Nimewakumbuka mawinga hatari wa Yanga enzi hizo Marehemu Celestine Sikinde Mbunga na Abubakary Salum Sure Boy

1979Magufuli

JF-Expert Member
Feb 20, 2023
439
1,754
Mimi sio shabiki hoya hoya, nilikuwa nikienda uwanjani bila kujalj kama mm ni Simba lia lia, kiukweli katika maisha yangu moja ya mawinga hatari niliowahi kuwaona kwa macho yangu ni huyu marehemu Celestine Sikinde Mbunga na huyu Abubakary Salum Sure Boy.

Sikinde alitokea Maji Maji ya Songea alikuwa mtu hatari sana, kuna wakati Yanga waliwahi kucheza na timu moja ya Morocco Sikinde na Sure Boy waliwasumbua sana hadi wakapigwa na waarabu hao, Sure Boy alipasuliwa mdomo.Sikinde alikuwa zaidi ya Edibily Lunyamila maana wengi wamemuona Lunyamila lkn sio marehemu Sikinde.

Sikinde akiwa na kijezi chake cha Vimto alikuwa hakabiki, huku kulia akiwa Sure Boy, moja ya mawinga ambao mimi nasema hadi Leo Sure Boy sijapata mfanowe.Sure Boy alikuwa akiniumiza sana moyo wangu alipokuwa akicheza na Simba maana alikuwa ana chenga za maudhi na uwezo wa kumfanya lolote beki wa kushoto.

Kwa maoni yangu, wametokea mawinga wengi akina marehemu Justin's Mtekere , John Alex, Sammy Bitumba Iyela, Akida Makunda nk lakini kwangu sitokuja kuwasahau hawa jamaa. REST IN PEACE SELESTINE SIKINDE MBUNGA
 
Waliusaidia nini mpira wa Tanzania???

Walilisaidia nini TAIFA.

Walilisaidia Nini yanga????

Mafanikio Yao ni yepi???????

UTOTO RAHA SANA!!!!
 
Mimi sio shabiki hoya hoya, nilikuwa nikienda uwanjani bila kujalj kama mm ni Simba lia lia, kiukweli katika maisha yangu moja ya mawinga hatari niliowahi kuwaona kwa macho yangu ni huyu marehemu Celestine Sikinde Mbunga na huyu Abubakary Salum Sure Boy...
Tukisema unajibu Sisi tunakushambulia. Lakini wewe kweli wa kusema Sikinde alimzidi Lunyamila? Endelea kaka maana labda unaandika kitabu lakini kitanunuliwa na watoto wa 2010.
 
Mimi sio shabiki hoya hoya, nilikuwa nikienda uwanjani bila kujalj kama mm ni Simba lia lia, kiukweli katika maisha yangu moja ya mawinga hatari niliowahi kuwaona kwa macho yangu ni huyu marehemu Celestine Sikinde Mbunga na huyu Abubakary Salum Sure Boy.

Sikinde alitokea Maji Maji ya Songea alikuwa mtu hatari sana, kuna wakati Yanga waliwahi kucheza na timu moja ya Morocco Sikinde na Sure Boy waliwasumbua sana hadi wakapigwa na waarabu hao, Sure Boy alipasuliwa mdomo.Sikinde alikuwa zaidi ya Edibily Lunyamila maana wengi wamemuona Lunyamila lkn sio marehemu Sikinde.

Sikinde akiwa na kijezi chake cha Vimto alikuwa hakabiki, huku kulia akiwa Sure Boy, moja ya mawinga ambao mimi nasema hadi Leo Sure Boy sijapata mfanowe.Sure Boy alikuwa akiniumiza sana moyo wangu alipokuwa akicheza na Simba maana alikuwa ana chenga za maudhi na uwezo wa kumfanya lolote beki wa kushoto.

Kwa maoni yangu, wametokea mawinga wengi akina marehemu Justin's Mtekere , John Alex, Sammy Bitumba Iyela, Akida Makunda nk lakini kwangu sitokuja kuwasahau hawa jamaa. REST IN PEACE SELESTINE SIKINDE MBUNGA
Huyu SIKINDE alikuja YANGA akiwa anaishia ishia tena.
SIKINDE haswa alikua MAJIMAJI.
 
Waliusaidia nini mpira wa Tanzania???

Walilisaidia nini TAIFA.

Walilisaidia Nini yanga????

Mafanikio Yao ni yepi???????

UTOTO RAHA SANA!!!!
Football ni teamwork mchezaji mmoja au wawilu hata wawe wazuri vipi kama wengine average players ni kazi bure.
SIKINDE alikua mashine, ukiona mpaka kwenye nchi ya kigeni kocha mzungu wa timu pinzani baada ya mechi anamsifia na kusema jamaa ana uwezo wa kucheza timu kubwa Ulaya ujue alikua na uwezo kweli.
 
Back
Top Bottom