Kuna ukweli hatutaki kusema kuhusu Sure Boy

Oldmantz

JF-Expert Member
Jan 24, 2023
430
996
ABUBAKAR Salum ‘Sure Boy’. Fundi mmoja wa mpira kuwahi kutokea nchini. Sio huyu wa sasa anayecheza pale Yanga, hapana, huyu ni baba yake mzazi. Ndiye mwenye jina halisi la Sure Boy.

Alipewa jina hilo kutokana na kazi yake njema uwanjani. Alikuwa na kasi kubwa uwanjani. Akipiga krosi na pasi zenye macho na pia alijua kufunga mabao na kulijengena jina tangu akiwa Sigara hadi Yanga na Tanzania Stars. Aliufanya mpira wa miguu kuwa kitu rahisi sana. Wengi wanamkumbuka namna alivyokuwa akikichafua pale Yanga enzi hizo. Inavutia sana.
Kama baba kama mtoto. Baada ya miaka mingi mtoto wake akarithi kila kitu. Tofauti ni kwamba Sure Boy orijino alikuwa winga teleza na mtoto ni kiungo fundi sana. Ndiye huyu Sure Boy wa sasa. Naye baada ya kutamba pale Chamazi kwa miaka mingi, hatimaye ameangukia Yanga. Fundi sana huyu kijana.

Bahati mbaya ni kwamba kama nchi kuna namna tumeshindwa kumpa Sure Boy heshima yake. Tunamchukulia kama mchezaji wa kawaida.
Sure Boy anacheza Ligi Kuu kwa mwaka wa 15 sasa. Alianza akiwa kijana mdogo pale Chamazi. Kwa kifupi umri wa Azam FC kwenye Ligi Kuu ndiyo umri wa Sure Boy pia katika Ligi.
Ni ngumu sana kudumu kwenye soka la ushindani kwa miaka mingi kiasi hicho. Ni wachezaji wachache sana wameweza kufanya hivyo.
Sure Boy anazidi kuwa bora kadri umri wake unavyozidi kusogea. Wakati huu ambapo watu wanahisi kuwa nahodha wa Simba, John Bocco anapaswa kustaafu, ndiyo kwanza Sure Boy anazidi kunoga.
Hawa walianza kucheza pamoja pale Chamazi, lakini muda umefika watu wanaamini kuwa Bocco anapaswa kuondoka kwenye soka, lakini Sure Boy anapaswa kuendelea kuaminiwa pale Yanga na Taifa Stars.
Huu ndio ukweli hatutaki kusema kuhusu Sure Boy. Kucheza katika kiwango cha juu kwa miaka 15 sio jambo rahisi hata kidogo. Ni wachezaji wachache sana wa zama hizi ambao wameweza.

Ukiachana na Bocco, Juma Nyosso pamoja na Kelvin Yondani, ni mchezaji gani mwingine wa zama hizi ameweza kudumu kwa kipindi kirefu hivyo?
Wamekuja mafundi wengi hapa katikati lakini wameshindwa kucheza kwa ubora. Hawa kina Jonas Mkude, Said Ndemla, Ibrahim Ajib na wengineo hawajaweza kufikia kilele cha Sure Boy. Bahati mbaya ni kwamba huko mtaani utakuta Mkude ana sifa nyingi kuliko Sure Boy.
Kwanini? Ni kwa sababu Mkude amedumu muda mrefu pale Simba. Timu yenye mashabiki wengi. Amekuwa midomoni mwa watu kwa muda mrefu.
Kwa kifupi ni kwamba Sure Boy alichelewa kufika timu za Kariakoo na ndio sababu watu wanamchukulia poa. Lakini kwa viungo wa ndani wa zama hizi hakuna mchezaji amekuwa na ufundi wa Sure Boy.
Sure katika ubora wake aliifanya kazi ya soka kuwa rahisi sana. Angelainisha kila kitu pale katikati ya uwanja. Ni kama tu ambavyo anafanya sasa pale Yanga.
Kwa namna anavyocheza, ni ngumu kuwaza kuwa amekuwepo kwenye Ligi hii kwa miaka 15. Ni miaka mingi sana.
Yondani pekee ndiye amedumu kwa muda mrefu zaidi yake. Ana miaka 18 sasa kwenye Ligi. Kati ya hiyo, miaka 13 aliitumia kwenye klabu za Simba na Yanga. Ni miaka mingi sana.
Katika miaka yote, Yondani alikuwa akianza katika vikosi hivyo vya Simba na Yanga. Akaenda Polisi Tanzania nako akawa chaguo la kwanza pia. Akaenda Geita bado ni chaguo la kwanza.
Huwa inatokea mara chache sana katika zama hizi kuona mchezaji ana miaka 18 kwenye Ligi na anaaminiwa kwenye kikosi cha kwanza.
Ni kama ilivyo kwa Juma Nyosso. Naye amedumu kwa miaka mingi sana. Ukiachana na changamoto yake ya nidhamu, bado Nyosso amecheza kwa ubora wa juu mno. Amekuwa chaguo la kwanza kila sehemu aliyokwenda.

Ndiyo sababu nasema inawezekana ni kwa bahati mbaya ama makusudi, lakini ukweli utabaki wazi kuwa hatumpi Sure Boy sifa anazostahili.
Alipaswa kupewa heshima kubwa zaidi. Alipaswa kuwa na jina kubwa zaidi kuliko wachezaji hawa wengi waliodumu kwa miaka minne ama mitano.
Ni kama vile niliwahi kusema hapa wiki chache zilizopita kuwa hatumpi heshima anayostahili Himid Mao. Mchezaji ambaye watu walimchukulia poa lakini yupo pale Misri kwa mwaka wa tano sasa. Ni nadra sana kwa mchezaji wa Tanzania kudumu katika nchi za watu kwa muda mrefu hiyvo.
Bahati nzuri kwa Himid ni kwamba kwa timu zote alizocheza pale Misri, amekuwa ni chaguo la kwanza. Inavutia sana.
CREDIT: MWANASPOTI
 
Binafsi namkubali JUMA NYOSO a.k.a Bongo Nyoso mtu mwenye roho ya paka

Kuhusu sure boy
'KAISHAA' HANA MAAJABU KABSAA
 
Nimemkumbuka Carlos Tevez,siwezi kuishi hapa msimu huu yaani kuanzia asubuhi hadi Jioni sioni jua 🤣🤣
 
Sure Boy huwa anakichafua sana pale katikati.
Sijui kwanini Nabi hakuona anafaa kuanza nae katika mechi ya mkondo wa kwanza wa fainali Vs Usma Alger, huwa naamini angebadili mchezo.
 
Back
Top Bottom