Kuna tatizo kubwa sana IKULU

Kuna tatizo kubwa sana IKULU

Waziri mkuu alisemaje baada ya Rais kushauri kuhamia Dodoma?
Amesema anataka Dodoma iwe kisiwa cha amani.

Hivi huyu Majaliwa ni mzima kweli? Dodoma iwe kisiwa cha amani, halafu kwingine kuweje, Syria?
 
Wizara zitahama lakin ikulu kuhamia Dodoma *HAIWEZEKANI*
Changamoto kubwa nayoiona ni suala la ulinz na usalama,Landlocked countries znataman sana uwepo wa bahari ktk nchi zao, lkn sisi tunataka tupuuze hilo.Dodoma itabaki ikulu ndogo tu lkn main campus ni magogoni

acha utoto ww, mbona kenya kuna bahari lakini mji mkuu ni nairobi na sio mombasa au lamu.
 
Siyo lazima serikali iwe Dar es Salaam. Hivyo kuhamia Dodoma ni sahihi tu. Wala jambo hilo halitaathiri jiji la Dar kwa kuwa bado litaendelea kukua kibiashara. La msingi hapa ni nini kifanywe ili Dodoma ikidhi mahitaji ya Mji Mkuu wa Taifa letu wakati kazi hiyo ilidharauliwa kwa miaka 30
Kwa mawazo yangu kuhama ni gharama, nadhani hakuna aliyedharau bali nafasi kipesa imekuwa haipatikani. Je kwa sasa ipo hiyo nafasi?Na kwa muda huu miundombinu ya kuhamia ipo, kama mkuu ataweza yeye kuhama na wengine kuchelewa watakuwa wamejifuka kazi?Malipo kwa watumishi watakao hama yapo, kama yapo haya ingilii mipango mingine. Majibu haya nadhani haya maswali ndy yanaleta mjadara huu kila kona ya nchi.
 
Kitu pekee kinanipa amani ni kua SIKUMPIGIA KURA mtu huyu wala chama chama chake mimi sio sehemu ya tatizo hili.
 
Mimi ningekuwa magufuli. Ningefanya kuhama kwa awamu. Ningehakikisha kuwa,barabara na miundo yote muhimu inapewa kipaumbele bila kuumiza bajeti kuu. Pili,ningehakikisha raisi ajaye anakuwa na makazi dodoma na sio kuhama ndani ya miezi michache. Huyu mtu hana akili,au haziko vizuri.
 
Amesema anataka Dodoma iwe kisiwa cha amani.

Hivi huyu Majaliwa ni mzima kweli? Dodoma iwe kisiwa cha amani, halafu kwingine kuweje, Syria?

Waandikiwe hotuba na wazisome.
 
Mkuu, kuna computer sikuhizi, hakuna anaebeba wala kutumia mafaili ya karatasi.

Serikali inatumia hardcopy kwa asilimia 80%. Hizo nyingine ni email tu.

Ukiandika barua kwenda serikalini watataka upeleke hard copy
 
Mkuu, nashukuru tuna mawaza yanafanana maana kuna mahali nimesema kuna tatizo nchini na watu wanaweza kukataa lakini ukweli kuna tatizo!

Watanzania hatuna uwezo wa kupambanua pumba na mchele.
 
Hahaaa, nyie mtaonekana hamumtakii mema huyo jamaa yenu! Mkulu wenu keshaona ikitokea sunami ikafanya ziara ya kushtukiza hapo bongo atakuwa wa kwanza kulambwa! Halafu mkumbuke kule Dom chama cha mang'ombe kinaungwa mkono kiasi chake. Ila kubwa anakimbia majanga ya sunami...!
 
Eventually if you fail you planned to fail!!!
You may fail not because you planned to fail; rather your plans did not factor in "failure and therefore strategic fall back position in case of failure of plan A"!!
 
acha utoto ww, mbona kenya kuna bahari lakini mji mkuu ni nairobi na sio mombasa au lamu.
Hahaha pima utoto wako sasa,
Tanzania mji mkuu wake ni Dar es Salaam ambako kuna bahari au mji mkuu ni Dodoma?
Ungegusa suala la ikulu ya kenya na kunipa vigezo vya kutosha ningekuona wa maana sana.
Karibu mkuu
 
Kitu pekee kinanipa amani ni kua SIKUMPIGIA KURA mtu huyu wala chama chama chake mimi sio sehemu ya tatizo hili.
Pole sana kwa mawazo yako mkuu, kumchagua au kutomchagua hakutaweza kumfanya asiwe Rais wako wala hakutafanya usiguswe na maamuz yake atakayofanya kwa nchi,ndomana hata leo umeguswa mpaka ukasema hukumchagua.
Penda nchi yako
 
Kuna tatizo kubwa sana Ikulu.

Ndio Ikulu nzima na watu wote wanaomzunguka rais katika shughuli za kila siku.

Ina maana hawatambui "Urais" ni taasisi kubwa na nyeti kuliko zote nchi nzima?

Ina maana hawatambui kuwa anachoongea au kutenda rais ndo sauti na matendo ya Tanzania nzima?

Inakuwaje wanamuacha rais atoe hutuba ngumu na zilizojaa utata kila siku? Hana washauri wa kumuambia anakosea?

Mfano, anasema akihamia dodoma atauza majengo yote ya serikali Dar es Salaam, kwa hii kauli unadhani anafikisha ujumbe gani kwa jamii ya watanzania na wasio watanzania wanofuatilia siasa za tanzania? Niambie serikali yeyote duniani inayouza majengo yake hasa kwa sehemu 'potential' kama dar es salaam? Na huko Dodoma atajenga au atakodi pia? Nyumba za serikali ziliuzwa, kipi kilipatikana baada ya hayo mauzo? Unahamia Dodoma kwa bajeti gani uliyoitenga? Hao watakaohamia wataenda kukaa wapi? Serikali ina majengo ya kupokea hizo Wizara? Wanajua idadi ya hao watakaohamia Dodoma?

Yani kila siku mapya yaanzishwa kutoka hewani na yanahitajika kutekelezwa.

Swali linakuja: Kwa bajeti ipi?

Hao washauri wanatakiwa wamwambie mambo hayaendi hivyo, serikali sio familia. Kila kitu kinatakiwa kipangwe na kutekelezwa kutokana na mpango elekezi. Jambo jipya litakalojitokeza litekelezwe bajeti inayofuatia.

Zoezi la kuhamia Dodoma linahitaji fedha nyingi sana na linatakiwa kutekelezwa kwa awamu. Ila hili la kusema hadi Septemba wawe wameshahama sio sawa kabisa. Hata hao watumishi mnawatesa na familia zao.

Pia, inavyoonekana hata hotuba zinatolewa kwa jazba au hazifanyiwi tafiti. Nimesoma sehemu anasema 'Wizara ya takwimu'. Hapa alikuwa ana maanisha nini?

Kurugenzi ya ikulu imetoa taarifa kituko haijawahi kutokea. Maswali yanakuja, inamaana wametoa kwa utashi wao kwa shinikizo?

Binafsi, nadhani Rais yupo pale kulipa kisasi na kuwakomoa watu fulani. Mtaani hali ni ngumu, biashara zinadorora. Ina maana wao hawaoni? Au wanaishi mbingu gani?

Mawaziri wanajua wanachofanya? Wana sera gani kumkomboa mwananchi wa kawaida?

Kuna tatizo Ikulu.
Umejiuliza maswali muhimu kabisa lakini hilo la biashara mitaani siungi mkono. Nionacho; biashara zote muhimu zinasonga kama kawaida. Tatizo liko kwenye biashara za uchina, india na Taiwani. Zile za kuingiza maziwa na kudai yametengezwa Z'bar. Biashara hizi zilidumu kwa kutegemea ujanja unaoumiza serikali.

Kilio cha kwanza kusikika, ilikuwa ni hoteli. Hoteli siyo mali ya serikali na wateja wa mahoteli ni kila raia. Hoteli hazikujengwa kwa PPP, kwamba serikali ilikuwa na ahadi ndani yake. Wenye mahoteli wanatakiwa wawe wabunifu. Kundi la wateja unaowategemea, likitoweka vutia wateja wengine badala ya kusari serikali ilegee!

Watumishi au waajiliwa serikalini walistahili kuwa pamoja siku nyingi na kuomba maslahi mazuri. Badala yake kilio cha mishahara kilikuwa cha watu wa chini tu! Walioko juu wakitegemea safari za per diem ya dola 450, semina, 10% ya kumbi za mikutano kwa ujumla ile bajeti iliyoitwa ni ya chai. Hii sasa imekatwa ndo mtu anashindwa kuishi jijini. Kama mafuta ya gari ulitegemea vyanzo vya aina hiyo, tafadhari tumia mabasi yeaendayo kasi ili jiji likutunze!
 
Wizara zitahama lakin ikulu kuhamia Dodoma *HAIWEZEKANI*
Changamoto kubwa nayoiona ni suala la ulinz na usalama,Landlocked countries znataman sana uwepo wa bahari ktk nchi zao, lkn sisi tunataka tupuuze hilo.Dodoma itabaki ikulu ndogo tu lkn main campus ni magogoni
Aliyekwambia Ikulu lazima iwe pwani nani?
 
Back
Top Bottom