Kuna tukio la kishirikina liliwahi kunitokea miaka kama 20 iliyopita na limebadilisha maisha yangu

Mambo gani yanayoshabihiana na kujirudiarudia?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jaribu kuwaona na kuwaeleza yanayokusibu kifikra, wataalamu wa Masuala ya afya ya akili na saikoloji.
Wanawezavkukupa amani unayotaka kuhakikishiwa juu ya maisha yako.
Mpaka leo kukumbuka baibui, je unakumbuka abiria wengine walivaa nini?
Pengine ulimtolea macho mpaka mwenyewe akagutuka, na kutaka kukutanabahi kwamba, ' acha kunitolea macho', ndio akakugusa machoni, kutenda ambacho sio cha kawaida na hukukitegemea. Ndio ikakufanya uzidi kuchanganyikiwa zaidi. Yaliyofuata baada ya hapo, nina imani wataalamu watakusaidia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vua uhoga na dhana dhaifu,mabadiliko yako kwako mwenyewe
Hawa wanaokejeli ndio wachawi wenyewe ,wewe unaposema uchawi haupo unataka kutuaminishisha shetani hayupo?Ili muendelee kuroga watu vizuri. Misingi ya dini zote ni kumpinga shetani.Mtu mzima kufikia kuleta uzi hapa ujue amepambana alivyoweza imeshindikana.
Washirikina wengi wanatumia nyota za watu kujipatia mafanikio.
Ndugu mleta mada endelea kuomba,shirikisha watu unaowaamini muombe pamoja,mmoja hufukuza maelfu ,wawili hufukuza makumi elfu.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Una maana huyo mchawi alikuroga wewe na familia yako? You're being delusional mkuu, usitafute mchawi wakumpa lawama sababu uchawi wenyewe haupo pambana.
Ninyi ndo wachawi wenyewe una uhakika uchawi haupo uko dunia gani? Acha uchawi Mungu anakuona.
 
Kama hujawahi kulogwa usicomment. Maisha yana tiba mbalimbali usidanganywe nenda kwa waganga pia nyumba za Ibada bora usiende kwa nia ya kudhuru mtu. Wote ni wa Mungu. Tumedanganywa na wazungu kwa maslahi yao.
 
kijana nenda kwa watu wa saikolojia wakakutibue uwe sawa naona unalaumu kila kitu... nadhani huo urefu wa story yako ndo changamoto ya maisha yako, kuna muda wa ku focas mbele.. mbali...
 
Kama hujawahi kulogwa usicomment. Maisha yana tiba mbalimbali usidanganywe nenda kwa waganga pia nyumba za Ibada bora usiende kwa nia ya kudhuru mtu. Wote ni wa Mungu. Tumedanganywa na wazungu kwa maslahi yao.
Hivi katk hiyo story umeona proof ya yeye kurogwa? Watu hawakatai kama hakuna uchawi, ila kwa alichojielezea yeye uchawi hauonekani. Hiyo taaluma ina misingi yake mkuu, Haiendi kwa hisia tu.
YAANI KAMA KAROGWA SIYO KATIKA TUKIO HILO. Kwanza aeleze vizuri aliachaje shule.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unasema hivyo kwasababu tukio limehusisha baibui? Wakati watu wa vazi hilo ndio wenyewe kwa yale mambo. Acheni ujinga kuna tatizo hapo na msaada unahitajika. Ndugu nenda kwenye maombi ya watumishi wa Mungu aliye hai, YESU KRISTO na utapona kabisa.
 
Unasema hivyo kwasababu tukio limehusisha baibui? Wakati watu wa vazi hilo ndio wenyewe kwa yale mambo. Acheni ujinga kuna tatizo hapo na msaada unahitajika. Ndugu nenda kwenye maombi ya watumishi wa Mungu aliye hai, YESU KRISTO na utapona kabisa.
Unajua ukiumwa ukaenda hospitali hushangaaji dr ana kukuuliza maswali ambayo kwa kawaida unawza kuona hayana uhusiano na ugonjwa wako? Mfano unaishi wapi? Unafanya kazi gani? Mara ya mwisho umekula nini? Unatumia mafuta gani ? Umeolewa? Una mpnz?
Ulishajiuliza niini msingi wa hayo maswali with relation na ugonjwa wako?
Sasa yeye mhanga wa baibui haya na hao ndugu zake huko nyumbani ambao ni wakubwa kuliko yeye? Nao walipitiwa na baibui?
Muulize vizuri akuelezee maisha ya familia yao kabla ya kuzaliwa kwake, kisha akuelezee maisha yako toka alivyo darsa la kwanza. Akupe maisha toka anaanza chuo na mahusiano. Yachanganua kisha utaona tatizo la mshikaji.
TATIZO LAKE LIKPO KICHWANI MWAKE YEYE MWENYEWE. HAJAROGWA.
Uchawi una kikomo cha muda kwanza ujue.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtoa mada yaani mtu akutie vidole machoni unamwangalia tu!
Ingekuwa mimi ndani ya dakika 2 hana meno yote ya mbele

Sent by Diaspora
 
Hapa umenena mkuu, nyie ndio mnatakiwa katika jamii na kuonesha mmekomaa kiakili kuliko hao wengine wanakuja kwa kejeli kusema mleta mada ni muongo... Ulichosema ni sahihi kabisa, sometimes mtu anahisi amerogwa kisa mambo hayaendi na familia imevurugika ila kumbe tatizo hata sio kulogwa ni mfumo wao mbovu wa uendeshaji wa maisha yao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Pole kama ni kweli, na naomba kinachokuumiza kisiwe hiko cha wenzio kuitwa waheshimiwa, maana hapa ndio naona kuna kiini cha wewe kuteseka na si uchawi,
Ushauri, kila mtu amezaliwa akiwa na bahati yake ya mafanikio, wapo wanaozaliwa nakukuta mafanikio yako ndani ya familia, wapo wanaozaliwa nakukuta familia haina kitu na wao wakawa chachu ya mafanikio,
Fahamu kwamba kila mja anabahati yake ambayo huja kwa wakati wake, hata kama si kesho ikawa uzeeni mwako ndio ulipangiwa utoboe ukiwa na miaka hiyo 60 or 70.

Riziki hugawiwa na Mungu binadamu huizuia tu
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…