Kuna umuhimu mkubwa sana kufanya check up ya mifumo ya umeme na electronics kwenye gari yako

JituMirabaMinne

JF-Expert Member
May 4, 2020
3,327
9,328
Kwanza kabisa naomba radhi kwa sababu thread kidogo ni ndefu. Lakini ni muhimu kuisoma kwa sababu inaweza ikaokoa gharama kubwa au hata kuokoa maisha yako.

Sasa tuendelee..

Watu wengi wakienda kufanya ukaguzi(check up) wa magari yao, Huwa wanakagua vitu kama Brake pads/brake shoes, ball joints, bushes, Shock up na vitu vingine vinavyofanana na hivyo.

Lakini kuna vitu vya msingi ambavyo mara nyingi huwa vinaachwa na pengine huenda mwisho wa siku vitu hivyo vikaja kumuingiza mtu kwenye gharama kubwa au hata kuyagharimu maisha yake kuliko kama angejua mapema na kuvibadili. Labda ngoja nielezee mifano hii mitatu labda watu wengi wataweza kunielewa vizuri zaidi.

Mfano wa kwanza:
Baadhi ya relay zikianza kuharibika, winding ya relay huwa inakuwa na Electrical impedance(resistance) kubwa. Hii hupelekea relay hiyo kuzima na kushindwa kufanya kazi kipindi ambacho kutakuwa na high electric load katika gari yako. Hebu fikiria relay ya head lumps inabehave kama nilivoeleza hapo juu then uko barabarani usiku, uko speed mara ghafla taa zinazinazima (Nadhani hapa wote tunajua ni nini kinaweza kutokea).

Au ifikirie EFI relay au Ignition relay iwe na tatizo kama hilo, yaani uko speed tena mteremkoni ghafla engine inazima. Engine ikizima wakati upo kwenye speed kali kuna uwezekano wa wewe kushindwa kulicontrol hilo gari kwa sababu steering na brake zote zinategemea nguvu kutoka kwenye engine( Brake inategemea vacuum kutoka kwenye engine wakati steering inategemea engine kudrive pump ya power steering). Matukio haya mawili yanaweza kukupelekea ukapata ajali mbaya, ambayo ikapelekea ukapata majeraha mabaya au hata kifo kabisa.

Mfano wa pili:
Kwa mfano kuna baadhi ya components kwenye gari(Mfano, Relays) zikianza kufa, Huwa zina tabia ya kuchukua umeme kutoka kwenye battery yako hata kama umezima kabisa gari yako(yaani Switch off). Hii hupelekea battery yako kuchoka haraka na hivyo itakulazima kununua battery nyingine na kama hautarekebisha tatizo kabla ya kununua hiyo battery mpya haijachukua muda imekufa tena.

Hiyo utakuwa unaingia gharama ambazo ungeweza kuziepuka kwa kufanya marekebisho madogo kwenye mfumo wako wa gari na kila kitu kikawa kinaenda poa. Kama ukiacha gari yako hata siku mbili bila kuwasha, then ukaja kuwasha ikagoma hata kucrank, basi huenda una hili tatizo au kuna shoti ambayo inadraw umeme mwingi kutoka kwenye battery.

Mfano wa tatu:
Hili tatizo la bettry kutumika hata kama umezima gari hutokea pia ikiwa gari yako ina Shoti(Short circuit). Shoti hutokea ikiwa nyaya mbili zimegusana(live na ground) au ikitokea waya wa live umegusa chuma chochote katika gari yako. Madhara ya shoti yanaweza kuwa ni madogo kama battery yako ya gari kuisha haraka na kuungua sehemu ambayo shoti inatokea au yanaweza kuwa makubwa kama Gari yako kuwaka moto. Inategemea tu na mazingira ambayo shoti hiyo imetokea.

Hiyo mifano mitatu niliyoeleza hapo juu inaweza kutokea bila wewe kujua kinachoendelea . Labda tu kama ukifanya check up kwenye mifumo ya umeme na electronics ya gari yako ndiyo utaweza kujua. Gari yako haitakiwi kudraw zaidi ya 50mA za current kutoka kwenye bettery kama ikiwa switch off au kwa magari ya kisasa hakutakiwi kuwe na voltage drop yoyote across fuses/au small mV kwa baadhi ya fuses unapokuwa umeweka switch off.

Sasa kutokana na hilo mimi binafsi nimeamua kuanza kufanya check up kwa mtu ambaye atahitaji nimfanyie kwenye gari yake. Basically nitakagua vitu vitatu katika hiyo check up.

1. Nitapima kama kuna Shoti(short circuit) na kujua ukubwa wa hiyo shoti kwenye mifumo yote ya umeme kwenye gari.

2. Nitapima kama kuna Open circuit kwa baadhi ya mifumo.

3. Ntapima kama relay za gari yako zinafanya kazi kama ilivo kwenye manual ya hizo relay. Hapa kwenye relay nitapima vitu vitatu(resistance kati ya pin 85 na 86, nitapima kama relay inatoa mlio ukienergize pin 85 na 86 na mwisho nitapima resistance na continuity kati ya pin 30 na 87 huku nikiwa nimeenergize pin 85 na 86 kwa NO relays au bila kuenergize pin 85 na pin 86 kwa NC relays ). Mafundi wengi hupima tu kama relay inatoa mlio na kusema ni nzima wakati kuna relay zinatoa mlio na ni mbovu au kuna relay ambazo ni solid state. Huwezi kusikia mlio wowote.

Gharama zangu ni nafuu sana. Na pia kama mtu ana gari ya kawaida kazi inaweza kuchukua nusu saa mpaka saa moja. Ila kama gari yako ni ya kisasa, kazi inaweza kuchukua masaa mawili hadi matatu(Hapa gharama itaongezeka kidogo tofauti na mwenye gari la kawaida).

Pia kama kama utahitaji nikufanyie check up ya sensors, switches na components kama sparking plug, coil on plug, sparking plug wires, injector nozzle n.k. ninaweza kukufanyia. Baadhi ya hivi vitu huondolewa kwenye magari kwa madai ya kuwa ni vibovu wakati vingine huwa huwa ni vizima au vingine huhitaji kusafishwa tu na kurudishiwa na vikafanya kazi bila shida. Hivyo watu huingia gharama kubwa ambazo huenda wangeziepuka.
N.B: Ninapozungumzia kupima hizo components sizungumzii kupima kwa kutumia OBD2 Scanner au Code readers.
 
Mkuu tumekusoma na inaonekana kichwani upo njema sana kiongozi.Kwa ushauri wangu ungetoa pia hata makisio ya juu na ya chini ya gharama ambazo mteja utaweza kumtoza,hii italeta hamasa na psychological confidence kwa wateja wengi ambao vipato vyao havilingani,lakini pia itahamasisha hata kwa madreva wanao tumwa safari na maboss wao,atajua hili tatizo ngoja nimpitishie fundi pale Moro na chenji itabaki mfukoni.

Kumbuka kwenye biashara yoyote ile watu wako very sensitive na price.Tupia hapa makadirio ya juu na ya chini ya bei zako maana hata mimi nina tatizo hilo la gari langu na very soon nitakutafuta unipe ufumbuzi.Asante mkuu piga kazi
Kwanza kabisa naomba radhi kwa sababu thread kidogo ni ndefu. Lakini ni muhimu kuisoma kwa sababu inaweza ikaokoa gharama kubwa au hata kuokoa maisha yako.

Sasa tuendelee..
 
Mkuu tumekusoma na inaonekana kichwani upo njema sana kiongozi.Kwa ushauri wangu ungetoa pia hata makisio ya juu na ya chini ya gharama ambazo mteja utaweza kumtoza,hii italeta hamasa na psychological confidence kwa wateja wengi ambao vipato vyao havilingani,lakini pia itahamasisha hata kwa madreva wanao tumwa safari na maboss wao,atajua hili tatizo ngoja nimpitishie fundi pale Moro na chenji itabaki mfukoni.Kumbuka kwenye biashara yoyote ile watu wako very sensitive na price...

Mkuu shukrani sana. Ninaupdate uzi wangu sasa hivi.

Kuhusu swala la bei nmeweka magari katika makundi mawili.

1. Gari za kawaida ni Tsh. 30,000/= tu

2. Gari za kisasa ni Tsh. 55,000/= tu Hapa gharama imeongezeka kidogo kwa sababu method yake inatake time na haifanani ya ile ya gari za kawaida.

Karibu sana mkuu.
 
Safi. Pia ni muhimu sana kujua aina ya relay(utaweza kujua ikiwa relay ina mchoro). Relay nyingi zinazotumika kwenye magari ni Normally open. Akija kukutana na normally closed relay anaweza akadhani ni mbovu... Kwa sababu normally open relay na normally closed relay zinaoperate in an opposite way.
Asante kwa madini.
 
Back
Top Bottom