Kuna ukweli wowote wa sadaka kupelekwa Vatican?

MENERIKI II

JF-Expert Member
Oct 21, 2014
321
534
Habari wana JF kama kichwa hapo juu kinavyojieleza.

Leo kuna rafiki yangu mmoja nimemsikia akisema kuwa kuna sadaka wanazo changia kanisani (Kanisa Katoliki) zinaenda Vatikani. (Yeye ni mkatoliki)

Hili kwangu ndio kwanza nalisikia kwa huyu rafiki yangu, sikutaka kumbishia kwakua mimi sio Mkristo nikajisemea moyoni nitalifanyia kazi nipate uhakika wa hili.

Kama ni kweli inakuaje wao kwa utajili walionao baada ya kutusaidia sisi tuna wasaidia wao?
 
Iko hivi yaani sadaka huwa zinakusanywa kutoka vijijini ndani kabisa huko, makatekista wanazihesabia tena kwa kusimamiwa na watu zaidi ya mmoja, zinaandikwa kiasi halafu katekista anapeleka wilayani

Ikifika wilayani inapelekwa jimboni, yaani mkoani, hapo inapigwa hesabu yote ya mkoa mzima, halafu zinapelekwa makao makuu, hapa naamini wanaingiza bank, zikifika makao makuu sasa ndiyo zinachenjiwa kutoka Tshilingi kwenda Euro zinapelekwa Vatican, sijui kama huo utaratibu wameubadilisha kwa sasa
 
Kuna percentage flani ndogo sana kila jimbo lina wajibu wakupeleka Vatican ilikuwa hasa miaka ya nyuma.

Pia kuna mchango unaitwa Peter’s Pence, au shilingi ya Peter. Mchango huu na mingine hupekekwa Vatican kwa ajili ya uinjilishaji sehemu zile zenye mahitaji makubwa na zilizo maskini.

Michango hii mingi hupelekwa Afrika na huwa ni matrilioni ya hela.
 
Kuna katekista mmoja alipokuwa anazipeleka zile hela jimboni,alikuwa anaongozana na mke wake, akifika mjini anaenda kilabuni, piga ugimbi sana, akimaliza hera analudi zake kijijini

Paroko akaja kustukia mchezo, ilibidi asimamishwe, tulikuwa tunamuita anadhambi ya kula sadaka kipindi hicho wakati mdogo, alikuwa na maisha magumu, watoto zake si kuona hata mmoja ingalau kupewa msaada na kanisa, zaidi ya kuishi kwenye dibwi la umaskini, wakati mapadiri na masista walikuwa wanaishi vizuri tu, baada ya kuwa mkubwa nimemsapoti kwa alichokuwa anakifanya, yaani usalishe usipewe hata hela ya sabuni, halafu sadaka wapewe watu wa Vatikani kweli?

Ukatoliki unauonevu mkubwa sana, ni zaidi ya utumwa
 
Sasa kama kila nchi sadaka zinaenda Vatcan, hao jamaa wa Vatcan wanaweza kununua bara la Afrika wakiamua,fikiria kila wiki sadaka zinaenda vatcan, na sio sadaka za Tanzania tu Duniani kote walipo wa Roman catholic,kila wiki sadaka ziende Vatcan miaka yote,
Kuna jamaa mmoja alikuwa kwenye kitengo cha uhasibu kama sikosea, aliiba hera za huko vatican, ilibidi akodi ndege ili ajaze pesa, isingewezekana kutumia bank

Hao jamaa wanampunga mrefu sana
 
Sadaka zinatumika kwa Kuleta Maendeleo Mahali husika..!
Ndo maana unaweza Kuona Makanisa Yanajengwa kwa utukufu wa Mungu,ili jina Lake litukuzwe.
 
Iko hivi yaani sadaka huwa zinakusanywa kutoka vijijini ndani kabisa huko, makatekista wanazihesabia tena kwa kusimamiwa na watu zaidi ya mmoja, zinaandikwa kiasi halafu katekista anapeleka wilayani

Ikifika wilayani inapelekwa jimboni, yaani mkoani, hapo inapigwa hesabu yote ya mkoa mzima, halafu zinapelekwa makao makuu, hapa naamini wanaingiza bank, zikifika makao makuu sasa ndiyo zinachenjiwa kutoka Tshilingi kwenda Euro zinapelekwa Vatican, sijui kama huo utaratibu wameubadilisha kwa sasa
kuna muvi kanumba alitoa,sadaka zilikusanywa makanisa yote kupelekwa vatcan saa mzee magari akaona sasa huo ni uzuzu akafanya mpango waibe zilepesa zisipelekwe vatican,..koment yako mkuu imenifanya nikumbuke hii muvi .r.i.p kanumba
 
Back
Top Bottom