Kuna shule Morogoro ilipokea 56,787 kwa mwaka wa fedha 2024/25 ili kufinance elimu bure

Kuna shule Morogoro ilipokea 56,787 kwa mwaka wa fedha 2024/25 ili kufinance elimu bure

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,286
Reaction score
10,831
Ili kuhakikisha elimu bure kwa shule za serikali, serikali hutoa fedha ili kuhakikisha jambo hilo linafanikiwa. Kwa data za TAMISEMI, shule ya Msingi Matambwe iliyoko Wilaya ya Morogoro, tarafa ya Kisaki, ilipokea Tsh 56,787 kwa mwaka wa fedha 2024/25. Shule hii ina jumla ya wanafunzi 18 kuanzia la kwanza hadi la saba na mwalimu mmoja.

Shule nyingine iliyopokea hela ndogo ni Shule ya Msingi Kikoboga ambayo ilipata kitita cha 69,132 kwa mwaka 2024/25 wa fedha. Shule hii ipo Wilaya ya Kilosa, tarafa ya Mikumi. Hii ina jumla ya wanafunzi 10 na walimu 7 kwa kuanzia darasa la kwanza hadi la saba.

Twende kwenye shule nyingine kwa haraka haraka kuokoa muda, hii ni shule ya msingi Sikula, ambayo iko Kilindoni, Wilaya ya Mafia mkoani Pwani. Hawa walipewa kitita cha Tsh 73,198 kwa mwaka wa fedha 2024/25. Hii inawanafunzi 41 kuanzia la kwanza hadi la saba na walimu wawili.

Achana na hizo kuna hii, Shule ya Msingi Klenk, ambayo iko Reha, Wilaya ya Rombo, hawa walipata 100,557 kwa mwaka wa fedha 2024/25. Hawa kwa mwaka 2025 hawakuwa na wanafunzi ila kuna walimu wanne.

Tumalizie ya mwisho ni-logout. Hii ni shule ya msingi Buyuni iliyoko Mkwaja, Wilaya ya Pangani, Tanga. Hawa walipata kitita cha Tsh 106,841. Hawa wana wanafunzi 26 kuanzia la kwanza hadi la saba na walimu watatu.

Baada ya shule hizo karibu kuangalia orodha ya shule zilizopokea fedha nyingi kwa mwaka wa fedha 2024/25

Shule kumi zilizopata hela nyingi
Halmashauri
Jina la Shule
Jumla
Temeke MCMBANDE
40,714,109
Temeke MCMSUFINI
38,500,789
Temeke MCCHAMAZI
34,000,859
Arusha CCMURIET DARAJANI
33,076,991
Temeke MCMAJIMATITU
31,657,818
Temeke MCMBAGALA KUU
29,041,915
Geita DCIBOZYAMAGIGO
27,634,341
Geita DCNTINACHI
27,602,916
Dar es Salaam CCKIMWANI
26,873,878


Shule kumi zilizopata hela chache.

Halmashauri
Jina la Shule
Hela iliyopewa
1
Morogoro DC
MATAMBWE

56,787
2
Kilosa DC
KIKOBOGA

69,132
3
Mafia DC
SIKULA

73,198
4
Rombo DC
KLENK

100,557
5
Pangani DC
BUYUNI

106,841
6
Makambako TC
IKELU.B

142,964
7
Siha DC
NURU ENGLISH MEDIUM

157,120
8
Bagamoyo DC
KALIMENI

165,920
9
Makambako TC
KIBEDANGE

179,486
10
Mvomero DC
WAMI VIJANA

182,259

Data Source: Home
 
Shule ina wanafunzi 10 kuanzia darasa la 1 hadi 7? Halafu ina waalimu 7.

Shule yenye wanafunzi 41 inakuwa na waalimu wawili.

Waziri wa elimu alikuwa mtaalamu wa mifugo au nini
 
Itoshe kuwaambia matako yao hao fiisieemu wanaboa sana yaani hakuna wanachoweza hata kimoja wanasifiana tu.
 
Kwahy hyo shule isiyokuwa na wanafunzi na ina walimu ,je hao walimu kazi yao ni ipi?
 
Kuna shule zingine raha sana. Shule inawanafunzi 41 kuanzia lakwanza halafu ya serikali..Wakati maeneo mengine darasa la tatu wanafunzi 80.
 
Hizo pesa wanafanyia nin mbona za bia tu jamani😀
 
Back
Top Bottom