Kuna uhusiano gani wa lugha ya kiarabu na majini?

Me pia najiulizaga, kwanini majini karibu yote yana majina ya kiarabu? Sijawahi kusikia jinni linaitwa Joseph, John au basi hata Jini Mary/Maria, Hellen, Lidia nk, majini karibu yote niliowahi kuyasikia ni Maimuna, Makata, Juja wa majujani, Rajabu nk. Ndio na mimi najiuliza, je kuna uhusiano wowote wa Kiarabu na majini?
 
Wewe binafsi ushawahi kumsikia jini akitaja jina lake au unasikia watu wakisema hivyo tu kuwa majini wana majina ya kiarabu? Kwa mfano labda kanisani wakati wakitoa watu mapepo huwa wanauliza majina na kutaja majina ya kiarabu tu?
 
Proof
Ipo kwenye Qurani.
Soma Surat Jinn, utaelewa vizuri.
Inasema Majini ni Waislamu wenzenu.
Na mpaka yanawaita ndugu zenu.
Kwanini wewe hujui hili ?
Ila tatizo hapa ni kwamba waislamu wanaposema jini hukusudia tofauti na wakristo wakisema jini,na ndiyo maana utata unaanza hapo mkristo ajuavyo yeye kuwa majini ni malaika waovu hivyo hakuna jema kutoka kwao na muislamu ajuavyo yeye hakuna malaika muovu malaika wote hutenda mema tu ni tofauti na binadamu mwenye uhuru wa kuchagua kutenda mema au uovu na jini ni kiumbe tofauti hana asili na malaika na ndiyo maana hutenda mema na wakati mwengine huweza kutenda mabaya.
 
Wewe binafsi ushawahi kumsikia jini akitaja jina lake au unasikia watu wakisema hivyo tu kuwa majini wana majina ya kiarabu? Kwa mfano labda kanisani wakati wakitoa watu mapepo huwa wanauliza majina na kutaja majina ya kiarabu tu?
Yote ya maswali yako, majibu yangu ni NDIO
 
Umenena vyema Sana.
Unajua Siku zote Binadamu anapopandisha Jini.
Jini likiulizwa, unaishi naye vipi huyo mkiti wako yaani Binadamu uliyemkalia ?
Siku zote Jini linajibu namtendea mambo maovu Kama kumpa magonjwa, kumfanya awe maskini, kumfanya taahira au Tasa na mambo Kama hayo.
Sijawahi kusikia popote Jini anasema anamsaidia Binadamu kwa Jambo jema, huu ni ushahidi wa ana kwa ana.
Sijawahi kusikia Jini yeyote anasema anamcha Mwenyezi Mungu.
Sasa Bwana Tz mbongo, unaweza kutupa ushahidi wowote wa Jini kutenda wema popote pale. ?
Ndio maana Wakristo sio tu Kwamba wanaamini Bali ndivyo wanavyofundishwa na Mungu wao, Kwamba hakuna Jini Jema.
Chukua Mfano.
Yesu alipokutana na mtu mwenye Majini kule ziwani, aliyakemea na kuyafukuzia kwenye Nguruwe.
Je Ni kwanini aliyafukuza? Na kwanini hakupatana nayo ?
Yesu pia aliletewa Kijana Ambaye anaanguka kifafa kwa kusababishwa na kukaliwa na Majini, alipoyafukuza Kijana akapona tatizo lake.
Hivyo hadi anapaa Mbinguni Yesu hakupatana na Majini Wala hakusema kuwa mengine ni mema na aliwaagiza wanafunzi wake kuyakemea na kuyafukuzia mapepo popote watakapo kutana nayo.
Katika Agano la kale Kitabu cha Mambo ya Walawi aya ya 17 mstari wa 7, Mungu anawaonya watu kuto husiana na Majini kwa maisha yao yote.
Hakusema kuna mengine ni mazuri, wala kusema iko siku huko mbeleni yatatubu na kuwa mema.
Biblia inasema Mapepo na Majini ni wafuasi wa Ibirisi, yaani ni Malaika wa Ibirisi Rusifer, ambaye Yuko katika Utawala wa Giza.
Inasema Kuna Malaika wa Nuru, ambao wapo upande wa Mungu, na Malaika wa Giza, ambao ndio Majini.
Full stop.
Sasa Naomba wewe unipe Jambo moja tu Jema ambalo linafanywa na hayo Majini Mema.
 
Yote ya maswali yako, majibu yangu ni NDIO
Sasa mkuu unavyoelewa wewe kwa mfano hilo jina Maimuna au makata ni jina la jini au type ya jini? Maana tunasikia kuwa majini wana majina ya kiarabu ila mara nyingi utaona hayo majina ya Maimuna mara Makata ndiyo hutolewa mfano,hapa watu wanachanganya kati ya majina ya majini na majina ya type za majini ila kwa majina ni kwamba majini wana majina tofauti tofauti na sio ya kiarabu tu kama watu wengine humu ambao wamepata kushuhudia majini wenye majina ya kizungu na n.k Sasa sielewi kwanini kanisani tu ndio kuwe na majini wenye ya kiarabu tu?
 
Mkuu elewa kuwa kinachofanya uwe mwema au muovu ni matendo yako na si kwamba kuna majini wenye asili ya wema na wenye asili ya uovu hata hao malaika waovu unaosema ni baada ya vitendo vyao vya uovu,sasa kitendo cha jini kumuingia binaadamu ni kitendo kibaya kwamba hakiruhusiwi bila kujari amemuingia huyo binaadamu kwa sababu ipi maana si kila jini anayemungia binaadamu huwa anakusudia kumfanyia maovu labda wewe tu hujawahi kusikia kwamba kuna majini huwaingia binadamu kwa sababu amempenda huyo mtu na anaweza kumfanyia mengi tu mazuri wapo wengine huwakinga huwapenda watu na kuwakinga mabalaa ila pamoja na yote kitendo cha jini kumuingia mtu ndicho kisichotakiwa hivyo jini akifanya hivyo amefanya makosa iwe kwa kujua ama kutokujua.

Sasa hayo ya malaika waovu ni kesi tofauti na majini na ndiyo maana kwenye majini kuna majini mahaba ambao hufanya mapenzi na binaadamu kitu ambacho sijui kama kinawezekana kwa malaika.
 
imekuaje hadi nikajiuliza hilo swali?

story yenyewe iko hivi.

nina rafiki yangu wa kike,siku za hivi karibuni yapata kama mwezi sasa,mara kwa mara na humtokea baada ya kutoka kusali tu,anajikuta anandika vitu ambavyo hata yeye havijui.anakuja kushtuka tu ameandika.hiyo hali haikutushtua na tuliona kawaida tu

kilichotushtua ni hiki

alianza kuandika kwa kukoroga koroga kama ambavyo watoto wa awali huwa wanafanya wakipewa daftari na peni bila kufundishwa chochote.kisha akaanza kuimprove kidogo kidogo na ikafikia hatua anaandika kitu furan kinachoeleweka ambacho hatujui ni nini na ni lugha gani.

kwa kifupi kapitia hatua zote za mtu ambaye anajifunza kuandika lakini hata yeye binafsi hajui.ila anaandika mtindo kama kikolea au kichina kwa kwenda chini,tumejaribu kugoogle lugha mbali mbali hatukupata hata lugha moja ya mtindo huo

mashaka yakaanza
baada ya hiyo hali tukaanza kupata mashaka kua inawezekana kuna namna kiroho,pengine ni lugha ya kiMungu au ni mapepo.

tukaona tuwashirikishe watu wa Mungu(nazungumzia waokovu).siku ya ijumaa ikabid aende kwenye jumuiya na akawasimulia kila kitu.
baada ya kuonesha hilo daftar analoandika mama wa kwanza tu ambaye ndio mkuu wa jumuiya akashtuka ,akasema hiki si kiarabu lugha ya mashetani au majini.kisha akamwambia chukua namba ya simu badae utanipigia.lakini mpaka saizi hatujampigia maana bado tunamaswali mengi juu ya kauli yake.

swali liko hivi.
Ni kwanini ?hasa wakristo huwa wanahusisha lugha ya kiarabu na mambo ya kishirikina,majini,mapepo nk.
ikitokea sehemu yoyote ambayo inautata frani hivi kukawa na lugha ya kiarabu basi wazo la kwanza ni mapepo.

hiki kitu nmekisikia mara nyingi na nlijua ni kwa watu ambao hawajui.mambo ya Mungu sasa kilichonishangaza hadi myu wa Mungu nae yumo kwenye huo mkumbo.

mwenye ufahamu tafadhali tubadirishane uzoefu.

Angalizo,mimi ni mkristo na naamini katika Mungu,pia naheshimi dini zote duniani.kama.ninavyoheshimu dini yangu.mada kama hizi huwa hazichelewi kuhama lakini mimi sipo hapa kukashifu dini ya mtu yeyote.nipo hapa kupata ufafanuzi.na pia kama kutakua na mtu ambaye anaweza kunisaidia kuhusu tatizo la huyo dada nitamshukuru sana.

kama kuna sehem patahitaji kueleweshana nipo hapa,

natanguliza shukran
Kiarabu au Irab????
Mfano kila irab unayoiona inaandikwa toka kushoto kwenda kulia ni kiarabu? Iran,Pakistan,Afghastan nk maandishi yao unaweza hisi ni kiarabu lakin ata waarabu hawawez soma au wakisoma hawaelewi ni nini kilichoandikwa! Maandishi ya kiswahili japo yatafanana na maandiahi (Irab) za kimasai lakin huwez sema ni kiswahili.....
 
Hata huko Marekani kuna Majini / shetani ndipo mpaka hizi filamu nyengine husema kuwa zina asili ya ukweli, ingekuwa hayapo, basi wangesema tu sehemu fulani Afrika n.k
Ila hapa kwetu ndio yanafuatiliwa sana haya mambo.
 
Ndugu zetu huwa mnajitahidi sana kukataa hili, ila ukweli kuna uhusiano mkubwa wa quran, kiarabu na majini.

Hivi vitu vinaenda sambamba kama nyanya kitunguu na chumvi.

Eleza tu vinahusiana kivipi mkuu,mbona kama huna uhakika na ulisemalo
 
Au ashawahi sikia jinni linaitwa Maria,
Huwa najiuliza mie, nchi kama Brazil, Cuba n.k wao hutumia Vodoo, sijui majini hayo yanatumia majina kama ya kwetu ? Au wao hutumia María, José n.k ?
Haya tunayaita sisi hivi kwa mazingira yetu, ambapo wamepewa majina hayo. Sasa ukienda Zimbabwe usitarajie majina ya huku ....
 
Kwanini watu wakipandisha majini wanaongea kiarabu??
Swali ni wote huongear kiarabu?
Nshawahi kuona wanaoongea kiswahili cha pwani na waongeao kimasai,na hawa utasemaje?

Majini ni miongoni mwa viumbe wajuao lugha nyingi hata kiingereza,unataka useme ulaya hakuna majini? Au wa huko pia wanazungumza kiarabu?
 
Mkuu labda hufanyi tafiti ,hao hao wazungu wameya categorize majini kwa makundi tofauti tofauti.,

na wameyapa majina tofauti tofauti,,kuna majina zaidi ya 100 ya majini kwa lugha ya kiyahudi.

pia kuna majina ya majini kedekede kwa kizungu hivyo hivyo kwa kichina nk...

ungesoma theolojia ya hizi vitu ungeshajua kuna majina ya kigiriki ya majini tofauti tofauti,kiyahudi,kiwelsh,kihindu,kiarabu nk..mbona hujiulizi masuala ya nyota ya capricorn,cancer na nyota zipo kwa kiingereza..ukija TZ ukiwatafuta waganga watakupa majina ya mizimu na majini nk..

baadhi yao haya hapa

Abaddon
Abraxas
Adramelech
Agares
Ahriman
Aim/Haborym
Alastor
Alloces
Amdusias/ Amduscias
Amon
Amy
Andras
Andrealphus
Andromalius
Anzu
Asmoday/Asmodeus
Astaroth
Astarte/ Astaroth

Azazel
Bael
Balam
Barbatos
Bathin
Beelzebub
Behemoth
Beleth
Belial
Belphegor
Berith
Bhairava (Shiva)
Bifrons
Botis
Buer
Bune
Cacus

Cali (Kali)
Callicantzaros
Camio
Cerberus
Chiang-shih (or kiang shi)
Cimejes
Crocell
Daevas
Dagwanoenyent
Daityas
Dantalion
Decarabia
Deumus
Eligos/Abigor
Ereshkigal
Erinyes
Eurynome
Samael
Lezabel
Jezebeth

Asante mkuu
 
Sasa mkuu unavyoelewa wewe kwa mfano hilo jina Maimuna au makata ni jina la jini au type ya jini? Maana tunasikia kuwa majini wana majina ya kiarabu ila mara nyingi utaona hayo majina ya Maimuna mara Makata ndiyo hutolewa mfano,hapa watu wanachanganya kati ya majina ya majini na majina ya type za majini ila kwa majina ni kwamba majini wana majina tofauti tofauti na sio ya kiarabu tu kama watu wengine humu ambao wamepata kushuhudia majini wenye majina ya kizungu na n.k Sasa sielewi kwanini kanisani tu ndio kuwe na majini wenye ya kiarabu tu?
Mi sijui, ukisema kanisani utakua unawaonea watu wa kanisani cause sio wao waliotoa hayo majina, majina hayo hua yanatamka yenyewe yanapokutanaga na moto wa huko kanisani ( YESU) buta again hata ukizisoma habari za majini kupitia maandishi ya wana zuoni wa Kiislam ( mfano Sheikh Yaha ) na wenyewe hua wanataja majina hayo hayo ya kina maimuna, mahaba, Anzura nk.
 
Wewe binafsi ushawahi kumsikia jini akitaja jina lake au unasikia watu wakisema hivyo tu kuwa majini wana majina ya kiarabu? Kwa mfano labda kanisani wakati wakitoa watu mapepo huwa wanauliza majina na kutaja majina ya kiarabu tu?
My answer is definitely YES, nimewahi kusikia sio mara moja au mara mbili, mara nyingi tu na tena sio kanisani tu hata maandishi ya Waislamu wenyewe huandika hivyo hivyo.
 
My answer is definitely YES, nimewahi kusikia sio mara moja au mara mbili, mara nyingi tu na tena sio kanisani tu hata maandishi ya Waislamu wenyewe huandika hivyo hivyo.
Kwenye maandishi ya waislamu utakuta wakieleza kwamba majini sio tu kwamba wana majina ya kizungu bali kuna hadi majini wenye imani ya ukristo na wengine hawana dini kabisa.
 
Mi sijui, ukisema kanisani utakua unawaonea watu wa kanisani cause sio wao waliotoa hayo majina, majina hayo hua yanatamka yenyewe yanapokutanaga na moto wa huko kanisani ( YESU) buta again hata ukizisoma habari za majini kupitia maandishi ya wana zuoni wa Kiislam ( mfano Sheikh Yaha ) na wenyewe hua wanataja majina hayo hayo ya kina maimuna, mahaba, Anzura nk.
Ndiyo maana nikakwambia hayo si majina ya majini bali ni aina za majini maana majini wako wengi hivyo wako aina ya majini ambao ni majini mahaba,makata na wengineo,na ndiyo maana ukienda hata huko arabuni utakuta hao majini mahaba wanaitwa tofauti hawaitwi majini mahaba.
 
Back
Top Bottom