  Hiyo statement aliyotoa ndiyo iliyonipa nguvu ya kufanya listing! I'm on my middle 40s and there is no way kuwa sijakutana na score ya wasichana during my "boyhood". Kwa hiyo tulivyo funga pingu - 14 years ago, I thought we were starting a New Life (in Kyerefaso) and hakukuwa na haja ya kuongelea past/present experience no matter umekasirika kiasi gani!

  Alimwaga Mboga na Mimi nikwamwaga Ugali!

  Imagine if this was your husband, anakwambia "...kwani wanawake nimeona wangapi..." ungefanya nini Wofs?
   
 16. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #16
  Apr 2, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Patamu hapo!
  Na wewe unamalizia...." tena wenye pesa kukuzidi " hahahahah
  Hizo ngumi utakazopata utabaki wewe, Mungu wako na daktari!
   
 17. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #17
  Apr 2, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Duh mkuu unataka umjue adui yako?
  Ukimjua na ikitokea kipindi anapita pita maeneo ya kwako home hapo taswira gani utakayo jenga kichwani?
  Mara nyingi story za nyuma iwa zinakuwa za uongo uongo na kutungwa ili muhusika ajingeee heshima kwa mwenzie na aonekane mwaminifu kumbe wizi mtupu.
   
 18. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #18
  Apr 2, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Mie tena hapo sipo........:D
   
 19. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #19
  Apr 2, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  B_E
  Ningejikaza kisabuni..halafu ningemjibu.." uliona wengi baba, lakini hapa kwangu ndo breki yako..mwisho wa njia! "
  Ila uongo si kazi..ningeumia sana rohoni na ningemchukia sana!
   
 20. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #20
  Apr 2, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Ulewako umwambie utaona reaction yake....unajaribu nguo kwa kuchovya kwenye maji ya betri?
   
Loading...