Kuna "Uasi" wa Wabunge wa CCM unaendelea?

Elli

Platinum Member
Mar 17, 2008
55,520
86,081
Jamani kumekucha! Kumekucha mapema kuliko tulivyodhani. Naam Asanteni Wabunge wa CCM ambao mmetoa sauti zenu wazi wazi kuonyesha kutokukubaliana na hali ilivyo. Ukweli wenu japo unakuja kwa kuchelewa lakini asanteni; huenda ukabadilisha baadhi ya mambo. Asante Bashe, Asante Masele, Asante wale Wabunge wote wa jana kwa nguvu moja waliompinga Jenista na "surprise" zake.

Je, huu sio "uasi" kwa chama tawala? Je, haiwezi kuwa mwanzo wa kupata maendeleo ya kweli? Hope hamtaitwa kwenye vile vikao vyenu na kusulubishwa. lakini pia hongera Lema naona somo la juzi limepenyeza mahali pake. "Uasi" wenu ndio utaokoa taifa hili. Hongereni
 
Yaani huyu rais tunamchagua anakuja kututesa hivi? Haya yote ya uchumi na hali mbaya chanzo ni yeye.
 
Kazi ya bunge ni kuisimamia serikali. Walipokuwa kwenye dunia ya posho n.a. kujilipa walijisahau sana.
 
Mkuu Elli, ungeleta flashback ya kile walichosema hao wabunge ili na sisi tulio mbali na media tujue kama kuna uasi na mgawanyiko kweli ndani ya chama tawala, chama la rangi ya njano na kijani, au na wabunge wamekatiwa mirija ya kutafuna? Manake ukiona mwana CCM analalama ujue tu amenyumwa "fursa"!!!
 
Mi nimsifu Magu kwa kubana pesa. Hakika wabunge wasingeamka kama wagekuwa na posho ndefu. Asante J. Kaza kotekote tusome namba ili wabunge waisimamie serikali sawasawa.
 
Je, huu sio "uasi" kwa chama tawala?
Huu sio uasi wala usaliti ni kujitambua. "Uasi" mara nyingi unapotokea au kufanywa kwenye nchi iwe wanasiasa,vikosi ay jamii ni kosa la jinai. Lilio fanyika ni kwa wabunge wa CCM ni kuzinduka, kujitambua na kuanza kuthamini wajibu wao kwa Taifa na watu walio wachagua/wanao wawakilisha
Waliongea nini?
Wengine hatuna taarifa!
Usipoteze muda mwingi kwenye Maskani. CCM waliliona hili ndio maana wakapiga marufuku matangazo ya moja kwa moja kutoka bungeni.

.
 
Asante sana kwa ufafanuzi mzuri ndio maana neno UASI nililifungia, nikiamaanisha kuwa wamejitambua ila kwa upande wa pili ni UASI
 
  • Thanks
Reactions: BAK
1478090208326.jpg
 
Back
Top Bottom