Kuna sababu gani Tanzania kuendelea kuwa na wabunge wa viti maalum?

The Evil Genius

JF-Expert Member
Mar 21, 2014
5,576
17,704
Nchi masikini kama Tanzania ambazo zaidi ya 40% ya mapato yake ya kuendeshea serikali yanatokana na mikopo na misaada, zina idadi kubwa sana ya baraza la mawaziri pamoja na bunge.

Kuna kipindi Tanzania tuliwahi kua na baraza la Mawaziri zaidi 60.

Hoja yangu ni kwamba, kwa nini bado tunaendelea kua na wabunge wa viti maalum karne hii ya 21? Tunachagua wabunge kwenye uchaguzi mkuu, bado vyama vinaleta wabunge wa viti maalum na bado rais analeta wabunge wake 10.

Dhana ya viti maalum ilikua ni kuwasaidia watu walio kwenye makundi dhaifu kama walemavu wa viungo ama special groups au marginalized groups. Sasa leo mtu ana PhD anafundisha chuo kikuu anaenda kugombea viti maalum na anashinda eti yeye pia ni special group au marginalized groups, unajiuliza hivi watanzania tunawaza sawasawa kweli?

Leo wanawake hawataki kujishughulisha kupambana kuomba kura tena wasomi wakubwa na wenye ushawishi wanaenda kupigana vikumbo kwenye viti maalumu na walemavu ambao hawana fursa sawa na wao.

Nimeshangaa hata feminists ambao hua wanaamini mwanamke anaweza kila kitu na wao wameenda kugombea viti maalum, kwamba hawawezi kitu na hawajiwezi.

Kwa hali ya sasa ya viti maalumu, je kuna haja tena ya hivi viti kuendelea kuwepo?
 
Viti Maalumu ni Maalumu kwa hao Maalumu
Huo ni uwanja acha Maalumu wapambane unaweza kumuona mtu ni Dr au Prof. lakini haiondoi umaalumu wake.

Ninachokiona hapa umaalumu upo ndani ya mtu na sio mwonekano au vile tunavyomuuona

I think hata wanaume wapo walio Maalumu ingawa haipo wazi saana kama ilivyo kwa hawa wenzetu
Acha Maalumu waitwe Maalumu
 
Umeongea point sana.....wanaamini wanawake wanaweza halafu wanataka special seats
 
Hapa mi naona ni kama viburudisho vya wakubwa Fulani, maana wengi wao huwa ni wanawake pia kati yao wengi huwa wana sura nzuri, so hivi viti maalumu ni maalumu kweli kweli kama alivyosema mdau hapo juu!
 
Hii ni sawa kabisa
Akina sisi tusiokuwa na vyama ,sijui lini tutafikiriwa.
 
Hata idadi ya majimbo ya uchaguzi ni mengi Sana. Yaani majimbo 250+ yote ya Nini. Walau tungefanya kila wilaya itoe mwakilishi mmoja tuachane na majimbo.
 
Back
Top Bottom