Kama ningekuwa na Remote ya kurudisha nyuma umri wa mtu kipindi hiki Basi ningerudisha umri wa Saidoo ntibazonkiza na Abubakari Salumu (Sure boy).

NALIA NGWENA

JF-Expert Member
Oct 6, 2016
10,206
12,747
Naam! NALIA NGWENA mpenda football Tena mpira mzuri uliojaa talanta ndani yake hakika nimejikuta nawaza na kuwazua kuhusu hizi talanta mbili ambazo umri umeenda lakini ukiwatazama kwenye Pitch bado wanawaka.

(1) Saidoo ntibazonkiza, huyu mtu wa ball kiungo mshambuliaji asiyechuja, mwamba alikichafua Yanga sc Kisha akaenda Geita alikiwasha kwa kiwango kile kile bila kushuka kiwango, Simba sc walimsajili mpaka wanayanga waliona Wivu alivyoendelea kuwa tishio katika kikosi Cha Simba sc.

Kwa kiwango anachokionesha Saidoo ntibazonkiza hakuna kocha anaweza kumuacha laiti Kama isingekua umri huyu Saidoo ntibazonkiza ni hatari na Nusu, ninapomtazama touches zake mpaka huwa natamani kupata Remote ya kurudisha umri nyuma ili aendelee kuleta burudani katika ligi yetu hii.

(2) Abubakari Salumu (Sure boy) , Wengi wamechelewa kumjua huyu kiungo Bamia, huyu kiungo kutoka mitaa ya Chamazi huyu ni Mtu wa ball kabisa, nakumbuka nilishawahi kuleta Uzi humu unaosema "ulipo mpira Sure boy yupo" Naam nafikiri watu wa mpira wanaelewa huyu kiungo namna anavyopenyeza pasi (snake pass) natamani kumuona katika ligi yetu akikichafua milele.

Nidhamu yake kubwa mno huyu fundi wa mpira na ndiyo role model wa Feisal salum Feitoto, Fei Alishawahi kusema "kipindi nakua nilikua nilikua najiita Abubakari Salumu sureboy" katika harakati zangu za mpira.

@@NALIA NGWENA ukinitajia sureboy namkumbuka sure boy Yule aliyewasumbua waarabu kule Tunisia aliwasha Moto dimba la kati.

(3) Khalid Aucho (the tank) Achana na huyu mwamba wa kiganda ni Moto wa kuotea mbali kabisa hakika mchango wake mkubwa Dimba la Kati katika ligi yetu tumeuona bila kificho, Kuna muda Natamani ningekua na Remote ningerudisha nyuma umri wake Hadi miaka 18 aendelee kuleta burudani katika ligi yetu
ya Tanzania.

Huyu kiungo kwa Dimba la Kati Hana mpinzani japokua Tuzo za TFF za kinafiki zinampitia kushoto.

(4) John Bocco the Fantastic captain zao la Azam kutoka Chamazi huyu mwamba kafanya makubwa sana tuliomshuhudia akifanya maajabu hatuna la kumdai Ila tunasema aheshimiwe na mchango wake katika klabu ya Simba sc utambulike.

Mashabiki acheni zomea zomea kwa legend huyu kafanya mengi sana laiti kama ningekua na Remote ningerudisha umri wake Nyuma aendelee kuleta burudani.

(5) Chama (mwamba wa Lusaka) nakumbuka huyu mwamba aliwatesa Yanga Sc kipindi hicho Yanga tia maji tia maji, Ilikua ni Gemu ya Derby Chama alinifanya nikalia nikatoa machozi kwa jinsi anavyowanyanyasa wachezaji wa timu yangu Yanga sc.

Sijui Kama atakuja kutokea fundi wa mpira Kama huyu mwamba, mwamba anaetembea na mpira Kama hataki watu wa Yanga tunamuita konokono au Kobe lakini alikua hatari balaa.

Hao wachezaji mpaka Sasa wapo wanakiwasha laiti Kama ningepata Remote ya kurudisha nyuma umri ningewadisha hao.

Unaweza kuongezea wako bila kujali Usimba na Uyanga.
 
Hapo ujakuwepo enzi za nsajingwa,Pawasa,Machupa na hata Ivon mapunda wa juzi
Nimezungumzia kipindi hiki na bado wanaendelea kucheza mkuu najua malegend wapo waliokiwasha kuliko hata hao nilio wataja.
 
Hapo hamna mchezaji... Mi ningepwa limoti ningerudisha nyuma umri wa Mrisho Ngassa ili Niweze Ku ENJOY SOCCER....
Jamaa aliwahi kuwapiga chenga wachezaji wa Simba halafu akaukalia Mpira ilikua balaa...kuna Muda Ngassa alitakiwa kuzaliwa Brazil akacheze zake Barcelona
 
SAWA MKUU
 
Naam! NALIA NGWENA mpenda football Tena mpira mzuri uliojaa talanta ndani yake hakika nimejikuta nawaza na kuwazua kuhusu hizi talanta mbili ambazo umri umeenda lakini ukiwatazama kwenye Pitch bado wanawaka.

(1) Saidoo ntibazonkiza, huyu mtu wa ball kiungo mshambuliaji asiyechuja, mwamba alikichafua Yanga sc Kisha akaenda Geita alikiwasha kwa kiwango kile kile bila kushuka kiwango, Simba sc walimsajili mpaka wanayanga waliona Wivu alivyoendelea kuwa tishio katika kikosi Cha Simba sc.

Kwa kiwango anachokionesha Saidoo ntibazonkiza hakuna kocha anaweza kumuacha laiti Kama isingekua umri huyu Saidoo ntibazonkiza ni hatari na Nusu, ninapomtazama touches zake mpaka huwa natamani kupata Remote ya kurudisha umri nyuma ili aendelee kuleta burudani katika ligi yetu hii.

(2) Abubakari Salumu (Sure boy) , Wengi wamechelewa kumjua huyu kiungo Bamia, huyu kiungo kutoka mitaa ya Chamazi huyu ni Mtu wa ball kabisa, nakumbuka nilishawahi kuleta Uzi humu unaosema "ulipo mpira Sure boy yupo" Naam nafikiri watu wa mpira wanaelewa huyu kiungo namna anavyopenyeza pasi (snake pass) natamani kumuona katika ligi yetu akikichafua milele.

Nidhamu yake kubwa mno huyu fundi wa mpira na ndiyo role model wa Feisal salum Feitoto, Fei Alishawahi kusema "kipindi nakua nilikua nilikua najiita Abubakari Salumu sureboy" katika harakati zangu za mpira.

@@NALIA NGWENA ukinitajia sureboy namkumbuka sure boy Yule aliyewasumbua waarabu kule Tunisia aliwasha Moto dimba la kati.

(3) Khalid Aucho (the tank) Achana na huyu mwamba wa kiganda ni Moto wa kuotea mbali kabisa hakika mchango wake mkubwa Dimba la Kati katika ligi yetu tumeuona bila kificho, Kuna muda Natamani ningekua na Remote ningerudisha nyuma umri wake Hadi miaka 18 aendelee kuleta burudani katika ligi yetu
ya Tanzania.

Huyu kiungo kwa Dimba la Kati Hana mpinzani japokua Tuzo za TFF za kinafiki zinampitia kushoto.

(4) John Bocco the Fantastic captain zao la Azam kutoka Chamazi huyu mwamba kafanya makubwa sana tuliomshuhudia akifanya maajabu hatuna la kumdai Ila tunasema aheshimiwe na mchango wake katika klabu ya Simba sc utambulike.

Mashabiki acheni zomea zomea kwa legend huyu kafanya mengi sana laiti kama ningekua na Remote ningerudisha umri wake Nyuma aendelee kuleta burudani.

(5) Chama (mwamba wa Lusaka) nakumbuka huyu mwamba aliwatesa Yanga Sc kipindi hicho Yanga tia maji tia maji, Ilikua ni Gemu ya Derby Chama alinifanya nikalia nikatoa machozi kwa jinsi anavyowanyanyasa wachezaji wa timu yangu Yanga sc.

Sijui Kama atakuja kutokea fundi wa mpira Kama huyu mwamba, mwamba anaetembea na mpira Kama hataki watu wa Yanga tunamuita konokono au Kobe lakini alikua hatari balaa.

Hao wachezaji mpaka Sasa wapo wanakiwasha laiti Kama ningepata Remote ya kurudisha nyuma umri ningewadisha hao.

Unaweza kuongezea wako bila kujali Usimba na Uyanga.
Ukifanikiwa kurudisha nyuma umri wa hiyo miamba hutafanikiwa kurudisha umri tu, kila kitu kitarudi proportionally.
Sijui wakirudi kwenye umri ambao hutakua na access nao
 
Back
Top Bottom