Kuna "Uasi" wa Wabunge wa CCM unaendelea?

Kuna "Uasi" wa Wabunge wa CCM unaendelea?

Hivi commercial bank waganategemea pesa ya serikali au wamiliki wa bank hizo wanamitaji yao...maana niliskia jamaa akilaumu serikali kupeleka makusanyo yake BOT
Hapo ndio ugomvi. benki zetu ni za kimagumashi wanataka hela ya serikali ndio wafanyie biashara hata kuikopesha serikali yenyewe bafala ya setikali kufanya miradi ya maendeleo.
 
Mi nimsifu Magu kwa kubana pesa. Hakika wabunge wasingeamka kama wagekuwa na posho ndefu. Asante J. Kaza kotekote tusome namba ili wabunge waisimamie serikali sawasawa.

Posho za wabunge zimefutwa? Si zipo?
 
Unamaanisha nini kuwa muwazo aisee
Anajua kuchanga karata zake yule Mzee Mamvi.. Na Wabunge sasa hivi Wana njaa huku Bunge halina fedha za kutolea copy karatasi... ikumbukwe Naibu Spiker alirejesha billion Sita kwa Magufuli nae raisi bila ajizi akazipangia kazi pesa za bure yayo.

Mapinduzi Daima ila yasijemgeukia tu yeye maana hicho chama ajue ni cha kimapinduzi pinduzi
 
Hahahahah ngoja wakasulubiwe kama wale wa kipindi kile wakapoteza majimbo yao
 
Kuna kitu wanataka.

Watapewa na watakuwa wapole back to ndiyoooo.
 
Jamani kumekucha! Kumekucha mapema kuliko tulivyodhani. Naam Asanteni Wabunge wa CCM ambao mmetoa sauti zenu wazi wazi kuonyesha kutokukubaliana na hali ilivyo. Ukweli wenu japo unakuja kwa kuchelewa lakini asanteni; huenda ukabadilisha baadhi ya mambo. Asante Bashe, Asante Masele, Asante wale Wabunge wote wa jana kwa nguvu moja waliompinga Jenista na "surprise" zake.

Je huu sio "uasi" kwa chama tawala????? Je haiwezi kuwa mwanzo wa kupata maendeleo ya kweli??? Hope hamtaitwa kwenye vile vikao vyenu na kusulubishwa. lakini pia hongera Lema naona somo la juzi limepenyeza mahali pake. "Uasi" wenu ndio utaokoa taifa hili. Hongereni
Somo gani?
 
Hakuna uasi wala nini. Tatizo wameshtuka kuwa mamilioni yao waliyotumia kununulia ubunge hayatarudi kwa kibano hiki. Na hata hiko kidogo wanachopata (posho ya makalio) inaweza kuondolewa pia mbele ya safari.

Zile rushwa za wafanyabiashara na taasisi (mfano wa zile alizokuwa anakusanya Jairo wa nishati na madini) sasa hazitapatikana tena.

Wabunge Wa ccm walipewa sana hizi kutokana na wingi wao.

Ahsante Magufuli endelea kuwakazia.
 
Tukiendelea kuchagua chama cha majipu tutatawaliwa hata na vichaa.wehu.machizi.mateja.majangili.mafisadi .magaidi na nk.sijui sasa hivi tupo fungu lipi mana mbunge jangili kakutwa na bunduki kibao
 
Huenda ni ujao wa lowassa na sumaye bungeni
 
Kwa mwendo wa wabunge wa ccm kuiponda serikali yao hali ya mambo haitakua shwari kwa viongozi watukufu sana!! Kama sio kinana bas mkuu mwenyewe atafanya kikao na wabunge kuwapunguza kasi watu wao. Hili halitakua jipya mara kadhaa ikitokea hali kama hii viongoz hutokea dodoma kuweka mambo sawa!

Mwendo huu wa ukosoaji lazma nape asemelee!! Yaan JPM kukosolewa hivi hawez vumilia. Sijafikilia kama Dada Tulia atatulia bila kusema kwa mkuu wa kaya!!

Maana kwa mwendo huu wale wenye kazi ya kumsifia mfalme watakosa nafasi ya kuchangia. Katikati ya michango ya wabunge kama Bashe na Ahmed ally Lusinde ataongea cha maana kipi hadi wabunge wampigie makofi?? Yaan nawahakikishia Lusinde na wengineo wale wa kusifia wataomba kuchangia wiki ijayo.

Ushauri kwenu wabunge, msikubali kupigwa mikwala, nyie akina jecca wakat mwingine hushindwa kuwabeba mtaenda na maji. Mkuu anaweza kuwa na nafasi kubwa ya kupewa ushindi wa mezani!! Kingine maisha magumu hayachagui wewe chama gani!! Haya ngoja twende!!
 
Ni vizuri wakiombwa waache kuisimamia serikali kwa uadilifu kwa sababu watakuwa wamerudi kwenye misingi yao mikuu ya wizi na ujambazi as usual so tutakuwa tumerudi kulekule.
 
Back
Top Bottom