G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,555
- 35,883
Awali katika kile kilichoelezwa na BAVICHA kuwa watazuia mkutano mkuu wa CCM tuliona kilichotokea Dodoma siku chache kabla na wakati wa kikao. Tulioenda Dodoma tulishuhudia jinsi ambavyo jeshi la polisi lilijipa jukumu la kuhamishia mashine Dodoma na eneo lote likalindwa kwa ulinzi wa hali ya juu kupita kiasi.
Leo ikiwa ni siku chache kabla ya operesheni UKUTA tunaona jinsi jeshi la polisi linavyojipa mazoezi makali maandalizi ya kukata na shoka eti kupambana na watu wasio na silaha hata ya kuulia mende.
Mbona enzi za Kikwete mambo yalikuwa kawaida tu tena sana? Leo hii ni kina nani wanapambana? Kina nani wanatishana kisirisiri bila sisi wengine kujua?
Maandalizi ya jeshi la polisi, matamko yao yanaashiria kuwa kutakuwa na mpambano wa kukata na shoka kumbe ni harakati tu za kudai katiba ya nchi kufwatwa kama ilivyoapiwa! Hilo linahitaji majeshi? Labda kuna lingine!