Kuna shida kubwa ya akina mama na mabinti kupenda kula chipsi mayai

Elimu inatolewa kwenye Tv kuna makala za afya kila siku. Dr janabi nae anasaidia...
Serikali ishindwe kupiga marufuku utengenezaji na uvutaji wa sigara ambao madhara yake yapo wazi wajikite kwenye chips mayai kweli?
Unakubali kua junk food ina madhara?
 
Chips na mayai ni combination nzuri zaidi kuliko atakayekula ugali na maharage.

Ndio..

Viazi ni wanga na ni easy kuwa digestible kuliko ugali wako mgumu.

Mayai hasa ya kienyeji yanavirutubisho vingi.. pia umegusia kuwa hawali mboga za majani.

Tunarudi jikoni, chips yai kuna ubunifu wa kutiwa carrots na hoho ambazo hazikwivi sana. Pia Kachumbari inayofata huwa ina mchanganyiko wa carrots, tango, vitunguu bila kusahau vikorombwezo vingine kama Mayonnaise, ukwaju, Tomato etc..

Nachelea kusema wanapata chakula Bora sana.. tatizo ni UBORA wa maandalizi ya upishi, na materials hasa MAFUTA.
Hii ndio akili kubwa tunazozihitaji kama taifa.

Mimi nitaongezea: Kwambaa; katika ulaji mzima wa chipsi yai, ambacho hakifai kiafya sio viazi wala sio mayai........ bali ni ile soda au juisi utakayoongezea. Lakini lawama zote kwa chipsi yai.

Viazi ni chakula bora✅
Na mayai ni chakula bora✅

Sasa ubaya upo wapi ndugu zangu.
 
Uchunguzi wangu huru umeonesha akinamama na mabinti walio wengi wamekuwa wapenzi wakuu wa kula viazi vya kukaanga vinavyochanganywa na mayai maarufu kwa jina la chips mayai.

Ukitaka kuhakikisha hili wewe ingia sehemu yoyote ya kula na uchungulie mezani vilivyoagizwa, utaona asilimia kubwa ya akinamama na mabinti ni chips mayai na wengine wanaongezea nyama choma au mishikaki na wengi wao unakuta hawapendi mboga za majani.

Lililo wazi ni kwamba watu hawa hawali chakula bora. Na kama hata huko majumbani kwao wanakula hivi basi kama taifa tuna janga kubwa kwa kizazi cha huko mbeleni maana hawa ndo mamazetu wa sasa au baadaye.

Sasa kwa ulaji huo tutakuwa na kizazi cha namna gani hapo baadae. Wizara ya Afya Tanzania angalieni jambo hili kabla hali haijawa mbaya.
Kila mtu ashinde mechi zake wazungu mamiaka mengi wamekuwa wakishindia mikate tu wanabadili majina tu sijui pizza, baga sijui nini ila ni mikate tu na wapo miaka nenda rudi.
 
Back
Top Bottom