Kuna uhusiano gani kati ya akili na malezi?

Mawazo yangu,
Hamna uhusiano wa moja kwa moja kati ya akili(intelligence) na malezi. Akili(intelligence) ni uwezo wa mtu binafsi aliozaliwa nao ila intellect(kisomo) ni mtu anajifunza katika makuzi yake ambapo kipimo chake ni IQ test.
Malezi ni way of life ambayo ni more of a social aspect (inapimwa kijamii).
Mi nafkiri utofauti kati ya hizo familia mbili ni PLATFORM tu ya kuwasilisha uwezo wao na fikra zao ambayo ndo ina athiriwa na mazingira na kipato.
Akili sio intelligence, intelligence ni kijisehemu cha akili,

Akili kwa kiingereza ni mind au Mental au psych
 
Sijui wenzangu mnaelewa nini kuhusu akili.

Kwa upande wangu nasema akili haina uhusiano na malezi, akili ni akili tu, mtu anazaliwanazo(karithi kutoka kwa wazazi).

=>Pia binadamu tumezidiana uwezo wa kiakili, usije ukafikilia kua kipindi watoto wanazaliwa huwa wanakua na akili sawa hapana.

=>Mazingira ya malezi ambayo mtu anayokulia yanazaa kitu kinaitwa ustarabu.<=>(Eksipozya ya mtu itapelekea kua au kutokua na busara).

Mtu kua mstarabu wa ushuani, malezi bora haina maana ndio anaakili wapo wenye uwezo mkubwa wa akili na wakawaida, hivyo hivyo hata uswahilini.

Mtu kutokua mstarabu haina maana ndio hana akili ( mtu anakula bangi matusi wizi nk) lakini akili zimo, na wapo ambao wakawaida pia.
Mfano; 20% na 👮🏿Sele, 😂🏃🏾🏃🏾🏃🏾

=>Duniani huko kuna waharifu/wauwaji na majambazi wanauwezo mkubwa wa akili ila ndio hivyo tena ustaarabu ni zer0.
Mkuu kuna njia ya kutambua akili ya mtu bila kuangalia amefanya jambo gani(au kusema) ambalo limeleta tija kwa watu wanaomzunguka ?

Yaani bila mtu kusema na kutenda unawezaje kujua kama ana akili nyingi au laa ?
 
Nadhani matendo yake ndio yatakayo tujulisha kua anauwezo kiasi gani.

Kufanya matendo mazuri na yenye tija kwa jamii haimaanishi ndio anaakili, na kinyume chake. Kuna watu wanauwezo mkubwa tu ila hawajajikita huko, (hii ni kutokana na malezi (exposure)),

Ma-genius wengi tunaowafahamu walikua ni watu wenye akili alafu wakaendana... waka-match na mazingira(exposure), wakateleza na iyo chance.

Naamini Kulikua na wengine wengi tu walikua na uwezo ila hawakupata mazingira sahihi, hakuna equal chance duniani.

Kuna watu wanauwezo mkubwa ila wanautumia/wanatumika kwenye mambo ya ovyo.

Mfano; mashindano ya riadha au urembo wale walioshinda walipata nafasi ya kushiliki sio kwamba ndio wanaongoza duniani, kuna watu dunia za tatu huku wanajishughulisha na kuwinda swala, kuna watu wazuri wamejikita kwenye kudanga(au mama wa nyumbani tu).

NOTE. Ili tuelewane vizuri inatakiwa wote tupate maana sahih i ya akili. Wengi naona tunachanganya na ustaarabu.
 
Mkuu bado hujajibu swali langu.

Unajuaje kuwa huyu mtu ana akili kubwa bila kuangalia anayoyatenda au kuyasema ?

Naamini Kulikua na wengine wengi tu walikua na uwezo ila hawakupata mazingira sahihi,
Umejuaje kama walikuwa na uwezo wakati hawakupata mazingira ya kuonesha uwezo wao ?
Kuna watu wanauwezo mkubwa tu ila hawajajikita huko
Umejuaje kama wana uwezo mkubwa ?
Mfano; mashindano ya riadha au urembo wale walioshinda walipata nafasi ya kushiliki sio kwamba ndio wanaongoza duniani, kuna watu dunia za tatu huku wanajishughulisha na kuwinda swala, kuna watu wazuri wamejikita kwenye kudanga(au mama wa nyumbani tu).
Hapa tayari umeshagusia matendo yanayoonekana kama vile uzuri au kuwinda ama kukimbia,ili tujue mtu anauwezo wa kukimbia lazima akimbie tumuone.

Ili tujue huyu mtu ni mzuri lazima tuuone uzuri wake utuvutie,hapo maana yake uko pamoja na kauli yangu kwamba tunadefine uwezo ama akili baada ya kuona matendo.
 
Mkuu bado hujajibu swali langu.

Unajuaje kuwa huyu mtu ana akili kubwa bila kuangalia anayoyatenda au kuyasema ?

Umejuaje kama walikuwa na uwezo wakati hawakupata mazingira ya kuonesha uwezo wao ?

Umejuaje kama wana uwezo mkubwa ?

Hapa tayari umeshagusia matendo yanayoonekana kama vile uzuri au kuwinda ama kukimbia,ili tujue mtu anauwezo wa kukimbia lazima akimbie tumuone.

Ili tujue huyu mtu ni mzuri lazima tuuone uzuri wake utuvutie,hapo maana yake uko pamoja na kauli yangu kwamba tunadefine uwezo ama akili baada ya kuona matendo.
Nimekujibu apo mkuu
Nadhani matendo yake ndio yatakayo tujulisha kua anauwezo kiasi gani.
Umejuaje kama walikuwa na uwezo wakati hawakupata mazingira ya kuonesha uwezo wao ?
Katika hili sijafanyia utafiti hivyo sina haki ya kusema. Ila...

Kwa akili tu yakawaida ukifikilia utaona watu wenye uwezo mkubwa walikuepo wapo zaidi ya hawa tunaowatambua na watakuepo ila kwenye kufahamika sasa.

Naweza kusema nimejua kutokana na kigezo kwamba hakuna equal chance, laiti kama kungekua na fursa sawa kwa wote wangetambulika zaidi.

Mfano; hawa waliofika vyuo vikuu kuna Wa kawaida na wenye akili kubwa haina maana kuwa wasiofika vyuoni hawana akili kubwa, wengi walikosa fursa.
 
Kipimo cha akili kubwa ni kufanya mambo makubwa ambayo watu wengi kama wewe wamgeshindwa kufanya.

Isack newton ni akili kubwa kwa sababu alifanya mambo makubwa ambayo wengi hawakufikiria kuyafanya.

Eistein ni akili kubwa kwa sababu kafanya mambo makubwa ambayo wengi hawakuyafanya.

Sliyegundua simu ni akili kubwa kwa sababu wengi hawakufanya.

Hivyo akili kubwa ni kufanya mambo makubwa katika jamii yako au kwa watu wanaokuzunguka.

Ukipata G.P.A YA 5 alafu ikawa wewe ndio wa mwanzo kupata hiyo tunasema wewe ni akili kubwa.

Ila leo ukisema unatengeneza gari hatusemi ni akili kubwa kwa sababu gari imeshakuwepo hivyo unakopi tu ya watu,unatakiwa uvumbue cha kwako.

Mkuu kama kuna sehemu hujaelewa usisite kuuliza maana sote tunajifunza kwa kubadilishana mawazo
Ila mkuu hii akili kubwa (uwezo wa kufanya makubwa) huwa inatokea tu acidentally (gifted kwa mtot) ama kuna factors?
 
Sijui wenzangu mnaelewa nini kuhusu akili.

Kwa upande wangu nasema akili haina uhusiano na malezi, akili ni akili tu, mtu anazaliwanazo(karithi kutoka kwa wazazi).

=>Pia binadamu tumezidiana uwezo wa kiakili, usije ukafikilia kua kipindi watoto wanazaliwa huwa wanakua na akili sawa hapana.

=>Mazingira ya malezi ambayo mtu anayokulia yanazaa kitu kinaitwa ustarabu.(Eksipozya ya mtu itapelekea kua au kutokua na busara).

Mtu kua mstarabu wa ushuani, malezi bora haina maana ndio anaakili wapo wenye uwezo mkubwa wa akili na wakawaida, hivyo hivyo hata uswahilini.

Mtu kutokua mstarabu haina maana ndio hana akili ( mtu anakula bangi matusi wizi nk) lakini akili zimo, na wapo ambao wakawaida pia.
Mfano; 20% na Sele,

=>Duniani huko kuna waharifu/wauwaji na majambazi wanauwezo mkubwa wa akili ila ndio hivyo tena ustaarabu ni zer0.
Nimekupata vizuri mkuu

"Kuna akili na ustaarabu ni vitu viwili tofauti"

Ila nimegundua kutumia akili vizuri nayo ni sehemu ktk ustaarabu
 
Ila mkuu hii akili kubwa (uwezo wa kufanya makubwa) huwa inatokea tu acidentally (gifted kwa mtot) ama kuna factors?
Kwa muono wangu naweza kusema kuwa asilimia kubwa ni factors.

Na hizo factors kwa uono wangu watu wengi hatuzijui.

Na bahati mbaya kwa uono wangu nahisi hizo factors zinaanza kutengenezwa tokea mtoto anazaliwa pale mpaka umri wa kujitegemea kwa kila jambo kwenye miaka 7 mpaka 10 hivi.

Shida ni kwqmba wazazi wengi wanadhani kulea mtoto kunaanzia miaka mitatu pale akianza kuongea na kutembea,kumbe pale anatakiwa wwe amepata misingi ama factors mbalimbali za kukuza ubongo wange na kumfanya awe mtu wa kuhoji sana.

Na hapa kwenye kuhoji ndio kuna siri kubwa ya akili kubwa.

Bila kuhoji ama kujiuliza hupati vumbuzi yoyote ile.

Sasa mtoto kitu kikubwa anachotakiwa kutenegenzewa ni kufundishwa namna gani awe ni mtu wa kuhoji mambo tokea akiwa na umri wa siku moja mpaka miaka ambayo ataweza kuongea lugha mama kwa ufasaha.

Kuna msemo napenda kuutumia kwamba "mtoto akishajua lugha kwa ufasaha basi ameshajua kila kitu kinachohusu maisha yanayomzunguka"
 
Poa nimekupata vzuri mkuu
 
Katika hili sijafanyia utafiti hivyo sina haki ya kusema. Ila...
Hahah Mkuu ujue tayari umeshasema kwa sababu unathibitisha kwamba wana akili lakini hawajapata mazingira rafiki,hapa umeshasema.

Nataka kujua umetumia kipimo gani kujua wana akili ama umeassume tu ?

Au hujafanyia utafiti njia uliyotumia kujua wana akili lakini unajua kama wana akili ?

Kwa akili tu yakawaida ukifikilia utaona watu wenye uwezo mkubwa walikuepo wapo zaidi ya hawa tunaowatambua na watakuepo ila kwenye kufahamika sasa.
Mkuu nataka kujua unatumia njia gani kujua kwamba wana akili kubwa lakini hawafahamiki ?
Naweza kusema nimejua kutokana na kigezo kwamba hakuna equal chance,
Pale ulisema hujafanya utafiti hivyo huna haki ya kusema,hapa unasema unaweza kujua kwa kigezo kwamba hakuna equal chancr hapa maana yake kutokuweko na equal chance ndio kigezo ulichotumia kujua mtu mwenye akili.
Mfano; hawa waliofika vyuo vikuu kuna Wa kawaida na wenye akili kubwa haina maana kuwa wasiofika vyuoni hawana akili kubwa, wengi walikosa fursa.
Haya nakuuliza mkuu Watu waliofika vyuo vikuu wale wenye akili kubwa utawajuaje na wale wasio na akili kubwa utawajuaje ?
 
Hahah Mkuu ujue tayari umeshasema kwa sababu unathibitisha kwamba wana akili lakini hawajapata mazingira rafiki,hapa umeshasema.

Nataka kujua umetumia kipimo gani kujua wana akili ama umeassume tu ?

Au hujafanyia utafiti njia uliyotumia kujua wana akili lakini unajua kama wana akili ?

Mkuu nataka kujua unatumia njia gani kujua kwamba wana akili kubwa lakini hawafahamiki ?

Pale ulisema hujafanya utafiti hivyo huna haki ya kusema,hapa unasema unaweza kujua kwa kigezo kwamba hakuna equal chancr hapa maana yake kutokuweko na equal chance ndio kigezo ulichotumia kujua mtu mwenye akili.

Haya nakuuliza mkuu Watu waliofika vyuo vikuu wale wenye akili kubwa utawajuaje na wale wasio na akili kubwa utawajuaje ?
Matendo yao mkuu, kupitia action zao... ule uchap wao kuchambua mambo na kutoa/kutatua tatizo katika njia sahihi zaidi. (Mtu anakua na mambo lukuki kichani kupitia hayo mambo mtu Anaya-organize anaya-link kuendana na tukio husika na kufanyia kazi kwa muda mfupi).

Kama kuna tatizo linahitaji ufumbuzi. Mtu kwa kawaida anakuaga na taarifa mbalimbali labda tufanye trillion 10 kichwani ila zinazohusiana na hilo tatizo zipo laki moja na zipo randomly na alijifunza nyakati tofauti tofauti....

Sasa kwamtu mwenye uwezo mkubwa wa akili anazipangilia hizi taarifa ndani ya muda mfupi na kuja na maamuzi yaliyo sahihi. Wenye upeo/akili yakawaida itawachukua muda kidogo na pengine wasijue cha kufanya kabisa.
 
Matendo yao mkuu, kupitia action zao
Ndio maana nikasema akili ni matokeo ya matendo ya mtu ama maneno.

Na wewe umekubaliana na mimi kwa kusema unawajua kwa matendo yao au action zao kuwajua watu wenye akili.

Na hiyo ndio mantiki ya kukuuliza.

Bila matendo maa matokeo yenye kuonekana hatuwezi kujua akili kubwa ya mtu.

Kwa hiyo akili kwa uono wangu haitenganishwi na matokeo,lazima tuone matokeo tujue akili yako.
 
Ni sawa kabisa mkuu... na ndio wengi walikosa chance yakuchunguzwa.

Pengine walikosa kiki/ushawishi katika harakati zao.
 
View attachment 1929013

Chukulia mfano mimi na wewe tumezaliwa leo, mimi baba yangu anaishi Masaki wewe baba yako anaishi Buza,

Hilo kabati tupu lisilo na kitu ndio sawa na ubongo, yaani mimi na wewe tupo ktk stage moja.

Baada ya miaka minne mimi nkapelekwa DAY CARE nkaanza kufundishwa kusoma kuandika n.k means naanza kupanga vitu precious kwenye kabati langu (ubongo), wakati huo wewe ndugu zako wanaenda pamoja nawewe wanakubeba mgongoni kwenda kuangalia vigodoro na singeli za akina Meja kunta, means kwenye kabati lako (ubongo) unapanga singeli mimi napanga elimu,

BAADA YA MIAKA 25
Mimi nina elimu ya chuo kikuu baba yangu alinipereka Havard, now nimeajiliwa B.O.T
Kabati langu (ubongo) kuna mambo mazuri mazuri kama vile elimu n.k
View attachment 1929019

Wakati huo wewe elimu yako ni ya kidato cha nne, wavuta bangi wote mtaani unawajua, nyimbo zote za akina Manfongo unazijua yaani kwenye kabati lako (ubongo) kuna usseles material

View attachment 1929024

TUKISIMAMISHWA MIMI NA WEWE TUKAAMBIWA TUTOE MAONI KUHUSU jambo flani mimi nitakuwa kwenye nafasi nzuri ya kutoa maoni positive kwa sababu kwenye kabati langu kuna vitu muhimu, ila wewe utaishia kuongea vitu ambavyo havina mashiko maana kwenye kabati lako kuna singeli na vitu vingine visivyo na tija

Umeelewa????
Mhh hata Mimi nimekuelewa
 
Akili nikuwa wakwanza mpaka wakumi darasani kisha ukaja ajiliwa na wale wakumi mwisho mpaka wamisho darasani ambao hawana akiri. Au nasema uongo
 
Back
Top Bottom