mtazamo wangu ni kwamba, tunaposema lets say 8×3=24 katika hisabati na uhalisia ni kwamba...(chukulia mfano huohuo wa machungwa). unatoka Moro kwenda Dodoma kufuta machungwa. ukaenda trip tatu (3). Trip1 ukachukua machungwa 8. hesabu yako itakuwa machungwa 8 kwa trip moja utakuwa na hayo hayo 8. ie 8×1=8. haya, utakwenda mara(trip) ya pili utachukua nane. ukiongeza kwenye stock ya mwanzo yatakuwa 16. ie 8×2=16. utakwenda tena mara ya tatu utaleta mchungwa 8, utaongeza kwenye yale 16 yatakuwa 24. kwa hyo tunasema umefuata safari tatu na kila safari ulileta machungwa 8. kwa hiyo unamachungwA 24. (8×3=24 au 8+8+8=24).
sasa hebu fikiria. Uko Moro, huna machungwa. Dodoma kuna machungwa mengi tu. sasa unataka ufuate machungwa 8. (kumbuka wakati huo huna mchungwa ila sasa unataka kufuata.) sasa unafuata machungwa 8 mara sifuri. kwa kifupi ni kwamba hujafuta trip yoyote japo ulitaka kufuata matunda8. kwa hiyo utaendelea kuwa huna kitu. ndio maana 8×0=0 au hata 0×3=0; kwamba umekwenda Dodoma safari tatu kufuata machungwa.lakini kila safari uliyoenda hukurudi na kiru (machungwa sifuri). unadhani baada ya safari hzo 3 utakua umekusanya kiasi gani?..........