Maana ya mnara wa babeli na mwanzo wa kuvurugika kwa lugha moja

LA7

JF-Expert Member
Aug 26, 2019
457
1,744
Usiku wa Leo nikiwa Dunia ya Sita kama kawaida nilikuwa na Mababu zangu ili kuzungumza, Mara zote nimekuwa nikiwauliza juu ya Dini za Dunia ya Tatu, niliwauliza kuhusu Mnara wa Babel na swali langu lilikuwa hivi "Babu zangu eeh, Hivi mnara wa Babeli ni kweli ulikuwa na Urefu wa kutaka kumfikia MUNGU? ndio maana Mungu akauvunja? Na hapo ndipo Lugha zilianzia?"

Babu mmoja amenijibu
"Mjukuu wangu Biblia au Quran ni vitabu vilivyo andikwa kwa Mafumbo makubwa Sana, yakupasa utumie akili kubwa kuyafumbua mafumbo hayo, Hakujawahi kujengwa Mnara wa Babel popote pale Duniani hiyo wametumia tu neno mnara Ila wana Maanisha tofauti kabisa."

"Mwanzo 11, 6_7 Ndipo Yehova akasema: "Tazama watu hawa ni kitu kimoja na wanazungumza lugha moja, na hili ndilo jambo waliloanza kufanya. Sasa hakuna jambo lolote wanalokusudia kufanya litakalowashinda. 7 (njooni!) Tushuke huko na kuvuruga lugha yao ili kila mmoja wao asiielewe lugha ya mwenzake"

"Sasa Mjukuu wangu ipo hivi Kabla ya Dini kutungwa Watu wote walikuwa wakiabudu Mungu wao tena kwa Umoja na Mungu aliwajibu kabisaa ndio maana unaona wanasema (hakuna jambo lolote wanalokusudia kufanya litakalo washinda) Watu mvua ilipokosekana walimuomba Mungu na mvua ilinyesha dakika hiyo hiyo, palipotokea janga lolote iwe ugonjwa watu waliomba na janga hilo liliisha, jambo hili la Umoja na kumuomba Mungu na kujibiwa haraka hawakulitaka kabisaa"

"Kwa hiyo unaposoma kuwa Mnara wa Babel ulipoangushwa na kuwatawanya watu duniani kote ina maana
"Imani ya Kweli ya Umoja ndio imesimama kama Mnara Babel. Walipofanikiwa Kuivunja Imani ya kweli na kuleta sasa Dini zao ndipo ilipo maana ya Msitari wa Saba unaosema (Njooni Tushuke huko na kuvuruga lugha yao ili kila mmoja wao asiielewe lugha mwenzake) Leo hii Mkristo wanaelewana na Muislamu? Jibu ni hapana kwa hiyo hapo walifanikiwa kutimiza Adhima yao ya kila mmoja kuwa na Lugha tofauti (dini tofauti, kila aliyeishika Dini aliona ya kwake ndio Bora kuliko ya Mwenzake, na huo ndio ukawa Mvurugano wa kutoelewana Lugha) maana Msitari wa nane hapo Mwanzo 11, 8 wakasema Basi Yehova akawatawanya duniani pote kutoka huko, na hatua kwa hatua wakaacha kujenga jiji hilo."

Hapo wana maanisha kuwa Baada ya kuwavuruga katika Imani yenu (Kuangusha Mnara wa Babel) Wakaanza kuwatawanya Duniani pote (wakaanza kuchukuliwa Utumwa) na kuacha kujenga jiji hilo. (Na kuacha kuijenga Africa na kwenda kujenga Nchi Zao, Mjukuu wangu naamini Leo utakuwa umejifunza kitu kuhusu Mnara wa Babel, Najua wapo watakao kupinga Ila naomba uwaulize wakikupa majibu basi uwe katika Dini zao.

1. Waulize hivi Mnara huo Ulikuwa na Urefu kiasi gani Mpaka Mungu aogope kufikiwa na Watu wake? Ulikuwa ni Mrefu kuliko jengo la Dubai? Ikiwa watajibu ndio waulize.

2. kutoka hapo Dunia ya Tatu hadi huko wanaposema ni mbinguni kuna Umbali gani? Kama watashindwa basi waulize hivi Ikiwa Mungu aliuangusha Mnara kwa hofu ya kufikiwa Mbona Leo hii Mataifa hayo hayo yalio andika habari za mnara wa Babel wanarusha Vyombo Nje kabisa ya Sayari hiyo ya Tatu kufanya utafiti, je Huyo Mungu haogopi kufikiwa?"

Hakika Babu amenijibu huku akilia sana Amechukia wajukuu zake wasaliti.

imeandikwa na crow prince
 
Back
Top Bottom