Kuna siri nzito inaendelea nchini, nini chanzo? Kina nani wanapambana kwa siri?

G Sam

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
11,555
35,881
Awali katika kile kilichoelezwa na BAVICHA kuwa watazuia mkutano mkuu wa CCM tuliona kilichotokea Dodoma siku chache kabla na wakati wa kikao. Tulioenda Dodoma tulishuhudia jinsi ambavyo jeshi la polisi lilijipa jukumu la kuhamishia mashine Dodoma na eneo lote likalindwa kwa ulinzi wa hali ya juu kupita kiasi.

Leo ikiwa ni siku chache kabla ya operesheni UKUTA tunaona jinsi jeshi la polisi linavyojipa mazoezi makali maandalizi ya kukata na shoka eti kupambana na watu wasio na silaha hata ya kuulia mende.

Mbona enzi za Kikwete mambo yalikuwa kawaida tu tena sana? Leo hii ni kina nani wanapambana? Kina nani wanatishana kisirisiri bila sisi wengine kujua?

Maandalizi ya jeshi la polisi, matamko yao yanaashiria kuwa kutakuwa na mpambano wa kukata na shoka kumbe ni harakati tu za kudai katiba ya nchi kufwatwa kama ilivyoapiwa! Hilo linahitaji majeshi? Labda kuna lingine!
 
ccm wameifilisi nchi kabla ya uchaguzi, wamepora ushindi wa ukawa, wamemuweka mtukufu wakadhani mambo yatapoa lakini bado. sasa wanaogopa wapinzani wataambia wananchi usaninii wanaoufanya
 
daa! leo nilkuwa naongea na staff mwenzangu(umri umeenda) huwa ni ccm damu, alikuwa anataman kuona siku mojawapo kati ya zile za JK mkwere, kwamba maisha ya kazi yamekuwa magumu kuliko hata alivyofikiria((nikabaki kucheka kimoyomoyo,))
 
Maandalizi ya jeshi la polisi, matamko yao yanaashiria kuwa kutakuwa na mpambano wa kukata na shoka kumbe ni harakati tu za kudai katiba ya nchi kufwatwa kama ilivyoapiwa! Hilo linahitaji majeshi? Labda kuna lingine!

Ndio swala la kujiuliza. Kwa nini Vyombo vya dola vinapata shida na wapinzani? Kwani toka mwaka jana katika harakati za kampeni hadi kumalizika kwake kuna jambo la ajabu na la kukosesha amani limefanywa na vyama vya upinzani??? Kwa nini sasa watumie nguvu kupambana na watu ambao hawanashida ya kuanzisha vita hapa Tanzania? Kwani toka lini watu wenye lengo baya huwa wanatoa taarifa ili mjipange kupigana nao? KUTOA TAARIFA YA KUWEPO KWA UKUTA ni dalili tosha kuwa wapinzania hawataki vita bali wanataka kupewa haki yao ya msingi
 
Leo ikiwa ni siku chache kabla ya operesheni UKUTA tunaona jinsi jeshi la polisi linavyojipa mazoezi makali maandalizi ya kukata na shoka eti kupambana na watu wasio na silaha hata ya kuulia mende.

Waache wajipange tu. Kwani wanafikiri katika kundi hilo watakaowadhuru watakuwa raia tu. Watakuwepo mama zao, wadogo zao, baba zao, binamu zao, na ndugu zao kadha wa kadha. So watawaua bila wao kujua halafu baadaye waende makwao wakalie msiba.
 
Back
Top Bottom